Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Brigadier Ahmed Takadiri Kitete: Shujaa aliyepiganisha vita toka Kagera mpaka Koboko alikozaliwa Idi Amin

Mkuu Ndahani, asante kwa huu wimbo. Hii ni kazi ya Zahir Ally Zorro akiwa na bendi ya JKT Kimbunga Stereo.
Kiukweli ni moja ya nyimbo zenye very good lyrics na umetulia. Hizi ni enzi za uzalendo. Zahir yupo, naweza kumpata, wakati wa Vita vya Kagera, Zahir alikuwa Coplo wa Jeshi.
P
Hawa ndio wanajua maana ya uzalendo sio kina Mrisho Mpoto kujichekesha kwa rais halafu wanajiita wazalendo
 
Seychelles ilikuwa na Luteni Jenerali Shimbo kama sikosei.

Vita ya Msumbiji tulikosa sana faida kutoka kwa Luteni Jenerali Tumainieli Kiwelu. Huyu alikuwa na mengi sana ya kueleza, na ndiye aliyemkabili Mwalimu akimweleza kwanin tunaua vijana wetu kwa vita ya ''wajomba''

Hiyo ilikuwa breakthrough ya kumaliza vita ya FRELIMO na RENAMO ambayo kwa kiasi fulani ilikuwa biashara ya viongozi na si vita ya wananchi.
Mkuu natambua hii ni comment ni ya April lakini unaweza kutupa details kuhusu hii 'vita ya wajomba'
 
Mkuu natambua hii ni comment ni ya April lakini unaweza kutupa details kuhusu hii 'vita ya wajomba'
Baada ya Mreno kuondoka ilitokea vita ya RENAMO na FRELIMO. Hivi ni vyama vya ukombozi vya nchi moja.
Mfano wake ni MPLA na UNITA ya Savimbi kule Angola.

Maana yake ni moja, ni ndugu wanapigana, si Mreno si Kaburu.
 
Huyu shujaa wetu KITETE ana mtoto wa kiume anaitwa TAKADIRI ambaye naye kwasasa ni mwanajeshi?
 
Basi kwa jibu simple hilo ni kuwa kamanda aliyepanga vita yote mezani alikuwa kanali Kitete siyo Kiwelu; ukisoma mahojiano hayo anaeleza alivyokuwa akizunguka naye kuvinjari lile eneo la mto ambapo kanali kKitete ndiye aliyeweka mkakakati wa kuwazunguka askari wa Amini kutokea Magharibi. Wakati huo kanali Kitete ndiye aliyekuwa Chief Tactician wa Ngome kabla hajapandishwa cheo kuwa Brigedia na yeye pia kupewa brigedi ya kuongoza ndani ya uganda.

Nadhani unawajibu vizuri. Lakini nadhani kinachosumbua watu ni kutojua kuwa ndani ya jeshi kuna division of labor. CoS anafanya mambo ya administration....anaangalia mambo ya kuajiri watu, mambo ya procurement na mengine. Hivyo hawezi kuwa anayeongoza tactics kwenye uwanja wa mapambano.
 
SUNDAY MONITOR, TANZANIA - UGANDA (KAGERA) WAR:

Maj Gen Abdallah Twalipo was TPDF’s Chief of Defence Forces but the responsibility to respond to Amin’s invasion fell on Brig Gen Tumainieli Kiwelu who had to reorganise the army from different parts of the country.

By then, TPDF had only one army division with four infantry brigades in different parts of the country.

Brigade 101st, nicknamed Nyuki (Bee) was based in Zanzibar, 302nd in Dar es Salaam, 202nd Faru in Tabora and 401 Tembo in Songea.

The youth who had participated in national service training were transformed into a reserve force; trained militias were prepared for battle, police and prisons personnel were mobilised, while the ordinary civilians offered food and livestock, private companies surrendered their vehicles to transport troops and hardware.

At the same time the Uganda exiles living in Tanzania also united to form the Uganda National Liberation Army, which included groups such as Fronasa of Yoweri Museveni, Save Uganda Movement of Akena p’Ojok, Ateker Ejalu and William Omaria and Kikosi Maalum (Special Unit) led by Lt Col David Oyite Ojok and Col Tito Okello. They established a joint training camp of close to 1,200 recruits at Tarime near Musoma on the shores of Lake Victoria.

