BRICS yafanya demo ya mfumo wa malipo kwa kadi (BRICS payment system cards) ikiwa ni maandalizi ya mfumo mpya wa malipo BRICS Pay

BRICS yafanya demo ya mfumo wa malipo kwa kadi (BRICS payment system cards) ikiwa ni maandalizi ya mfumo mpya wa malipo BRICS Pay

Wanaamini kila kitu hakiwezekani
Kinacho nisikitisha, eti hawa watu ndio huaga wanakaa vikao vya kujadiri mustakabari wa Tanzania; ndio maana bandari imewashinda kuendesha, mwendokasi imeshindikana, shirika la simu yaani TTCL, nk. Halafu ni vitu ambavyo wala havina ushindani wa kugombania wateja; wateja wanajileta wenyewe tu. HATARI sana
 
Mpuuzi mmoja anaye tawaliwa na ccm anapo jifanya ana akili kuliko viongozi wote wa brics.
Ndugu yangu,hii nchi ni ngumu sana.
Mtu huyo utamkuta ni mashabiki wa sinema za katika mabanda umiza zilnazotafasiliwa kwa kiswahili.
Iwe ni ya kihindi, kiingereza,kichina lkn mkalaimani anaongea kwa kiswahili.
Na Wana enjoy kweli aisee.
 
Countries lining up to join BRICS – Putin
Some 30 nations have shown interest in cooperating with or joining the group, Russian President Vladimir Putin has noted.

The number of countries engaging with the BRICS group has been growing, with some 30 nations showing interest in cooperating with it in some form, Rus

The president made the remarks on Friday during a meeting with leading reporters from BRICS nations. Collectively, the group already incorporates some 45% of the world population, while its trade turnover and share in the global economy has been growing steadily, Putin noted.

“Our group is expanding. The number of friends and like-minded people within the BRICS association has increased, and interest in the association’s activities is very high,” the Russian president said.

“To date, some 30 countries have expressed their desire to cooperate with BRICS to one degree or another, to join the activities of the organization in one way or another,” Putin added.

The group should not be perceived as a bloc of any kind, Putin stressed, explaining that the nature of BRICS makes it globally beneficial, and not just for its own participants.

“We are not building some bloc directed against someone’s interests. This is not such an organization. And in this sense, it has a universal character and, in my opinion, will have a beneficial effect on world affairs as a whole, including the world economy,” Putin said.

The Russian president also rejected assertions that BRICS is somehow geared against the collective West.

BRICS is not an anti-Western association. It’s simply non-Western.

The prospects of further expansion of BRICS must be carefully assessed by its standing members and a solid consensus on the matter must be reached, Putin said. While potentially growing in numbers, the group must remain multilateral and keep its current efficiency, he explained.

“By increasing the number of the organization’s members, we should not reduce the effectiveness of the whole structure to a minimum,” Putin cautioned.
 
Mfumo ukifanya vizuri watu wata adopt tu. Kwani nani alitarajia android ingekuja kuimeza Symbian Os na blackberry Os?

Leo hii hata ukipewa nokia E62 au blackberry yoyote huwezi kuifurahia kama ilivyo Samsung Galaxy S24 Ultra au Iphone 16 pro max au Google Pixel 9 Pro.
 
Ni miaka miwili imepita sasa tangu umoja wa BRICS kuanza kusaka na kutafuta mfumo mbadala na huru wa wa malipo ya kifedha ambayo itatumika kufanya manunuzi na kulipia bidhaa mbali mbali baina ya nchi wanachama wa BRICS.

Huu ni moja ya mpango kabambe wa kuondoa utegemezi wa mfumo wa kimagharibi wa sasa wa malipo 'SWIFT payment 'na matumizi ya dola Marekani.

Mfumo huu wa BRICS Payment 💳 ulianza kufanyiwa majaribio rasmi katika Mkutano wa Biashara wa BRICS huko Moscow ukiofanyika tarehe 17 Oktoba 2024.

Mkutano mkuu wa BRICS 2024 unatarajiwa kuona uzinduzi kamili wa mfumo wa malipo huo.

Faida za mfumo huu mpya wa BRICS Pay ni kama vile:
1) Uondoaji wa Gharama za Malipo
Mfumo huu unaweza kupunguza au kuondoa gharama za malipo za kimataifa kwa kuepuka wasimamizi wengi, kama vile mabenki, ambazo yanahusika katika mfumo wa sasa wa malipo ya kimataifa. Hii inafanywa kwa kutumia teknolojia ya blockchain ili kuwezesha malipo ya kati ya kati bila wasimamizi kama vile mabenki.

2) Malipo kufanyika kwa haraka
Blockchain itaokoa muda wa malipo ya kimataifa, ambayo mara nyingi huchukua muda mrefu mfano siku moja tu badala ya siku kadhaa.

3) Kupunguza Kutegemea Dola ya Marekani
Mfumo wa BRICS Pay unalenga kupunguza kutegemea dola ya Marekani kama sarafu ya msingi kwa malipo ya kimataifa. Kwa kuruhusu malipo kufanywa kwa sarafu za ndani au sarafu ya kidijitali (digital currency) iliyoundwa haswa kwa kikundi cha BRICS, mfumo huu unapunguza gharama za ubadilishaji wa sarafu na hatari za kiwango cha ubadilishaji, na kuongeza uhuru wa kifedha kwa nchi wanachama wa BRICS.

Kiufupi, hii ni habari mbaya mno kwa Marekani na washirika wake.

