- Thread starter
- #61
Siyo kweli;
Wakati wote wa vita hakukuwa na mabadiliko ya uongozi wa juu jeshini. Makamanda walikuwa wanaongezwa tu; walikuwa hawapunguzwi au kuhamishwa. In fact unakosea kunaposema kuwa General Mwakalindile alikuwa actintig chief of staff kwani wakati wa vita Mwakalindile naye alikuwa na brigade yake. Baada ya vita ndipo nafasi ya Kiwelu ikachukuliwa na Imran Kombe ambaye naye alikuwa amepigana huko frontline. Hawa wakuu wa majeshi wengi walipewa nafasi ama za kisiasa au za kiserikali, na General Kiwelu aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM mkoa wa Tanga.
..nimeweka interview ya Tumainieli Kiwelu post # 59.
..naomba uipitie halafu tuendelee kuhabarishana.
..pia tafuta kitabu, " Vita vya Kagera " kimeandikwa na Lt.Col.Ngatuni, Major.Kigadye, na Captain.Ghahae.