From Brig Gen Kiwule’s reorganisation, a 20th division was created with different brigades like Brigade 206th under Brig Gen Silas Mayunga – later taken over by Brig Gen Roland Makunda, 207th under Brig Gen Butler Walden and 208th under Brig Gen Mwita Marwa.

As the war progressed more brigades were formed, including 201st under Brig Gen Imran Kombe, 205th under Brig Gen Herman Lupogo – later taken over by Brig Gen Muhidin Kimario, Brigade Minziro under Brig Gen Takadiri Kitete and Brigade Kagera under Brig Gen Ramadhan Haji.

The overall commander of the operation was Brig Gen David Msuguri who was promoted to the rank of Maj Gen as Brig Gen Kiwelu went back to the headquarters as Chief of Staff. Within weeks, the TPDF had mobilised its numbers from 40,000 to 100,000.
 
Nadhani unawajibu vizuri. Lakini nadhani kinachosumbua watu ni kutojua kuwa ndani ya jeshi kuna division of labor. CoS anafanya mambo ya administration....anaangalia mambo ya kuajiri watu, mambo ya procurement na mengine. Hivyo hawezi kuwa anayeongoza tactics kwenye uwanja wa mapambano.

..mchangiaji uliyemjibu alikuwa na nia ya kupotosha.

..na katika uzi huu ametoa madai bila kuwa na vyanzo vinavyaominika kutetea madai yake.

..wakati mwingine amepingana hata na waandishi wa Jwtz walioandika kitabu kinachohusu vita vya Kagera.
 
Its true, linawezekana haswa kwa kuzingatia mimi mwenyewe baada ya JKT, nilikwenda straight JWTZ,
Kati ya kazi ngumu sana za utengenezaji documentary, ni documentary za vita. Kuna waandishi waliokuwa front line wawili nawakumbuka walikuwa AVI, Dickson Saileni na Dick Kaombwe, ila pia changamoto ni nyingi, inahitaji
1. Passion
2. Dedication
3. Commitment
4. Equipments
5. Contents Resourceful personnel
6. Financial Resources
7. Logistics
Kwa fani yetu high season hutokea mara moja kila baada ya miaka 5, by now mawazo yote ni October, ila everything is possible.
P

Tunaomba mrejesho mkuu.
kwa talanta uliyo barikiwa taifa linakutegemea.
jitahidi utuandalie documentary
 
Mkuu ulichoeleza ni sahihi kabisa na umeleta kumbu kumbu nzuri sana.
Baada ya vita huyu kamanda Kitete alikuwa maarufu nadhani kifo chake kilichotokea mapema kimechangia sana jina lake kutosikika. Nakumbuka ilikuwa kawaida kusikia ''supersonic'' au kumsikia Kitete.

Kuna tatizo kubwa sana katika kuweka kumbu kumbu za vita ya Kagera. Wapo watu walioshiriki na michango yao haielezwi. Tungewatumia akina Major General Msuya ambaye yupo kuweka kumbu kumbu sawa sawa.

Msuya naye ni kama Kitete, ushiriki wake hasa kuteka Kampala hauelezwi vema. Ni wachache sana wanaojua

Kuna askari kama akina Brigedia Ambrose Bayeke, huyu alikuwa na cheo kidogo wakati wa vita, lakini alipanda sana hata kuongoza vikosi vyetu kule Kongo. Ni watu wenye hazina ya historia ya JWTZ. Sijui yupo wapi

Mwingine ni Major general Maneno, naye kama Bayeke alikuwa ni afisa wa ngazi za kati.

Pengine washauriwe kuandika 'memoir ' na JWTZ iwasaidia katika kufanikisha hilo.

Nilimshauri Pascal Mayalla kupitia ''Media yake ya PP'' aandae documentary ya vita.
Afande maneno Alisha fariki siku nyingi amekaaa tegeta nimekaa kambini na mwanae wa kike aliolewa na major

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ulichoeleza ni sahihi kabisa na umeleta kumbu kumbu nzuri sana.
Baada ya vita huyu kamanda Kitete alikuwa maarufu nadhani kifo chake kilichotokea mapema kimechangia sana jina lake kutosikika. Nakumbuka ilikuwa kawaida kusikia ''supersonic'' au kumsikia Kitete.

Kuna tatizo kubwa sana katika kuweka kumbu kumbu za vita ya Kagera. Wapo watu walioshiriki na michango yao haielezwi. Tungewatumia akina Major General Msuya ambaye yupo kuweka kumbu kumbu sawa sawa.

