Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Itakuwa ni jambo njema hana kashfa Mzee wa watu, ni mwenye huruma..........

Ila ikumbukwe kuna chatu mmeza watu ndani ya kampuni, Kibabu Tabasamu umakini na tahadhari dhidi yake unahitajika.
Na tujiandae na nusu mlingoti wa no 4 , anytime....

Na Wengi wanaofanya maandalizi na mipango ya kuhakikisha wanabaki kwenye viti hawatafika

Wataona ila hawatakula..,
 
Kuanzia leo

Ntakua naendesha Toyo yangu kwa uangalifu Zaidi kuliko msafara wa raisi mpaka mwezi wa 11 ili niyashuhudie haya nikiwa mzima wa afya akili na Moyo.

Isitoshe hata mapenzi napumzika saivi ili kisiwepo cha kunitenga na maono haya.

Na kama hayatatimia, Next year ntakua diasporah mpaka yatakayo timia haya maono.

Amandla.
 
Wakuu

1. Inahusiana na wewe kubaki bila kuondoka. Utaelewa vizuri katika wakati sahihi.
2. Utasimamia kufutwa kwa sheria ya kutoshtakiwa isipokuwa kwa mkuu kwa maamuzi aliyofanya akiwa madarakani ikiwa sio ya kijinai.
3. Hakutakuwa tena na mafao ya kudumu kwa viongozi wastaafu wala wenzi wao. Kila mmoja achangie kwenye mifuko ya pensheni.
4. Idadi ya wabunge iwe sawa na idadi ya halmashauri na mbunge lazima awe na masters degree.
5. Madiwani wawe idadi sawa na idadi ya kata na lazima diwani aanzie digrii moja na kuendelea. Madiwani wawe na mishahara rasmi.
6. Bunge liwe taasisi huru kama muhimili na utaratibu wa kujiendesha uwe nje ya usimamizi wa executive. Bunge liwe na mamlaka binafsi kwenye utendaji wake wa kazi.
7. Hapatakuwa tena na wakuu wa mikoa, ras, wakuu wa wilaya na das. Halmashauri ziongozwe na wakurugenzi kitaalamu na lazima wawe na masters na wapate kazi kwa kuomba na kufanyiwa usaili.
8. Posho zote zifutwe mara moja maana ndio chanzo cha matumizi holela na yasiyokuwa na tija katika taifa. Mishahara iboreshwe.
9. Kila mfanyakazi wa serikali ajitegemee kwa usafiri kama ilivyo kwa sekta binafsi isipokuwa kwa safari za kikazi hivyo magari yanayotumiwa kuwachukua na kuwapeleka watu majumbani yaondolewe.
10. Mgombea ubunge/udiwani/urais na mtu yeyote anayemsapoti asichangie kwenye kampeni zaidi ya kiwango fulani kitakachopendekezwa. Wagombea wapate support kutoka kwa raia kama kweli wanakubalika.
11. Wawajibishwe wote waliohusika na mashambulizi na mauaji ya watu mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni.
12. Fedha zilizokuwa zinatumika kulipa wakuu wa mikoa/wilaya, ras/das pamoja na ofisi zao zielekezwe kwenye kilimo na viwanda ili kuajiri vijana na kukuza uchumi.
13. Katiba ya Warioba ifanyiwe marekebisho kidogo sawa na andiko hili na ipitishwe kuwa rasmi kwa kura ya maoni.
14. Tume huru ya uchaguzi iundwe itakayojiendesha nje ya mfumo wa siasa. Mwenyekiti apatikane kwa kuomba nafasi, kufanyiwa usaili na kuthibitishwa na bunge.
15. Mtu asikamatwe wala kufunguliwa mashtaka kabla ushahidi haujakamilika isipokuwa kwa makosa ya jinai kama mauaji, ujambazi, ubakaji nk
16. Wizara ziwe fixed kwa idadi na taasisi zipelekwe huko kama idara ili kuondoa msururu wa tozo wanazolipishwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa kigezo cha uwepo wa vibali vya mamlaka mbalimbali.
17. Kodi zifahamike kwa uwazi na kuondoa malipo mengine yote ya halmashauri. Boresha mazingira ya kufanya biashara kuvutia uwekezaji zaidi.
18. Jenga kiwanda chetu cha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani maana soko ni la uhakika likiwemo lile la nje
19. Jeshi la polisi lifutwe na kuundwe usalama wa raia kama taasisi itakayolinda raia na mali zao na uongozi wake upatikane kwa uteuzi wa baraza la usalama la taifa na kuthibitishwa na bunge.
20. Pasiwepo na wizara chini ya rais bali ofisi yake isimamie wizara zote na halmashauri zisimamiwe na wizara.
21. Makamu wa rais afanye kazi ya kusimamia shughuli za kila siku za serikali, ofisi ya waziri mkuu ifutwe.
22. Rais akishindwa kuendelea na majukumu yake kwa kifo, kujiuzulu au tatizo la kiafya, bunge litapiga kura kumchagua raisi atakayetoka miongoni mwa wabunge watakaoomba. Makamu wa rais aruhusiwe kuomba.
23. Mahakama ijiendeshe kwa kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa kuomba nafasi, usaili na kuthibitishwa na bunge.
24. Usalama wa taifa iwe taasisi inayojiendesha kwa weledi na kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa mtu kupendekezwa na baraza la usalama na kuthibitishwa na bunge.
25. Hapatakuwa tena na uteuzi wa nafasi yoyote utakaofanywa na serikali kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya uma zikiwemo bodi. Watu waombe, wafanyiwe usaili na kuthibitishwa na bunge.
26. Asiwepo mtu yeyote atakayezuia uhuru wa maoni kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa mtu anayetukana. Maoni mengine yote yawe huru kwa kila mtu.
27. Serikali ipime ardhi yote ya nchi na kuhakikisha hati zinatolewa. Aidha kuwepo na standard za ukubwa wa ardhi unaotolewa inayoruhusiwa kupata hati.
28. Kusiwepo tena na mauzo ya mazao ghafi kwenda nje ya nchi na wageni wasiruhusiwe kwenda kwa wakulima bali kuwe na masoko ya kimataifa maeneo ya mipakani.
29. Serikali ifute mara moja utaratibu wa mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuwakopesha wananchi mikopo binafsi inayolipwa kwa mishahara. Benki zikopeshe biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.
30. Mpango wa makazi rasmi uanze mara moja ili kuondoa uholela wa makazi unaoendelea nchi nzima ambapo watu wanajenga baada ya kuuziana vipande vya ardhi.

