- Thread starter
- #41
..najua ningeandika kuhusu Bashite ungenisifia.
..vijana wa mataga / uvccm mna matatizo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwa msaada wa mitandaoKwa vile umemTAG Echolima tutapata uhakika na kuendeleza Historia hiyo
ila navyokumbuka Kamanda Mbogo ndiye aliyeipasua Uganda hadi kaskazini kabisa kuna wanaodai baada ya kupewa Kikosi cha Kamada Lupogo aliomba idhini ya kumkamata Nduli
Ila Kamanda Ben Msuya wa brigedi ya Tabora ndiye aliyeingia Kampala, baadaye nafasi yake kuchukuliwa na Kamanca Mayunga ambaye chini yake alikuwemo Brigedia Hemedi Kitete
luteni col Ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.
Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.
baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.
Ni wengi tu wa Makamanda wetu wanastahili sifa hizo ambapo hata kurasa ya JF itajaa
R.I.P. Kamanda Kitete
[QUOTE
HISTORIA FUPI YA MAKAMANDA. NA UPAMBANAJI WAO DHIDI YA NDULI IDDI AMIN (DADA)
Mwaka 1978 jeshi letu likuwa na Major General wawili tu, Major General Twalipo (aliyekuwa mkuu wa majeshi wakati huo) na Major General Sarakikya ambaye alikuwa balozi wetu huko Nigeria. Baadaya ya Major General kulikuwa na Mabrigadier sita au saba tu: Brigadier Marwa, Brigadier Musuguri, Brigadier Mayunga, Brigadier Walden, Brigadier Kiwelu, Brigadier Yusuf Himid nadhani na Brigadier Mkisi. Chini ya Mabrigadier kulikuwa na makanali kadhaa ikiwa ni pamoja na akina Moses Nnauye, Abdallah Natepe na wengineo.
Jeshi letu lilikuwa limegawanyika katika Brigade kama nne hivi: Kusini, Magharibi, Mashariki, na Zanzibar. Baada ya vita ile, ndipo Twalipo alipopandiswa cheo na kuwa Luteni General wakati Mabrigadier wale walipandishwa kuwa ma-major general;Muundo wa jeshi letu ukabadilishwa kidogo kuwa na division tatu. Miaka miwili baadaye Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General,ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General.
Kuhusu majina kama 'Black mamba" hayo yalikuwa maalumu au tunaweza kuita "usernames" ili kuficha utambulisho wao halisi hasa kwenye mawasiliano ya kijeshi vitani. Kila kamanda alikuwa na username yake.of course mengine yalitokana na jinsi kamanda alivyokabiliana na changamoto za kivita. Mfano Maj.Gen. Mwita Marwa (Kambale)aliitwa hivyo kwa sababu yeye binafsi na brigade yake walipigana wakiwa ndani ya maji kwa muda wa wiki mbili maji yanayofika kiunoni.Na bado walijitoa kimasomaso kukabiliana na adui. Brigade hiyo ilipata shida sana ya kuharibikiwa vifaa kama vile vya mawasiliano n.k.Radio za mawasiliano zote ziliharibika na maji.
KIPIGO CHA LUKAYA
Hapo mimi mwenyewe nilishiriki na nilijua kabisa kuwa sasa ushindi ni wetu baada ya kufanyia AMBUSH ambayo askari wengi wa Libya walipoteza maisha yao na wengine wengi kutekwa ilikuwa AMBUSH tamu sana yenye mashiko ambayo baada ya saa moja magari mengi sana yalionekana yakiwaka moto na Vilio vilikuwa vimetawala eneo hilo walisikika wakisema ALLAH-AKBAR enzi hizo mimi sikujua wana maana gani
Kilichonihakikishia ushindi ni Amin kuleta askari ambao wana uwezo kupigana Jangwani leo kawaleta kupigana kwenye misitu minene kama ya Uganda nilijua fika kuwa wata-Prove failer tu.Mateka waliletwa mpaka Dar-es-salaam Cha kilichowashangaza wengi ni kuwa walirudishwa makwao Bure kabisa Mwalimu alikataa Msaada wa mafuta kwa mwaka mzima ambayo Libya iliahidi kulipa kukomboa askari wao waliotekwa katika vita hiyo.Hapo Mwalimu alisema sisi hatufanyi Biashara ya kuuza watu. lakini kuna historia nzuri kuhusu kutekwa kwa mji wa kampala, ambapo Brig. Kiwelu (wakati huo) aliongoza mapambano kutokea lukaya, kuanzia usiku wa manane mfululizo kwa karibu masaa nane, BM 24 zikiunguruma na Kampala ikawa mikononi mwa jeshi la ukombozi.
