The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Brigedia Jenerali, Fransic Mndolwa alipofanya mahojiano na kituo cha Televisheni cha ITV kwenye kipindi cha dakika 45 Februari 10, 2025 alisema Wananchi kuongozwa haimaanishi hawana akili, kwani viongozi wanasaidia kusimamia kanuni ambazo zimekubalika, na kanuni hizo haziwezi kusimamiwa na watu wote kwani itakuwa ni fujo
"Wananchi kwa kuongozwa na kiongozi mmoja mfano mkuu wwa wilaya, mkuu wa mkoa hata Rais, Waziri sio kwamba wananchi hawana akili, hapana wana akili zao kila mmoja akipata nafasi anafikiria, huyu amepata nafasi ya uongozi hapa atafanya kazi za uongozi kuunganisha wenzake katika kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda, lakini sio kwamba yeye ana akili kupita wengine wote sasa tatizo lipo hapo. Mtu mwingine anapoambiwa yeye ni mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, anataka atakalosema yeye basi ni hilohilo hapana, lazima atambue wale anaowaongoza ni watanzania wenye hadhi sawa na yeye"
"Viongozi wanasaidia kusimamia kanuni ambazo tumekubaliana, kanuni haziwezi kusimamiwa na watu wote itakuwa ni fujo, lazima kuwa na mwenzenu mtaalamu anajua hiki kiko hivi anakumbusha ndo uongozi. Kuna watu wengine hawataki hata mawazo ya wananchi wa kawaida, kiongozi mzuri ni yule anayekubali kuongozwa, anapata ushauri wa wale anaowaongoza" alisema Brigedia Jenerali, Mndolwa
Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025