- Thread starter
- #21
Mkuu ulichoeleza ni sahihi kabisa na umeleta kumbu kumbu nzuri sana.
Baada ya vita huyu kamanda Kitete alikuwa maarufu nadhani kifo chake kilichotokea mapema kimechangia sana jina lake kutosikika. Nakumbuka ilikuwa kawaida kusikia ''supersonic'' au kumsikia Kitete.
Kuna tatizo kubwa sana katika kuweka kumbu kumbu za vita ya Kagera. Wapo watu walioshiriki na michango yao haielezwi. Tungewatumia akina Major General Msuya ambaye yupo kuweka kumbu kumbu sawa sawa.
Msuya naye ni kama Kitete, ushiriki wake hasa kuteka Kampala hauelezwi vema. Ni wachache sana wanaojua
Kuna askari kama akina Brigedia Ambrose Bayeke, huyu alikuwa na cheo kidogo wakati wa vita, lakini alipanda sana hata kuongoza vikosi vyetu kule Kongo. Ni watu wenye hazina ya historia ya JWTZ. Sijui yupo wapi
Mwingine ni Major general Maneno, naye kama Bayeke alikuwa ni afisa wa ngazi za kati.
Pengine washauriwe kuandika 'memoir ' na JWTZ iwasaidia katika kufanikisha hilo.
Nilimshauri Pascal Mayalla kupitia ''Media yake ya PP'' aandae documentary ya vita.
Nadhani Ambrose Bayeke ana mchango mkubwa ktk phase ya kwanza ya kuyatoa majeshi ya uvamizi ktk ardhi yetu.
Nasema hivyo kwasababu nimeona kuna mpaka picha za Bayeke akim-brief Mwalimu Nyerere alipowatembelea askari waliokuwa mstari wa mbele.
Kumbukumbu ya mwisho ya Brigadier.Ambrose Bayeke ni alipokuwa parade commander wa magwaride yote makubwa.