Jambo jingine, Generali Mboma wakati huo alikuwa Pilot na ndiye aliyeongoza kipigo kilichoziacha ndege yingi za amini kwenye uwanja wa Entebe taabani. Kama mnakumbuka ndege yetu iliyotunguliwa na majeshi yetu wenyewe kwa bahati mbaya,Rubani wa kijeshi aliyetunguliwa kwa makosa na JWTZ alikuwa ni Capt. Alexander Kaleya Mshana. Basi hawa akina mbona waliondoka Ngerere bila kutoa taarifa kwa makamanda wa vikosi vya nchi kavu (Hili lilifanyika makusudi) na wakaruka hadi Uganda. This wa the most precise target JWTZ did. hadi Amin akalalamika kwamba JWTZ ina mamluki wa kukodiwa. Kwa sababu ndege za amini zilikuwa zinajianda kuja kushambulia TZ, lakini ghafla, wakajikuta Ndege zetu zinaruka chini sana usawa wa ziwa hivyo kusababisha taharuki kubwa sana, na kwa kuwa ziliruka chini sana na kwa mwendo wa SUPERSONIC yaani mwendo unaozidi sauti zilisababisha hofu kubwa na majengo mengi ya vioo vilivunjika-vunjika na wetu wengi walitibiwa kwa Presha,wakati huo Benki kuu ya Uganda nayo ikapigwa.
Battelfield tactics zilipangwa na Col. Lupogo.
Makamnada walioongoza vita walikuwa ni Brig. Marwa, Brig. Mayunga, Brig. Kiwelu, na Brigadier Walden. Hawa ndio waliongia msituni na wapiganaji. Makamanda hawa alipata vyeo vyao hivyo kutokana na umahiri wao wa katika uongozi wa kijeshi, na wote walihudhuria mafunzo ya uongozi wa kijeshi ndani na nje ya nchi mara kadhaa. Baada ya Uhuru hatukuwa na wasomi wengi katika majeshi yetu. In fact ni hawa hawa makamanda walioweka mkakati wa kuhimiza elimu jeshini na kuanzisha Elimu ya sekondari compulsory kwa wanajeshi wote na kuhimiza ajira za kijeshi kwa wasomi.
BRIG GEN MOSES NNAUYE
huyu alishiriki kama muhamasishaji ..ni muhimu sana kuwa na vikosi vya bendi na burudani...[ie Mwenge jazz,na kwaya ya Marehemu Luten komba...]Hawa walikuwa na wajibu wa kuhakikisha askari wanaburudishwa na kuliwazwa baada ya kazi ngumu...na kuwatia hamasa...na propaganda za ushindi...
CHANGAMOTO ZA VITANI
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu,Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu. ikimzunguzia Marehemu Gen. Imran Kombe. Katika makamanda waliopiganisha vita kitaalamu na kwa ufundi wa hali ya juu mmoja wao alikuwa ni Gen Kombe.
Gen Msuguri alikuwa siyo msomi Lakini mabrigedia wake walikuwa wanaelimu ya kutosha na ndiyo maana waliweza kupanga mashambulizi ya kiufundi, ungeweza kuona jinsi hivi vikosi vilikuwa vinasonga mbele kwa kasi basi ungeona haikuwa kazi ya kubahatisha. Kutokusoma kwa Gen Msuguri siyo hoja kwani alikuwa na uwezo wa kujua mapungufu yake na ndio maana alizungukwa na makamanda wazuri, na hiyo ni sifa kubwa kwa kiongozi.
Askari wa Lupogo walipata matatizo kwasababu walikuwa wanapigana na kikosi cha Amini kilichokuwa mlimani.Hivyo wao walikosa OP Obsevartion Post wakajikuta wanashambuliwa kirahisi.
kuna uwezekano kabisa kwamba Lupogo alipandishwa cheo kwa kuzingatia rekodi yake ktk vita nzima na siyo wiki tatu za mapambano ambayo alifanya vibaya. labda tatizo lilitokana na intelligence na military planning.
Lt.Col.Ben Msuya. Huyu ndiyo aliongoza utekaji wa jiji la kampala, na baadaye ku-act kama mayor wa kampala, mkuu wa itifaki, na mwisho kuandaa shughuli ya kuapishwa Yussuf Lule.
Lt.Col.Hassani Boma na Lt.Col.Mazora wametajwa kwa umahiri wao ktk medani ya vita.
Maj.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu" ndiyo aliingia kijiji cha koboko ambako alizaliwa Iddi Amini.
luteni col Ben msuya ..alistaafu jeshi akiwa MEJA JENERALI..na jukumu lake la mwisho alikuwa mkuu wa kamandi ya tabora...yenye jukumu la kuangalia hadi Kigoma, Rukwa ..Masaka na Mbarara zilikuwa smoothered na mizinga kabla ya kutekwa. Hapo hatukupoteza askari wengi.
Amini na askari wake waliingia uoga tangu wapigwe na kutolewa Kagera. walianza kudai kuna Wacuba,Wachina,...ati wanasaidia Tanzania.
baada ya Mbarara kutekwa Mayunga alipandishwa cheo kuwa Major General na kupewa Brigade mbili kuziongoza. Chini yake walikuwepo Brig.Hemedi Kitete[rip] na Brig.Roland Makunda.
Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.
Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.
Ndugu zangu, vita huwa havipiganiwi ardhini, angani au kwenye maji peke yake..., vita hupiganwa pia kwenye Media, na kuongeza chumvi hufanya watu wasife moyo na kuwapa motisha..., "Ingekuwa ajabu sana kama vyombo vya habari vya nchi yetu vingesema jana tulipigwa sana lakini leo afadhali tunajaribu kuwapiga........." Think about it..
Echolima ni kweli kabisa mimi ni mshabiki wako na wengine wengi wameQuote habari zako humu JF na kuzibadili au kuuondoa uhalisiakwa msaada wa mitandao
Ukwaju na JokaKuu Nawashukuru kwa kunikumbusha mbali sana!!Nimesoma na nimekumbuka kuna sehemu nyingi niliandika mimi kwenye JF Niliandika VITA VYA KAGERA- HISTORIA YANGU SEHEMU YA KWANZA,PILI NA YA TATU.Labda nipende kukurekebisha kwenye andiko lako Ukwaju umeandika hivi( Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General,ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General) Hapo ondoa neno KIKABADIRISHWA Sijui sentensi nzima hiyo uliitoa wapi maana kwenye andiko langu hakuna sentesi kama hiyo hata nakushukuru sana umenirudisha Frontline kama tulivyokuwa tunasema kipindi hicho!!!!
sawa Humphrey!..najua ningeandika kuhusu Bashite ungenisifia.
..vijana wa mataga / uvccm mna matatizo.
Ukwaju na JokaKuu Nawashukuru kwa kunikumbusha mbali sana!!Nimesoma na nimekumbuka kuna sehemu nyingi niliandika mimi kwenye JF Niliandika VITA VYA KAGERA- HISTORIA YANGU SEHEMU YA KWANZA,PILI NA YA TATU.Labda nipende kukurekebisha kwenye andiko lako Ukwaju umeandika hivi( Luteni General Twalipo alipandishwa cheo tena na kuwa General,ambapo chief of staff wa Jeshi akawa na cheo cha Luteni General. Baadaye sana cheo cha Brigadier kikabadilishwa na kuwa Brigadier General) Hapo ondoa neno KIKABADIRISHWA Sijui sentensi nzima hiyo uliitoa wapi maana kwenye andiko langu hakuna sentesi kama hiyo hata nakushukuru sana umenirudisha Frontline kama tulivyokuwa tunasema kipindi hicho!!!!kwa msaada wa mitandao
Kichuguu,
..niliamua kuanzisha uzi wa Brigadier.Ahmed Kitete kwasababu niliona ni mmoja wa makamanda wakuu wa vita vya Kagera lakini hakuwa maarufu kama makamanda wengine wakuu. Na katika makabrasha niliyosoma Ahmed Kitete anaonekana tangu mwanzoni mwa vita, eneo la Mutukula, mpaka kuingia ktk Arua alikozaliwa Iddi Amin.
Akiwa kanali pale ngome, Kitete ndiye aliyeongoza upangaji wa plani yote ya vita kwa jeshi zima; ila baada ya kupandishwa kuwa brigedia ikabidi aongoze brigedi yake tu.
Hapana; vitabu vingine vinaweza kuwa vinapotosha. Brigadia Kiwelu alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati Kanali Kitete alikuwa Tactical Commander wa JWTZ. Katika brigade za kwanza kuingia Uganda, Kitete hakuwa mmoja wao ingawa Kiwelu alijivua ukuu wa mkoa hadharani na kuchukua bridage moja kuingia nayo Uganda, ila baada ya jeshi kuongezea na kuundwa brigades kadhaa mpaka kufikia divisions tatu ndipo Kitete akawa brigade commander na kukabidhiwa brigade moja. Hata kanali Msuya aliyeteka Kampala alipanda kuwa brigade commander wakati vita inendelea...Kitete alikuwa pamoja na Kiwelu.
..Kiwelu ndio alipewa jukumu na Mwalimu Nyerere la kuandaa vita ya kumuondoa Amin ktk ardhi ya Tz.
..sasa ukisoma vitabu vya vita vya Kagera utawaona Kiwelu na Kitete wakiwa pamoja.
..baada ya majeshi ya Amin kufukuzwa ktk ardhi ya Tz Kiwelu alirudi makao makuu kuendelea na kazi yake ya Chief of Staff wa Jwtz.
..Kitete alibaki frontline na aliongoza moja ya Brigades zilizoingia Uganda.
Hapana; vitabu vingine vinaweza kuwa vinapotosha. Brigadia Kiwelu alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati Kanali Kitete alikuwa Tactical Commander wa JWTZ. Katika brige za kwanza kuingia Uganda, Kitete hakuwa mmoja wao, ila baada ya jeshi kuongezea na kuundwa brigades kadhaa mpaka kufikia divisions tatu ndipo akawa brigade commander na kukabidhiwa brigade moja. Hata kanali Msuya aliyeteka Kampala alipanda kuwa brigade commander wakati vita inendelea.
You are right somehow; nitakujibu baadaye kidogo, ngoja nijibu maswali mengine kwanza..source yangu ni kitabu kilichoandikwa na wanajeshi wa Jwtz.
..aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza nadhani ni Muhidin Kimario.
..Kiwelu alikuwa Chief of Staff 1975-- 1980 wakati wa Lt.Gen. Twalipo, na mwaka 1988 -- 1994, wakati wa Gen.Ernest Kiaro.
..source yangu ni kitabu kilichoandikwa na wanajeshi wa Jwtz.
..aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza nadhani ni Muhidin Kimario.
..Kiwelu alikuwa Chief of Staff 1975-- 1980 wakati wa Lt.Gen. Twalipo, na mwaka 1988 -- 1994, wakati wa Gen.Ernest Kiaro.
Kura Moco aka one voteIts true, linawezekana haswa kwa kuzingatia mimi mwenyewe baada ya JKT, nilikwenda straight JWTZ,
Kati ya kazi ngumu sana za utengenezaji documentary, ni documentary za vita. Kuna waandishi waliokuwa front line wawili nawakumbuka walikuwa AVI, Dickson Saileni na Dick Kaombwe, ila pia changamoto ni nyingi, inahitaji
1. Passion
2. Dedication
3. Commitment
4. Equipments
5. Contents Resourceful personnel
6. Financial Resources
7. Logistics
Kwa fani yetu high season hutokea mara moja kila baada ya miaka 5, by now mawazo yote ni October, ila everything is possible.
P
Kitete alikuwa ni Tactical commander wa Ngome, na alikuwa Kanali. Ndiye aliyepanga utaratibu wa kukabiliana na vita ile; wakati huo alikuwa Kanali. Chief of Staff (Kiwelu- samahani nilimchanganya na Kimario) na CDF (Twalipo) hawakupigana vita moja kwa moja bali walikuwa wanatoa uongozi juu wa jeshi. Hakuna brigade au division iliyoongozwa na Kiwelu au Twalipo; wao walikua juu ya jeshi lote. Baada ya jeshi kupanuliwa na kuwa na brigade nyingi ndipo mabrigade kamanda wengine wakahitajika hivyo wale makanali waandamizi wote wakawa mabrigadier moja kwa moja na kuchukua brigade hizo; Kitete, Msuya, Faki na Lupogo ni kati ya makanali waandamizi waliopanda kuwa mabrigedia na kuongoza brigade mpya wakati vita inaendelea.
..vita ilikuwa na awamu mbili.
..awamu ya kwanza, ya kumtoa Amin ktk ardhi yetu, ilipangwa na kuongozwa na Kiwelu.
..awamu ya pili, ambapo majeshi yetu yaliingia, Uganda iliongozwa na Musuguri.
..wakati Kiwelu yuko frontline, Martin Mwakalindile alikuwa acting chief of staff.
Hii ni ndefu; sijaisoma. Nikiisoma yote kwa makini nitakujibu.Kichuguu,
Raia Mwema: Hali ilikuwaje kule eneo la mapambano wakati wa vita ya Kagera?
Jenerali Kiwelu: Kazi ilikuwa ngumu sana. Maana vijana wangu waliokuwa kule mbele, wale askari wa JWTZ walikuwa katika nusu morali, maana ukishatoka kwenye mstari wa mbele ukarudi nyuma morali ya vita inapungua.
Kwa hiyo kazi ya kwanza ilikuwa kuwajenga kisaikolojia. Kazi ya pili ilikuwa ni kupata reinforcement (kuongeza nguvu) kazi ambayo niliyomwachia Ernest Mwita Kiaro, hata CDF naye alikuja akakaa mahala fulani pale Bukoba (jirani), kwa hiyo Dar es Salaam tulimpa kazi Mwakalindile ndiye aliyekuwa anakaimu kama Chief of Staff, halafu Kiaro, chifu wa mgambo kazi yake ilikuwa kukusanya mgambo wote nchini, akina Mwakalindile ni kukusanya JKT, Polisi na Magareza, wote walikuja kule.
Ninaposema kulikuwa na changamoto kubwa sana ni kwamba hawa askari hata siku moja hawakuwahi kuwa eneo la vita ama eneo la mafunzo ya kivita kwa pamoja. Kwa hiyo, ilikuwa kazi kubwa, ndiyo maana ikatuchukua muda pale kabla hatujaruka daraja, ilikuwa ni lazima nifanye mafunzo ya pamoja ili kuwaweka watu (askari kutoka Magereza, Polisi, Mgambo na JKT) waweze kufanya kazi pamoja.
Lengo ilikuwa kuondoa fikra za kitabaka vitani, kuachana na mambo ya huyu mgambo au JKT. Kwa hiyo nilianzisha range ya kupiga silaha, mtu unampa risasi kumi anapiga zote wash out (anakosa kulenga shabaha), maana sisi (jeshini) tuna kitu kinaitwa bull, inner, outer n.k… sasa huyu unampa risasi zote anapiga wash out, tunampa nyingine, akipiga ile target namwambia umepiga bega (target hasa ni kifuani kwenye moyo au kichwani) sasa wakati mwingine ukimpa risasi tano… mbili anapiga ndani, nikasema sasa wameiva.
Kwa hiyo ilikuwa ni mafunzo ya msingi. Kwa mfano, ukiwa porini na ndege ya adui inakuja ufanye nini.
Unaulizwa ukiona ndege ya adui inatoka kule wewe unakwenda wapi? Namna gani mnaweza kusonga mbele, mnajihami vipi na namna gani mnaweza kupumzika kwa sababu askari hawezi kupumzika chini ya kivuli cha mti. Sasa baada ya mafunzo hayo ya pamoja, tukaridhika askari wetu wameiva, tukaanza kusonga mbele kutoka Katoro hadi tukafika karibu na mpakani, tukaweka kambi ambayo mpaka leo ipo pale, nyuma ya Mtukula.
Raia Mwema: Labda ungeeleza kuhusu Daraja la Kagera kushambuliwa na adui?