Msuya naye ni kama Kitete, ushiriki wake hasa kuteka Kampala hauelezwi vema. Ni wachache sana wanaojua

Kuna askari kama akina Brigedia Ambrose Bayeke, huyu alikuwa na cheo kidogo wakati wa vita, lakini alipanda sana hata kuongoza vikosi vyetu kule Kongo. Ni watu wenye hazina ya historia ya JWTZ. Sijui yupo wapi

Mwingine ni Major general Maneno, naye kama Bayeke alikuwa ni afisa wa ngazi za kati.

Pengine washauriwe kuandika 'memoir ' na JWTZ iwasaidia katika kufanikisha hilo.

Nilimshauri Pascal Mayalla kupitia ''Media yake ya PP'' aandae documentary ya vita.
Ninachojilaumu ni kuwa sikujiwekea kumbukumbu vizuri wakati ule kwa maana ya kuja kuziandika baadaye. Nilikuwa nimemaliza form 6 na nilikuwa na elimu ya kutosha kuweka kumbukumbu hizo. Nilifanya kwanye COMM unit ya brigade kwa zaidi ya miezi sita nikiwa napokea taarifa nyingi sana za vitani na kuzipeleka kiwa makamanda wahusika ndani ya brigade. Hata hivyo wakati huo nilikuwa nimepikwa kuwa msiri sana na niliamini kuwa habari hizo ni classified na hazikutakiwa kutoka nje ya maeneo ya kijeshi; kwa hiyo sikuondoka na notisi zozote za binafsi. Baada ya kushindwa kujiunga na air-force ambayo ndilo lililokuwa chaguo langu wakati huo, nikarudishwa uraiani, na kutupwa kule Anti-corruption Squad kama reporter tu, siyo afisa, lakini vile vile ikiwa ni kwa kuamini kuwa nilikuwa trained kuwa msiri. Hata hivyo baadaye nilipenda kuendelea na elimu ya juu na hivyo kuondoka kwenye system hiyo yenye habari classified. Leo hii najiuliza iawpo ningejiwekea notisi zakutosha ningeweza kuandika kitabu kizuri sana. Lakini ndiyo hivyo, wakati ule nilikuwa mtu msiri wa mambo ya kitaifa kweli kweli, yaani huwezi kuamini!!
 
Si wewe tu, kwakweli ni watu wengi tu walipatwa na hali hiyo. Nadhani siasa za wakati ule ambapo Watanzania walikuwa 'wamefungwa' zilichangia sana kutudumaza katika kuona mambo kwa mtazamo tofauti

Unakumbuka kuwa na 'passport' ya kusafiria ilikuwa 'issue' sasa nyaraka za jeshi kwakweli zilitisha sana

Katika mambo ninayotofautiana sana na Mwalim Nyerere moja ni hili la kuwafunga macho Watanzania kwa miaka kadhaa . Kipindi cha 1970-1985 ilikuwa ngumu sana kupata taarifa za dunia hata kusafiri ilionekana kama 'privilege' na siyo haki ya mtu.

Lakini pia JWTZ ifike mahali wabadilike. Habari za miaka 40 iliyopita zinaweza kuwa declassified na watu wenye kumbukumbu wakaunganisha dots na kuandika. Sioni kwanini vita ya Uganda ibaki kuwa classified
 
Supersonic Kitete ni moja wa makamanda walioandaa mpango madhubuti wa kivita wa kumuondoa kwanza Nduli na majeshi yake nje ya mipaka ya nchi yetu , na kazi hii iliwachukua masaa 24 tu . nilipata kumuuliza juu ya hili na alinijibu kwamba ilikuwa lazima adui atolewe kwanza nje ya mipaka yetu ndo vita iendelee. kwa maelezo yake mpango huu ulitengenezwa na yeye pamoja na Tumaineli kiwelu
CONTINUE TO REST IN PEACE SUPERSONIC KITETE
 
Huyu ni mmoja kati ya makamanda walioongoza vita vya Kagera lakini siyo maarufu ktk vyombo vyetu vya habari, lakini ukisoma VITABU mbalimbali vinavyohusu VITA VYA KAGERA utagundua kwamba alikuwa na mchango mkubwa toka mwanzo mpaka mwisho wa vita, yaani toka Mutukula/Kagera mpaka Koboko kijiji alikozaliwa Iddi Amin Dada.

