Brevis Bei nafuu. WHY?

Brevis Bei nafuu. WHY?

Daah mil 5 na bado inataka matengenezo?Hio jau tayari mzee baba.
Duh km vile unanishtua na Hio jau. Maana leo wameshuka hadi 4M eti wamenipunguzia za matengenezo au nikanunue engine nyingine kwa 1.5M Ilala.

Sasa bado AC na ma umeme hapo mng'ato naingizwa choo cha kike nikakabiziwe mzoga
 
duh km vile unanishtua na Hio jau
maana leo wameshuka hadi 4M eti wamenipunguzia za matengenezo au nikanunue engine nyingine kwa 1.5M Ilala
sasa bado AC na ma umeme
hapo mng'ato naingizwa choo cha kike nikakabiziwe mzoga
Mzee baba hapo kimbia fasta sana,wanataka kukushikisha kimeo hao jamaa.

Mil 4 mpk 5 hapo unapata Brevis imesimama mbaya kabisa na haina kasoro hata moja mkuu Ukwaju .
 
Crown ghafla limekua Yebo Yebo.
Kweli mkuu...ila sabau kubwa nadhani ni vile Watz tunapenda mambo ya fashion.
Magari mengi ni fashion ikishapita inakuwa yeboyebo.

1. Nianze na GX 100 chaser, mark ii na cresta.
2.Tukaja GX 110
3.Verosa haikufanya vizuri saana
4.Brevis nayo ilivamiwa sasa hivi watu wanaikimbia kama ukoma
5.Mark x hapo napo watu kibao walikimbilia ila bado inafanya vizuri.

6.Crown ndiyo kila mtu anakimbilia hapo na wanazi company kwa kufuga ndevu...yaani sasa hivi ujanja ni kufuga ndevu nyingi kisha ukae ndani ya crown.

7.Tako la nyani lilikimbiliwa saaana lakini sasa hivi naona wanaume wengi wameamua kuziacha kwa wadada...wadada wanapendeza sana wakikaa humo.

8.IST hapa ndiyo balaa...hii imekuwa kama sare sare za vijana wa kiume na wakike wanaochipukia maisha....Kuigana nadhani ndiyo sababu kubwa...

Kwa upande wa Subaru naona

1.Impreza kama vile imevamiwa na watu wanaichukulia kama mvadala wa ist.
2.Foresteranazenyewe zimeendeshwa sana hasa lile toleo la kati....sasa hivi wameachiliwa madogo wanaonyoa viduku ndiyo wanakaa sana humo.

Kwa hiyo kibongo bongo kumiliki gari inakuwa kama ni fashion flani hivi..

Ila sasa hivi naona kufuga ndevu ndiyo kunatawala
 
NAMBA 6 imenichekesha sana... vipi tunao endesha Nissan Fuga?
 
Kweli mkuu...ila sabau kubwa nadhani ni vile Watz tunapenda mambo ya fashion.
Magari mengi ni fashion ikishapita inakuwa yeboyebo.

1. Nianze na GX 100 chaser, mark ii na cresta.
2.Tukaja GX 110
3.Verosa haikufanya vizuri saana
4.Brevis nayo ilivamiwa sasa hivi watu wanaikimbia kama ukoma
5.Mark x hapo napo watu kibao walikimbilia ila bado inafanya vizuri...

Vipi premio
 
Mkuu nataka nijiripue kununu Brevis used, Hebu nipe Wastani wa matumizi wa mafuta kwa kilometer. ( Nipo huku mikoani hakuna foleni ), kuna jamaa anasema 6Km/l ? real

Brevis ni Gari zuri sana sema watu wanaishi na maneno ya vijiweni kuwa inakula mafuta mimi naendesha Brevis mwaka 4 huu sijaona shida. Mafuta ni 8.5km kwa Litre. Kwa siku ikiwa safari ndefu natumia mpk 14km/L. Pia ina stability kubwa sana barabarani hasa kwenye speed.
 
Duh! Yaani kuna watu wanaisifia Brevis na kuna watu wanaiponda balaa! Mnatupa wakati mgumu sana sisi tunao waza kumiliki magari[emoji34]
 
Jini hilo.watu wanakimbia linabugia sana.bora Safar ya mbali.lkn kwa mjin humu majanga
 
Ushauri maana usinunue gari inayouzwa na mtu mweusi agiza moja kwa moja anapouza jua ina tatizo au kuna tatizo linakuja kutokea

Inategemea mkuu, kuna gari nilinunua kwa mtu, fundi akaikagua na kunishauri niichukue. Tokea 2016 nilipoinunua nilichobadiisha ni wind screen (ilipasuka kwa jiwe wakati napishana na Bus), Battery na Tairi basi.
 
Kweli mkuu...ila sabau kubwa nadhani ni vile Watz tunapenda mambo ya fashion.
Magari mengi ni fashion ikishapita inakuwa yeboyebo.

1. Nianze na GX 100 chaser, mark ii na cresta.
2.Tukaja GX 110
3.Verosa haikufanya vizuri saana
4.Brevis nayo ilivamiwa sasa hivi watu wanaikimbia kama ukoma
5.Mark x hapo napo watu kibao walikimbilia ila bado inafanya vizuri...
nina mpango na forester sh5 vp mkuu niandae kidugu mapema, lkn mbona huku waheshimiwa wanazipenda sana na si vijana wa viduku
Anyway hizi gari zina shida gani mkuu

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Fuga naielewa sana Ila sina uhakika na uimara wake.
 
NAMBA 6 imenichekesha sana... vipi tunao endesha Nissan Fuga?
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]Fuga sina wasiwasi kabisaa...wamiliki wengi wa Nissan wana adabu flani hivi inayokaribiana na wamiliki wa European cars unlike most of Toyota owners..
Naona wengi wanaomiliki Toyota wanaziburuza sana, sijui vile wanapata spea kwa bei rahisi..?[emoji23]
 
Vipi premio
Hii gari nayo imevamiwa sana lakini bado ipo classic sana....kwa upande wangu naona hii gari itaendelea kutunza value yake kuliko hata hizo crown...naipenda bure...huku mtaani kwetu wajeda wliajiriwa majuzi ndiyo wamezikimbilia sana na IST..
 
nina mpango na forester sh5 vp mkuu niandae kidugu mapema, lkn mbona huku waheshimiwa wanazipenda sana na si vijana wa viduku
Anyway hizi gari zina shida gani mkuu

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
hahhahaa...kama una mpango wa kukaa ndani ya SH 5 wala usinyoe kiduku....wewe andaa suti za kutosha ndiyo zinapendeza mule...gari ya heshima sana ile.... binafsi naipa heshima kuliko hata wenzake wkina vanguard au x trail new model..

Kwenye forester SG5 na Altezza, mule ndiyo tunanyoa viduku, K vant kiasi au konyagi kubwa...hahahaa[emoji23][emoji23] bila kusahau suruali mibano za jeans zilizochanwa magotini..[emoji119][emoji119][emoji119]

Kuhusu uimara subaru hazijawahi kuwaangusha watumiaji. Kuna maneno ya vijiweni kuwa boxer engine zina tabia ya kuunguza head gasket.....ninachojua kuunguza head gasket si swala la kitoto..

Mapigo ya boys the way wanavyozishurutisha subaru, jumlisha service duni za bei rahisi, lazima tu waunguze hizo head gasket.

Hiyo SH5 ni gari nzuri japo spea zipo juu....kwa mujibu wa watumiaji wachache, matatizo ni yale yale ya kawaida kulingana na mazingira yetu
 
Back
Top Bottom