Jenerali Kiwelu: Daraja hili wakati nimefika tu, kutoka kupewa ile amri (ya kwenda vitani)… nimefika Kaboya, siku hiyo hiyo jioni nikatoka kwenda kutazama daraja. Nikafika darajani upande wa kulia kama unakwenda Mtukula umbali wa kilomita moja, nikaliona daraja ambalo baada ya dakika 15 nikiwa pale likalipuka, kwa hiyo sikuweza kuwahi kuweka askari pale darajani.
Wakati nafika pale na mtu mmoja anaitwa Kanali Kitete tunatazama…nataka sasa kufanya mbinu namna gani nitavuka daraja ili majeshi yangu yakae upande mwingine.
Basi nikarudi zangu Kaboya kwa ajili ya kuanza kufanya mkakati mwingine maana pale daraja limekwishavunjwa, nikaripoti daraja limevunjwa…hakuna daraja kuanzia sasa. Ndipo tukaanza mipango mingine kuhusu daraja, tukaleta madaraja ya muda na mtu mmoja anaitwa Brigedia Rajabu ndiye aliyekuja na vifaa hivyo kutoka kikosi chetu cha uhandishi na tukamweka sehemu ya umbali wa kama kilomita tano kutoka kwenye daraja, ndipo alipofanya mafunzo yake ili baadaye kufunga daraja la muda.
Raia Mwema: Ilichukua muda gani hadi kufanikisha daraja hilo la muda?
Jenerali Kiwelu: Unajua kuna wanazungumza kwa ushabiki mambo ya vita tu wakati hawajui chochote kuhusu vita, watu hawa mimi nawaita majitu, hawajui maana ya vita. Wapo wengine wanafikiri jeshi hii la Tanzania lilikuwa tayari kwamba unakwenda tu kwenye vita, sasa ukiwaambia kwamba jeshi hili tulipokwenda kwenye vita tulikuwa na mchanganiyo wa watu wote hawa, halafu pia kuleta vifaa vya kuvuka daraja, kuwafundisha namna ya kuweka daraja, kuleta vifaru, ndipo wataona ugumu wa kazi iliyokuwapo.
Pale ni lazima uwe na nguvu ya kutosha kuhakikisha kwamba mkiruka (daraja) hakuna kurudishwa nyuma. Kama nilivyotangulia kusema wale askari wetu waliokuwa kule awali, walikuwa wachache na walivurumishwa na adui kiasi cha morali yao kuwa chini kivita, kwa hiyo ilikuwa ni lazima nihakikishe sasa watu wangu ni imara, vifaa viko.
Tulikuwa tunafanya mipango na ukaguzi pamoja na makamanda wangu, akina Jenerali Marwa, Jenerali Luhanga, Mayunga, Walden… tunakwenda hadi tunafika pale kwenye daraja kwa sababu Idi Amin alirudisha majeshi yake (Uganda) akiamini kazi imekwisha. Sasa tulikuwa na makamanda wangu hao tunakwenda pale kupanga mikakati, lakini, swali kwamba wapi tupite (kuvuka daraja) na lini sikuwaambia.
Hakuna mtu aliyejua hata Edward Sokoine (aliyekuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Mwalimu Nyerere) alikuja akaniuliza …. sasa General nafikiri tumechelewa sana kuruka (daraja), sasa unaruka lini na unapitia wapi?
Nikamwambia hiyo ni siri ya kijeshi… akasema hata mimi? Nikamwambia ndiyo mzee. Kwa hiyo mimi nilikuwa napita kando ya ule mto kwa gari hadi Murongo, halafu watu wanapiga mabomu kila sehemu lakini hawajui tunaruka wapi kupitia wapi.. .tuliweka watu (askari) hadi eneo la Kakunyu huku Bukoba Vijijini, kwa hiyo kuna ambao walijua tunaruka kupitia huko. Hatimaye nikaona sehemu ya kuruka ni pale pale walipovunja (daraja), lakini sikuwaambia wapiganaji wetu.
Sasa imefika siku ya kuruka, ndani ya saa 24. Nikawaita makamanda wangu nikawaambia sasa inabidi turuke kwenda kumshambulia adui, vifaa na kila kitu tayari, na askari kama tulivyofanya mafunzo wako tayari. Makamanda wakasema tunangoja tu amri yako, nikasema amri itatoka, wakauliza na kutaka niwaambie tunaruka kupitia eneo gapi, nikasema nitawaambia.
