Chris wood
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 1,667
- 5,043
Asee Christmas kwangu imekuwa ya hovyo balaa, naona kama imekuja niumbua.
Kwanza kabisa mimi ni kijana wa miaka 33 ni degree holder lakini mpaka sasa sina kazi ya kueleweka, jambo ambalo limefanya nishindwe kuwa na familia.
Maisha Dar yalinitandika haswa ikabidi nirudi kwa mama ndio mpaka sasa nilipo,.. Niliwahi bahatisha kazi kwenye berau de change Dar lakini 2018 December tulivamiwa ofisini na askari wakatukamata japo baadae tuliachiwa lakini kibarua kikaota majani .
Baada ya hapo nilitafuta kazi bila mafanikio nikashindwa lipa pango ikabidi niendee kukaa kwa sista aka kwa shemeji nimekaa pale sana bila mishe yoyote kama miezi 6, kumbe shemeji, alikuwa anachukia ikabidi wanitengenezee zengwe pamoja na sista.
Siku hiyo asubuhi mimi sina hili wala lile nasikia ugonvi kati ya sista na shemeji, baadae sista akakasirika sana akachukua mabegi akaondoka. Mimi nikabaki najiuliza nimfate sista au niendele kukaa kwa shemeji? Nikasema wee mjinga usinitanie hapa siondoki,
Baada ya siku mbili sista kaniambia ameshafika nyumbani, shemeji nae siku hiyohiyo akaniambia kesho inabidi uondoke ninasafari ya kikazi nashukuru alinipatia kiasi kidogo nikachukua vyangu nikasepa kurudi kwa mama maana nilikuwa sina jinsi
Nimerudi home haikupita hata wiki mbili sista huyo akarudi kwa mumewe, nilimuuliza sista kama naweza rudi akasema nitulie kwanza.... hali iwe shwali.
Bahati nzuri mwaka huu brother kapata dili kwenye kampuni kubwa hapo Dar es salaam, ikabidi nitumie fursa ya kilimo kupata mtaji kutoka kwake kwa makubaliano kuwa tutakacho pata faida nusu kwa nusu mtaji wake ubaki pale pale
Mpaka naandika hapa sijawahi pokea hata shilingi kumi jamaa hatujamuona baada ya danadana kibao juzi hapa tunasikia kakamatwa sijui hata nianzie wapi.
Brother nae kila muda anataka nimtumie picha za mazao juzi nilisikia anaongea na mother kwenye simu kuwa anaumwa hawezi kuja kula Christmas jana usiku akapiga tena kuwa kapata nafuu ameshakata tiketi ya kuja asee nilivyosikia nimechanganyikiwa.
Leo asubuhi nimetoka njee nikakuta mbwa wanafanya mapenzi wamenasiana asee hasira zangu zote nimemaliza kwao nimewatandika bakora za kiwango cha stieglas gorge
hadi raia wakaingila kati, toka asubuh sijarudi nyumbani napiga hesabu sijui nitamwambieje brother

Last edited: