Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Huyu ni mmoja kati ya makamanda walioongoza vita vya Kagera lakini siyo maarufu ktk vyombo vyetu vya habari, lakini ukisoma VITABU mbalimbali vinavyohusu VITA VYA KAGERA utagundua kwamba alikuwa na mchango mkubwa toka mwanzo mpaka mwisho wa vita, yaani toka Mutukula/Kagera mpaka Koboko kijiji alikozaliwa Iddi Amin Dada.

Baada ya majeshi ya Uganda kuvamia ardhi ya Tanzania na kuikalia, Tumainieli Kiwelu [meja jenerali wakati huo] ambaye alikuwa Chief of Staff JWTZ alipewa jukumu la kuandaa majeshi yetu na kuongoza mapigano ya kukomboa ardhi yetu.

Ahmed Takadiri Kitete [kanali wakati huo] ametambulishwa ktk kitabu cha " Vita vya Kagera -- 'kagera hadi arua' "kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita ktk operesheni ya kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

Ahmed Kitete alipandishwa cheo na kuteuliwa kuongoza Brigade ya Minziro ambayo ilipigana maeneo ya Bushenyi, Kasese, Fort Portal, Hoima, Masindi, Karuma Falls, Pakwach, Bondo, Arua, Yumbe, na Moyo mpakani na Sudan [sasa hivi South Sudan].

Brigade ya Minziro ndiyo iliyohitimisha vita vya Uganda na Brigadier.Kitete ndiye kamanda wa Tanzania aliyefika mpaka kijiji cha Koboko alipozaliwa alipozaliwa Iddi Amin Dada.

Makamanda wote wakuu waliopiganisha vita vya Kagera walikuwa na majina yao ya kimapigano au nom de guerre, kwa mfano Major General Kimario alijulikana kama "kamanda mbogo."Major General Imran Kombe alijulikana kama "kamanda ngono" kwasababu aliongoza mapigano kuvuka mto ngono. Colonel Tumbi ambaye alikuwa mkuu wa vikosi vya mizinga aliitwa "kamanda radi." Ahmed Takadiri Kitete alipewa jina la " kamanda supersonic. "

Baada ya vita vya Kagera Ahmed Kitete alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz. Kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari jijini D'salaam.

Nakaribisha michango ya wengine wenye taarifa za Ahmed Takadiri Kitete shujaa na kamanda mahiri wa jeshi la wananchi Watanzania.

Kushoto Brigedia Tumainieli Kiwelu kamanda mkuu wa operesheni chakaza ya kuondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania. Kulia Kanali Ahmed Kitete mkuu wa mipango ya kivita ktk operesheni chakaza.

cc Echolima, Manyerere Jackton , gobore, Mohamed Said, Nguruvi3, gobore, The only, Ukwaju

Halafu ikawaje kwa Brigadia Kitete? Tuanze kuandika sasa. Nimefurahi kuona kuna maandishi ya Edward Moringe Sokoine. Kama hawa wote watakuwa na maandishi, basi watoto wetu watapata wasaa wa kujua nani ni nani na kujiuliza nani alikuwa poyoyo
 
Mkuu ulichoeleza ni sahihi kabisa na umeleta kumbu kumbu nzuri sana.

Baada ya vita huyu kamanda Kitete alikuwa maarufu nadhani kifo chake kilichotokea mapema kimechangia sana jina lake kutosikika. Nakumbuka ilikuwa kawaida kusikia ''supersonic'' au kumsikia Kitete.

Kuna tatizo kubwa sana katika kuweka kumbu kumbu za vita ya Kagera. Wapo watu walioshiriki na michango yao haielezwi. Tungewatumia akina Major General Msuya ambaye yupo kuweka kumbu kumbu sawa sawa.

Msuya naye ni kama Kitete, ushiriki wake hasa kuteka Kampala hauelezwi vema. Ni wachache sana wanaojua

Kuna askari kama akina Brigedia Ambrose Bayeke, huyu alikuwa na cheo kidogo wakati wa vita, lakini alipanda sana hata kuongoza vikosi vyetu kule Kongo. Ni watu wenye hazina ya historia ya JWTZ. Sijui yupo wapi

Mwingine ni Major general Maneno, naye kama Bayeke alikuwa ni afisa wa ngazi za kati.

Pengine washauriwe kuandika 'memoir ' na JWTZ iwasaidia katika kufanikisha hilo.

Nilimshauri Pascal Mayalla kupitia ''Media yake ya PP'' aandae documentary ya vita.

..kuna taarifa / video imetoka hivi karibuni inawatambulisha wakuu wa vikosi waliokuwa chini ya wale makamanda wakuu ambao ni maarufu.

..Ambrose Bayeke, Simba Waziri Simba, Ben Msuya, Lupembe, Gideon Sayore, Maneno, Kisanko, wametambuliwa kwa mchango wao kama wakuu wa vikosi ktk vita vya Kagera.

..kipekee, Ambrose Bayeke ndiye alikuwa 2-I-C wa gwaride la ushindi wa vita vya Kagera pale Bunazi. Parade commander alikuwa Gideon Sayore.

..utakumbuka Sayore alitumikia kama Mkuu wa chuo cha maofisa Monduli, na baadae Mnadhimu Mkuu wa Jwtz.
 
Huyu ni mmoja kati ya makamanda walioongoza vita vya Kagera lakini siyo maarufu ktk vyombo vyetu vya habari, lakini ukisoma VITABU mbalimbali vinavyohusu VITA VYA KAGERA utagundua kwamba alikuwa na mchango mkubwa toka mwanzo mpaka mwisho wa vita, yaani toka Mutukula/Kagera mpaka Koboko kijiji alikozaliwa Iddi Amin Dada.

Baada ya majeshi ya Uganda kuvamia ardhi ya Tanzania na kuikalia, Tumainieli Kiwelu [meja jenerali wakati huo] ambaye alikuwa Chief of Staff JWTZ alipewa jukumu la kuandaa majeshi yetu na kuongoza mapigano ya kukomboa ardhi yetu.

Ahmed Takadiri Kitete [kanali wakati huo] ametambulishwa ktk kitabu cha " Vita vya Kagera -- 'kagera hadi arua' "kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita ktk operesheni ya kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

Ahmed Kitete alipandishwa cheo na kuteuliwa kuongoza Brigade ya Minziro ambayo ilipigana maeneo ya Bushenyi, Kasese, Fort Portal, Hoima, Masindi, Karuma Falls, Pakwach, Bondo, Arua, Yumbe, na Moyo mpakani na Sudan [sasa hivi South Sudan].

Brigade ya Minziro ndiyo iliyohitimisha vita vya Uganda na Brigadier.Kitete ndiye kamanda wa Tanzania aliyefika mpaka kijiji cha Koboko alipozaliwa alipozaliwa Iddi Amin Dada.

Makamanda wote wakuu waliopiganisha vita vya Kagera walikuwa na majina yao ya kimapigano au nom de guerre, kwa mfano Major General Kimario alijulikana kama "kamanda mbogo."Major General Imran Kombe alijulikana kama "kamanda ngono" kwasababu aliongoza mapigano kuvuka mto ngono. Colonel Tumbi ambaye alikuwa mkuu wa vikosi vya mizinga aliitwa "kamanda radi." Ahmed Takadiri Kitete alipewa jina la " kamanda supersonic. "

Baada ya vita vya Kagera Ahmed Kitete alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz. Kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari jijini D'salaam.

Nakaribisha michango ya wengine wenye taarifa za Ahmed Takadiri Kitete shujaa na kamanda mahiri wa jeshi la wananchi Watanzania.

Kushoto Brigedia Tumainieli Kiwelu kamanda mkuu wa operesheni chakaza ya kuondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania. Kulia Kanali Ahmed Kitete mkuu wa mipango ya kivita ktk operesheni chakaza.

cc Echolima, Manyerere Jackton , gobore, Mohamed Said, Nguruvi3, gobore, The only, Ukwaju
RIEP General Kitete
 
Nadhani Ambrose Bayeke ana mchango mkubwa ktk phase ya kwanza ya kuyatoa majeshi ya uvamizi ktk ardhi yetu.

Nasema hivyo kwasababu nimeona kuna mpaka picha za Bayeke akim-brief Mwalimu Nyerere alipowatembelea askari waliokuwa mstari wa mbele.

Kumbukumbu ya mwisho ya Brigadier.Ambrose Bayeke ni alipokuwa parade commander wa magwaride yote makubwa.

Ameenda wapi?
 
Twendeni basi tukamtandike Kagame....Maana akichukua Goma maana yake mizigo ya bandari yetu kwenda Congo yeye ndio Bossi.......
Sio tunazama kwenye lindi za zilipendwa.....
 
Lini tuanze safari? 😂 😂 😂 😂 😂
Bado tunamalizana na maonyesho ya mitano tena , halafu ndio tutaianza safari....

1740347236736.png
 
Back
Top Bottom