Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Kwa hisani ya JF.

Jenerally Silas Mayunga - Mti Mkavu

 
Nadhani Ambrose Bayeke ana mchango mkubwa ktk phase ya kwanza ya kuyatoa majeshi ya uvamizi ktk ardhi yetu.

Nasema hivyo kwasababu nimeona kuna mpaka picha za Bayeke akim-brief Mwalimu Nyerere alipowatembelea askari waliokuwa mstari wa mbele.

Kumbukumbu ya mwisho ya Brigadier.Ambrose Bayeke ni alipokuwa parade commander wa magwaride yote makubwa.
Jana pia kashiriki katika kuwaenzi mashujaa wetu .
 
Please please, wapo watu wa kukusaidia dondoo za kuchokoza mada kabla ya kuwaona wahusika.

Fanyia kazi mkuu, hili ni jema kwako na kwa Taifa na najua unaliweza bila chembe ya shaka.
Its true, linawezekana haswa kwa kuzingatia mimi mwenyewe baada ya JKT, nilikwenda straight JWTZ,
Kati ya kazi ngumu sana za utengenezaji documentary, ni documentary za vita. Kuna waandishi waliokuwa front line wawili nawakumbuka walikuwa AVI, Dickson Saileni na Dick Kaombwe, ila pia changamoto ni nyingi, inahitaji
1. Passion
2. Dedication
3. Commitment
4. Equipments
5. Contents Resourceful personnel
6. Financial Resources
7. Logistics
Kwa fani yetu high season hutokea mara moja kila baada ya miaka 5, by now mawazo yote ni October, ila everything is possible.
P
Ni miaka mitatu sasa
Asanteni kunikumbusha
Bado sijafanikiwa kupata muda, na sijui kama wale ma source wangu wawili wakuu kama bado wapo!.
P
 
..ktk waandishi ambao wana viwango na wanaoweza kuitendea haki historia hii ni wewe.

..ila TIME is not on your side. Most senior commanders wa vita vya Kagera wametangulia mbele za haki.

..ambao bado wapo ni Gen.David Musuguri, Gen.Tumainieli Kiwelu, Gen.Robert Mboma, na Lt.Gen.Martin Mwakalindile.

..yupo pia Brig.Gen.Lupembe ambaye ana habari nyingi sana za Uganda kwasababu alikuwa msaidizi wa Gen.Musuguri wakati wa vita. Lupembe aliwahi kuhojiwa na magazeti ya Uganda and he was very resourceful.
Asante, zile hoja za Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin bado zinahusu!.
P
 
kwa msaada wa mitandao
Ukwaju na JokaKuu Nawashukuru kwa kunikumbusha mbali sana!!Nimesoma na nimekumbuka kuna sehemu nyingi niliandika mimi kwenye JF Niliandika VITA VYA KAGERA- HISTORIA YANGU SEHEMU YA KWANZA,PILI NA YA TATU.Labda nipende kukurekebisha kwenye andiko lako Ukwaju umeandika hivi( Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General,ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General) Hapo ondoa neno KIKABADIRISHWA Sijui sentensi nzima hiyo uliitoa wapi maana kwenye andiko langu hakuna sentesi kama hiyo hata nakushukuru sana umenirudisha Frontline kama tulivyokuwa tunasema kipindi hicho!!!!
[/QUOTE]
Naendelea kuifuatilia hii kitu!.
P
 
Naunga mkono hoja ya kutengeneza documentary ya vita ya Kagera pía ya ukombozi wa Msumbiji ambako Col. Mahfudhi alitoa mchango mkubwa sana. Muda sio rafiki kwani sina hakika kama wengi wa makamanda wa vita hivi kama wangari hai; Juzi juzi tu tumetoka kumzika Major General Maneno pale Tegeta na sina hakika kama Luteni General Tumainieli Kiwelu bado yuko kule Kagera alikoamua kuishi baada ya kustaafu! Tutumie wachache waliobaki kama Major General Msuya na General Robert Mboma kuweka kumbukumbu sahihi ya vita ambazo nchi ilipigana.
Noted
P
 
Its true, linawezekana haswa kwa kuzingatia mimi mwenyewe baada ya JKT, nilikwenda straight JWTZ,
Kati ya kazi ngumu sana za utengenezaji documentary, ni documentary za vita. Kuna waandishi waliokuwa front line wawili nawakumbuka walikuwa AVI, Dickson Saileni na Dick Kaombwe, ila pia changamoto ni nyingi, inahitaji
1. Passion
2. Dedication
3. Commitment
4. Equipments
5. Contents Resourceful personnel
6. Financial Resources
7. Logistics
Kwa fani yetu high season hutokea mara moja kila baada ya miaka 5, by now mawazo yote ni October, ila everything is possible.
P
Samahani mkuu hili ulifanikiwa kulitekeleza?
 