Ilipofika saa tano usiku nikawaambia makamanda… Marwa utakuwa katikati, Mayunga ukiruka tu unakwenda kushoto kuelekea eneo la Mbarara, Walden ukiruka tu unaelekea eneo la Minziro, Luhanga ukiruka tu unafuata njia ya Marwa halafu makamanda wengine watakuwa tayari kusubiri lolote (reserve). Baada ya maelekezo hayo nikawataka waende kuwaambia askari wao kwamba tunaruka leo (usiku huo), nikamwita Mhandisi Mkuu Rajabu na kumwambia utatandaza daraja lako (juu ya mto) saa nane usiku…akafanya kazi hiyo.
Saa nane usiku mpaka kufika saa tisa kuelekea saa 10 (takriban saa mbili hivi mfululizo) vikosi vikaanza kuruka kwa mujibu wa amri ya operesheni (operation order) ilivyotamkwa. Ilikuwa bahati mbaya nilipoteza askari mmoja tu pale wakati wa kuvuka daraja.
Baada ya hapo tulifanya mashambulizi, kazi ya kwanza ilikuwa ni kukamata eneo. Nimeeleza kazi niliyopewa nilitakiwa kurudisha heshima ya nchi hii na heshima ya nchi ni kurudisha mipaka yetu pale ilipokuwa awali na hivyo tukahakikisha tumefika Mtukula, wengine wamefika Minziro na wengine mpakani na Uganda kule.
Sasa jukumu la msingi la kurejesha mipaka ya nchi likawa limekamilika na Rais Julius Nyerere akaja kule na akasimama eneo lenye kilima pale na tukamweleza kwamba sasa mzee kazi ya kwanza uliyotutuma tumeimaliza, mipaka yetu sasa iko salama, akasema vizuri lakini huyu “mshenzi” huyu ametuharibia mambo mengi sana si bado yuko kule (nchini mwake), basi kazi bado haijakwisha.
Ndipo tukaingia hatua ya pili, maana sehemu ya kwanza ya ukombozi wa nchi yetu ikawa imekwisha ikafuata hatua hiyo ya pili ambayo ni kumwadhibu adui.
Raia Mwema: Je, baada ya kazi hiyo ya kwanza kukamilika ulirejeshwa kwenye nafasi ya Mnadhimu Mkuu (Chief of Staff)?
Jenerali Kiwelu: Pale kilichofanyika ni kwamba baada ya kumaliza ile kazi ya awali, tukaingia sasa kazi ya kuandaa na kutekeleza operesheni ya kuvuka mpaka ambayo ni tofauti na opereshani ya kumwondoa adui nyumbani kwako.
Sasa unakwenda nyumbani kwake lazima uwe na mkakati, sambamba na nguvu ya kutosha kwenda kwake, kwa hiyo rais ikabidi afanye utaratibu wa kumtafuta kamanda wa kuingia Uganda, mimi si ndiye niliyekuwa Chief of Staff na mkuu wa majeshi akiwa Twalipo ambaye naye hayuko makao makuu, kwa maana hiyo akiwa huku mbele (vitani) kule makao makuu hakuna maandalizi yoyote, nani anaanda nini… nani anafanya nini.
Kwa hiyo ilibidi nirudi Makao Makuu ya Jeshi Dar es Salaam na pale (vitani kuelekea ndani ya Uganda) nikamkabidhi Msuguri, mimi nakamwambia nakwenda (makao makuu) kukufanyia kazi ya kuandaa vifaa, wewe kazi yako ni kwenda ndani kumwadhibu Idi Amin. Nikarudi makao makuu nilikuwa na mtu mmoja alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi, Kanali Bakari, basi tukafanya kazi na Bakari, tunkaenda hadi nchi za nje kutafuta nguvu…. zana za kivita.
Wako marafiki walitusaidia, sina sababu ya kuwataja sana lakini kati ya nchi rafiki tulizokwenda ni pamoja na Urusi, China, Korea na Bulgaria. Ikabidi tukusanye vifaa na ndipo hapo wananchi walichangia mambo mengi sana, wapo waliojitolea magari yao, vyakula, mifugo kama ng’ombe ili kuwawezesha wapiganaji wetu kule mstari na hatimaye Msuguri akuvuka mpaka akiwa na uhakika wa nguvu za kutosha na uangalizi huku nyuma anakotoka.
Raia Mwema: Kwa wakati huo wewe ndiye uliyekuwa makao makuu Dar, sasa uliwezaje kudhibiti link (viunganishi vya taarifa) za silaha mlizopata kutoka nje ya nchi?
Jenerali Kiwelu: Kwanza wakati nikiwa pale Kagera tulikuwa tumedhibiti sana uvujaji wa taarifa. Unajua kuna mkutano mmoja mkubwa wa kimataifa ulikuwa unaendelea pale Arusha uliokuwa umehusisha nchi nyingi huku vita pia ikiendelea na hao washiriki wa mkutano hawakujua chochote kilichokuwa kikiendelea nilidhibiti uvujaji wa taarifa, viongozi wengine tuliwapa amri maalumu hakuna kufika kwenye eneo la vita na wala kupewa taarifa yoyote, ni kama tulivyokuwa tunapambana kuwasaidia kule Msumbiji siku moja tukakuta mzee mmoja wa kizungu kule Tunduru anayo redio ameijichimbia ndani, kumbe alikuwa anawasiliana kwa maana ya kupeleka taarifa, tukamkamata.
Hata pale Karagwe, tulikuwa na watu fulani pale ambao ni kanisa fulani sitaki kuwataja nao pia walikuwa na redio ya mawasiliano, ukiona utafikiri mtu anapiga kinanda kumbe anapeleka taarifa, kwa hiyo tukafunga njia zote za mawasiliano, nikasema hakuna mawasiliano ya aina yoyote na taarifa zozote kwenda Ikulu nitapeleka, tulihakikisha taarifa hazivuji vinginevyo tusingeweza kuvuka pale.
Raia Mwema: Vipi kuhusu Yoweri Museven (Rais wa sasa wa Uganda), alikuwa sehemu ya mapambano?
Jenerali Kiwelu: Museven yeye alitokea huku nyuma kapitia Karagwe kalala kijijini pale wakati Mayunga amekwishavuka mpaka, akaungana na Mayunga, ukweli ni kwamba Jeshi la Tanzania na chini ya Luteni Jenerali Mayunga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya kupita Mbarara na kutoka hapo kuelekea Kampala, na wengine wakapita Minziro kwenda kuungana kule. Museven hakuwa na jukumu la kuongoza ni kama alisaidia mambo kadhaa yakiwamo masuala ya taarifa.
Raia Mwema: Vipi kuhusu uteuzi wako kuwa mkuu wa mkoa?
Jenerali Kiwelu: Baada ya vita, tukawapokea vijana kutoka Uganda pale Bunazi, nikafanya kazi ya kuwasambaza na kuwarudisha kule walikotoka, wengine Ruvuma, Kigoma na maeneo mengine ya nchi. Tukahakikisha wamerudi na kupewa haki zao.
Baada ya kumaliza pale Bunazi, nikarudi Dar es Salaam kwenye kitengo changu cha Mnadhimu Mkuu, sasa makamanda wote wakawa wamerejea kutoka vitani. Ikabidi sasa jeshi lipangwe upya….unajua watu walikwishaonja kutoa roho za watu huwezi kucheza nao hivi hivi, ikabidi sasa tupangane upya.
Namna gani jeshi litakavyoendeshwa na kwa hiyo, Amiri Jeshi Mkuu akapanga upya…akasema sasa wewe bwana umemaliza kazi hii nakushukuru…sasa nataka kukupa kazi nyingine…nikamwambia sawa, nipo tayari kwa kazi yoyote, akaniambia utakwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, nikamwambia naenda lakini hii kazi sijawahi kufanya sasa ukiona nafanya vibaya uniite, na mimi nikiona kuna tatizo nitakuja. Kwa hiyo nikaenda zangu Tanga ndipo wakati huo yakafanyika mabadiliko, Twalipo akatoka pale akawa Waziri wa Ulinzi, Msuguri akawa Mkuu wa Majeshi halafu na Jenerali Kombe akawa Mnadhimu Mkuu, tukaendelea.