Baada ya majeshi ya Uganda kuvamia ardhi ya Tanzania na kuikalia, Tumainieli Kiwelu [ meja jenerali wakati huo] ambaye alikuwa Chief of Staff JWTZ alipewa jukumu la kuandaa majeshi yetu na kuongoza mapigano ya kukomboa ardhi yetu.

Ahmed Takadiri Kitete[ kanali wakati huo] ametambulishwa ktk kitabu cha " Vita vya Kagera -- 'kagera hadi arua' " kama mkuu wa mipango ya uamrishaji kivita ktk operesheni ya kuyaondoa majeshi ya Uganda ktk ardhi ya Tanzania.

Ahmed Kitete alipandishwa cheo na kuteuliwa kuongoza Brigade ya Minziro ambayo ilipigana maeneo ya Bushenyi, Kasese, Fort Portal, Hoima, Masindi, Karuma Falls, Pakwach, Bondo, Arua, Yumbe, na Moyo mpakani na Sudan [ sasa hivi South Sudan].

Brigade ya Minziro ndiyo iliyohitimisha vita vya Uganda na Brigadier.Kitete ndiye kamanda wa Tanzania aliyefika mpaka kijiji cha Koboko alipozaliwa alipozaliwa Iddi Amin Dada.

Makamanda wote wakuu waliopiganisha vita vya Kagera walikuwa na majina yao ya kimapigano au nom de guerre, kwa mfano Major General Kimario alijulikana kama " kamanda mbogo." Major General Imran Kombe alijulikana kama "kamanda ngono" kwasababu aliongoza mapigano kuvuka mto ngono. Colonel Tumbi ambaye alikuwa mkuu wa vikosi vya mizinga aliitwa "kamanda radi."Ahmed Takadiri Kitete alipewa jina la " kamanda supersonic. "

Baada ya vita vya Kagera Ahmed Kitete alikuwa mkuu wa operesheni na mafunzo wa Jwtz. Kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari jijini D'salaam.

Nakaribisha michango ya wengine wenye taarifa za Ahmed Takadiri Kitete shujaa na kamanda mahiri wa jeshi la wananchi wa tanzania

cc Echolima, Manyerere Jackton , gobore, Mohamed Said, Nguruvi3, gobore, The only
Tusiwasahau mashujaa wengine kama Jenerali Yusuf Himid wa Zanzibar aliyekuwa Mkuu wa Brigedi ya Tabora wakati tunavamiwa, na kikosi cha KMKM kilivyoonja mauti msitari wa mbele mwazoni kabisa. Hii inadhihirisha mshikamano wa Watanzania, khasa baada ya OIC kutuma askari wa Libya, PLO na Pakistan kuingia vitani kwa upande wa mwislamu "mwenzao" Idi Amin. Baadaye walijuta wakajirudi.
 
Mambo gani makubwa aliyoyafanya?? Kuuwa waislamu wenzie askari wa libya, Raia wa uganda wasio waislamu na waislamu/Civilians. Hayo ndio yakukumbukwa!!
 
Tusiwasahau mashujaa wengine kama Jenerali Yusuf Himid wa Zanzibar aliyekuwa Mkuu wa Brigedi ya Tabora wakati tunavamiwa, na kikosi cha KMKM kilivyoonja mauti msitari wa mbele mwazoni kabisa. Hii inadhihirisha mshikamano wa Watanzania, khasa baada ya OIC kutuma askari wa Libya, PLO na Pakistan kuingia vitani kwa upande wa mwislamu "mwenzao" Idi Amin. Baadaye walijuta wakajirudi.

..kweli kabisa.

..tulikuwa na askari wetu ambao walijitahidi kuzuia majeshi ya Amini yasivamie nchi yetu.

..na Brigade commander wao alikuwa Yussuf Himid, na nadhani battalion commander aliyekuwepo mpakani alikuwa Lt.Col.Maurice Singano.

..mchango wa vikosi vya Tanzania ambavyo vilikuwa vya kwanza kukabiliana na uvamizi wa majeshi ya Amin lazima utambuliwe.
 
1623015727686.jpeg

Kushoto: Brigedia Tumainieli Kiwelu kamanda mkuu wa operation chakaza.
Kulia: Kanali Ahmed Kitete mkuu wa mipango ya kivita operation chakaza.
 
Back
Top Bottom