Huyu ni mmoja kati ya makamanda walioongoza vita vya Kagera lakini siyo maarufu ktk vyombo vyetu vya habari, lakini ukisoma VITABU mbalimbali vinavyohusu VITA VYA KAGERA utagundua kwamba alikuwa na mchango mkubwa toka mwanzo mpaka mwisho wa vita, yaani toka Mutukula/Kagera mpaka Koboko kijiji alikozaliwa Iddi Amin Dada.

Baada ya majeshi ya Uganda kuvamia ardhi ya Tanzania na kuikalia, Tumainieli Kiwelu [ meja jenerali wakati huo] ambaye alikuwa Chief of Staff JWTZ alipewa jukumu la kuandaa majeshi yetu na kuongoza mapigano ya kukomboa ardhi yetu.

Ahmed Takadiri Kitete[ kanali wakati huo] ametambulishwa ktk kitabu cha " Vita vya Kagera -- 'kagera hadi arua' " kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita ktk operesheni ya kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

Ahmed Kitete alipandishwa cheo na kuteuliwa kuongoza Brigade ya Minziro ambayo ilipigana maeneo ya Bushenyi, Kasese, Fort Portal, Hoima, Masindi, Karuma Falls, Pakwach, Bondo, Arua, Yumbe, na Moyo mpakani na Sudan [ sasa hivi South Sudan].

Brigade ya Minziro ndiyo iliyohitimisha vita vya Uganda na Brigadier.Kitete ndiye kamanda wa Tanzania aliyefika mpaka kijiji cha Koboko alipozaliwa alipozaliwa Iddi Amin Dada.

Makamanda wote wakuu waliopiganisha vita vya Kagera walikuwa na majina yao ya kimapigano au nom de guerre, kwa mfano Major General Kimario alijulikana kama " kamanda mbogo." Major General Imran Kombe alijulikana kama "kamanda ngono" kwasababu aliongoza mapigano kuvuka mto ngono. Colonel Tumbi ambaye alikuwa mkuu wa vikosi vya mizinga aliitwa "kamanda radi."Ahmed Takadiri Kitete alipewa jina la " kamanda supersonic. "

Baada ya vita vya Kagera Ahmed Kitete alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz. Kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari jijini D'salaam.

Nakaribisha michango ya wengine wenye taarifa za Ahmed Takadiri Kitete shujaa na kamanda mahiri wa jeshi la wananchi wa tanzania.
View attachment 1810876

Kushoto Brigedia Tumainieli Kiwelu kamanda mkuu wa operesheni chakaza ya kuondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.Kulia Kanali Ahmed Kitete mkuu wa mipango ya kivita ktk operesheni chakaza.

cc Echolima, Manyerere Jackton , gobore, Mohamed Said, Nguruvi3, gobore, The only, Ukwaju
Tanzania tumebarikiwa kuwa na hazina kubwa ya wazalendo walioipigania sana nchi hii, tutafute namna ya kuhifadhi historia hii iliyotukuka na kujenga wazalendo wengine bora zaidi
 
JokaKuu mara nyingi sana tumeongelea manguli wa JWTZ na mmojawapo ni Brig. Gen Abrose Bayeke
Huyu kama unakumbuka niliwahi kueleza jinsi alivyokuwa na ukaribu na askari wa chini. Nilishuhudia hilo

Juzi kapewa heshima kubwa sana pale uwanja wa mashujaa. Kwakweli nilifaraijika sana maana miongoni mwa Askari wa ' kazi' alikuwepo. Walitoa wasifu wake wakisema alikuwa chini ya Maj. Gen Walden. Sasa fikiria mtu huyo amefanya kazi na akina Walden, Mayunga, Maneno, Lt Gen T.Kiwelu na miongoni mwa waliobaki ni Gen Misuguri.
Ametunukiwa nishani 9 kama ulivyoona katika sherehe

Bayeke ni mtu muhimu sana katika historia ya vita vya Kagera na utumishi wa jeshi
Nilisikitika sana Lt Gen Tumainiel Kiwelu alifariki lakini mazishi yake hayakupewa uzito unaostahili

Pascal Mayalla katika kazi yako fanya utaratibu wa kuonana na Bayeke , ana mengi sana ya kueleza. Kuna taarifa za kutatanisha kwamba aliyeongoza infantry kuingia Kampala alikuwa Brig. Gen Bayeke, alkini pia kuna taarifa za Maj Gen Msuya wakati huo akiwa Kanali kama sikosei ndiye aliyeongoza askari kuingia Kampala. Kulikuwa na Brigade ya mashariki na Magharibi na zilipofika Kampala kukaw na ''friendly fire'

Unaona hiyo picha Kitete akiwa na Kiwelu, hapo kuna jambo linapangwa.

Tanzania iliogopeka nyakati hizo!
 
Back
Top Bottom