Not necessarily mkuu!
As far as I'm concerned, quality of service vs value for money kati ya BA na Emirates hazi tofautini sana.
Emirates wanaweza kuwa na ndege mpya zaidi, lakini gharama zao za tiketi kwenda Dar es Salaam ni juu ukilinganisha na BA.
BA wanachaji dola 60 kwa sanduku la pili la kilo 23, wakati Emirates wanaruhusu masanduku mawili ya kilo 23 bure kwa gharama unayolipia tiketi, lakini at end of the day ukipiga mahesabu utagundua kuwa gharama za BA na Emirates ni almost equivalent haswa kwa wale Wasafiri waliozoea kusafiri na masanduku mawili kama wale wanaotokea USA na Canada.
Tatizo lingine na BA ni kwamba Wasafiri wao kutoka USA na Canada kwa kawaida wanakuwa na layover time ya hadi masaa 12 kutoka London Heathrow, kitu ambacho Emirates watakuwa wamejaribu kudili nalo, lakini sidhani itasaidia sana, maana sanasana wanaweza kukutoa mapema London Heathrow, lakini utaishia kutumia muda wako wa kusubiri ukiwa angani kwenda Dubai na baadaye mara baada ya ndege kutua Dubai utakaa pale masaa kadhaa huku ukisubiri connection flight ya kwenda Dar, ambayo kwa sasa ni moja tu kwa siku.