Waigizaji hao.
India wenyewe wamegoma kuitosa U$.
Halafu wote hao, ukimuondoa Russia, kila mmoja kwa wakati wake US trading partner ambako huko wanaendelea kufanya malipo kwa U$.
Ikumbikwe, Imekuja Euro na bado US$ ipo palepale.
Kama ni mchezo basi hawa jamaa wanacheza kibaba-baba😅
 
Hamna jipya hapo brics na wao wanatafuta namna na kupata pesa ili kukuza uchumi wao, hapo Kuna makoto na vitu vingine.
 
Sasa hayo mataifa ya brics yanayokabiliwa na mchoko yakitaka kufanya biashara na nchi za magharibi yasiyo wanachama wa hiyo brics watafanyaje sasa..!!
Hiyo ni hatua kuelekea kwenye one world payment system kwa hiyo hata hiyo BRICS payment system nayo itacollapse ila kupisha mfumo mmoja wa malipo dunia nzima
 
Sasa hayo mataifa ya brics yanayokabiliwa na mchoko yakitaka kufanya biashara na nchi za magharibi yasiyo wanachama wa hiyo brics watafanyaje sasa..!!
Watafanya kwa dola.. Watu wanafikiri brics ikianza kutuMika ndio dola itakufa hapana si kweli..

Kifupi kinachokwenda kufanyika ni kutengeneza multi- currency system kwenye biashara za kimataifa.. sababu sasa hv dola inatumika kama reserve currency, kwa lugha nyepesi ni kuwa inatumika kama reference ya kufanya miamala katika ya nchi na nchi..

Na sio kwamba toka kuumbwa kwa dunia US dollar ndio ilikuwa hivyi.. kabla ya hapo alikuwa pound ya uingereza na kabla ya uingereza ilikuwa France nahs.. vita ya pili ya dunia ndio iliipa nguvu Dollar maana Ulaya walikuwa hoi kiuchumi

Na kikao cha nchi nyingi kikaamua kuitumia dola kama reserve currency.. sababu wao kwa wao hawakuaminina kwenye stabilit ya currency zao wakaamua kutafuta neutral ground na wakat huo US hakuathirika na ile vita kivile.. infact ndipo alipoanza kuwa super power maana silaha za vita ya 2 ya dunia kwa "allies" nyingi alikuwa anawauzia. So mwisho wa vita nchi nyingi za ulaya zikawa zinadaiwa na US

Kwa kifupi dunia imechelewa kubadili huu mfumo wa kutumia currency moja kama reserce curency so wanachokifanya BRIC ni sawa ingawa sio kuwa dollar itakufa yaan mpaka dollar irudi tu kuwa ni pesa ya US na sio ya Dunia nzima itachukua kama 10+ years ama hata 20.. sababu kuna biashara kama za loan na bonds ambazo ziko kwenye mfumo wa dollar zingine maturity ni 10 tu 20 yeaars so bado dollar itaendelea kuwepo

Na mwisho kwangu mie mfumo mzima wa dunia kwenye uthaman wa pesa ni wa ovyo. Toka marekan alipopiga stop kuithaminisha dollar againts Gold.. ndio aliwafundisha mataifa dunian kuprint tu pesa.. mfumo wa sasa thaman ya pesa imebase kwenye trust na wala haina backup yoyote

Bank kikuu wa kiprint tu karatasi wakisema kuwa ss hv hii inathaman ya shilingi 20k ndio inabidi iaminike

Ndo maana nchi zinadefault sababu maden yakizid wanakimbilia ku print pesa.. unatakiwa urudi mfumo wa kuithaminisha thaman ya pesa urudi kama zaman utumie vitu ambavyo havishuki thaman. Mfano Gold, silver, diamond. Sio tu kikundi cha kiamue
 
Sasa hayo mataifa ya brics yanayokabiliwa na mchoko yakitaka kufanya biashara na nchi za magharibi yasiyo wanachama wa hiyo brics watafanyaje sasa..!!
Meza kwanza mate halafu uje uandike upya
 
Nadhani hiyo blockchain yao itakuwa ni kwa ajili ya kufanyia biashara among them only, ila beyond the Brics borders watalazimika kutumia Swift na $.
Sahihi unachokisema, na ndio maana wao wenyewe Sasa hivi wanachokifanya ni kukaribisha wanachama wapya hili kuongeza wigo wa kibiashara na hatimae kufanikisha mpango wao wa dedollarization. Mpaka Sasa hivi Kuna mataifa Zaid ya 50 yaliyoomba unaachana wa BRICS
 
Ili tusibabaishane sijui VIZA na Ujinga gani kwendaaa hawa jamaa vikwazo vyao watajutia sana kuna mtu aliwahi kusema matatizo ni mazuri mana yanakupa akili ya kujinasua na ndio unatokea humo humo
 
Sahihi unachokisema, na ndio maana wao wenyewe Sasa hivi wanachokifanya ni kukaribisha wanachama wapya hili kuongeza wigo wa kibiashara na hatimae kufanikisha mpango wao wa dedollarization. Mpaka Sasa hivi Kuna mataifa Zaid ya 50 yaliyoomba unaachana wa BRICS
Watanzania wanaanmin kila kitu hakiwezekan.. yaan hata sisi kama nchi hatuwezi kuendesha bandari TTCL mwendo kasi ila mpaka waje wazungu huko ndo wataweza kuendesha
 
Back
Top Bottom