BRICS yafanya demo ya mfumo wa malipo kwa kadi (BRICS payment system cards) ikiwa ni maandalizi ya mfumo mpya wa malipo BRICS Pay

BRICS yafanya demo ya mfumo wa malipo kwa kadi (BRICS payment system cards) ikiwa ni maandalizi ya mfumo mpya wa malipo BRICS Pay

State Propaganda

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2024
Posts
542
Reaction score
1,286
Ni miaka miwili imepita sasa tangu umoja wa BRICS kuanza kusaka na kutafuta mfumo mbadala na huru wa wa malipo ya kifedha ambayo itatumika kufanya manunuzi na kulipia bidhaa mbali mbali baina ya nchi wanachama wa BRICS.

Huu ni moja ya mpango kabambe wa kuondoa utegemezi wa mfumo wa kimagharibi wa sasa wa malipo 'SWIFT payment 'na matumizi ya dola Marekani.

Mfumo huu wa BRICS Payment 💳 ulianza kufanyiwa majaribio rasmi katika Mkutano wa Biashara wa BRICS huko Moscow ukiofanyika tarehe 17 Oktoba 2024.

Mkutano mkuu wa BRICS 2024 unatarajiwa kuona uzinduzi kamili wa mfumo wa malipo huo.

Faida za mfumo huu mpya wa BRICS Pay ni kama vile:
1) Uondoaji wa Gharama za Malipo
Mfumo huu unaweza kupunguza au kuondoa gharama za malipo za kimataifa kwa kuepuka wasimamizi wengi, kama vile mabenki, ambazo yanahusika katika mfumo wa sasa wa malipo ya kimataifa. Hii inafanywa kwa kutumia teknolojia ya blockchain ili kuwezesha malipo ya kati ya kati bila wasimamizi kama vile mabenki.

2) Malipo kufanyika kwa haraka
Blockchain itaokoa muda wa malipo ya kimataifa, ambayo mara nyingi huchukua muda mrefu mfano siku moja tu badala ya siku kadhaa.

3) Kupunguza Kutegemea Dola ya Marekani
Mfumo wa BRICS Pay unalenga kupunguza kutegemea dola ya Marekani kama sarafu ya msingi kwa malipo ya kimataifa. Kwa kuruhusu malipo kufanywa kwa sarafu za ndani au sarafu ya kidijitali (digital currency) iliyoundwa haswa kwa kikundi cha BRICS, mfumo huu unapunguza gharama za ubadilishaji wa sarafu na hatari za kiwango cha ubadilishaji, na kuongeza uhuru wa kifedha kwa nchi wanachama wa BRICS.

Kiufupi, hii ni habari mbaya mno kwa Marekani na washirika wake.

IMG_20241019_100222.jpg
Screenshot_2024-10-19-11-08-34-24.png
 
Sasa hayo mataifa ya brics yanayokabiliwa na mchoko yakitaka kufanya biashara na nchi za magharibi yasiyo wanachama wa hiyo brics watafanyaje sasa..!!
Swali zuri,

Nafikiri kwa sasa lengo ni kuvutia kupunguza utegemezi wa $ japo bado safari ni ndefu, ila hii move ni nzuri.

Wakati mwingine huwa nadhani BRICS wanafanya maamuzi nia si kuiangusha $ kwa haraka bali ni ili kuifanya $ isijisahau kama TANESCO.
 
Swali zuri,

Nafikiri kwa sasa lengo ni kuvutia kupunguza utegemezi wa $ japo bado safari ni ndefu, ila hii move ni nzuri.

Wakati mwingine huwa nadhani BRICS wanafanya maamuzi nia si kuiangusha $ kwa haraka bali ni ili kuifanya $ isijisahau kama TANESCO.


 
Back
Top Bottom