Utahitaji kuwa na wafanyakazi wengi kama sasa hivi au upunguze wabaki wachache wanaolipwa vizuri na kuleta tija? Hilo pia utalifanyia kazi ili ajira nyingi zitokee kwenye sekta binafsi.

Natangulia kukutakia kazi njema.
Inahusiana na wewe kubaki bila kuondoka. Utaelewa vizuri katika wakati sahihi.👣
 
Umerudi tena kutuhadaa!, ile ya kwanza mlipatia kwasababu mlijua jamaa anaumwa!, yani ile mlipenyezewa mkajua kabisa kwa hili hatoboi!.
Sasahivi imebaki kubabia babia tu, Hakuna kinachoweza kujiri hapo kwa yote uliyoandika Tz bado sana tena bado mno!.
ukitaka kujua bado angalia uhalisia wa upeo wa watu wake wa kawaida ndo utaelewa!, maana katika ngazi ya nchi maendeleo huwa hayaletwi na huruma ya kiongozi!, huwa yanaletwa na u serious wa wananchi!.
Wananchi wanaweza kumuadabisha yoyote wanaemtaka na ndio wanaoweza kubadili mifumo.

Usiitarajie tz uliyoandika hapo bila kuwa na mabadiriko ya wananchi wake, kama wananchi sio welevu basi wajanja wachache wataichapa nchi wawezavyo!.
Kuna mkeka wake upo humu umechanika maana baada Uzi wa Magu watu walimuona kama Nabii humu
 
Hii naogopa.
Nafungua code kwa code kwa wale wasio elewa brother nani anapewa ujumbe.

Yohana 6:5-7
5 Yesu alipotazama aliona umati mkubwa wa watu wanamfuata. Akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ya kuwalisha watu hawa?” 6 Alisema hivi kumjaribu Filipo maana yeye mwenyewe ali jua atakalofanya.

Note
Kwenye bold Filipo ni Philip kwa kimakonde. Huyu Philip ndiyo Mpango mzima wa haya maelekezo.
Na Dini zipigwe marufuku, wenye imani waabudu majumbani kwao. Iwe marufuku kuhubiri dini hadharani.
 
Mkuu sawa asante, ila ningekuwa mimi ni miongoni mwa member huko na nina cheo, huyo alikuwa wa kumchomoa huko, asijue chochote kinachoendelea huko
Inawezekana role yake kimedani ni kubwa sana na wamemtengenezea jina aonekane hivyo lakini in the background sio lengo lao!!
Hiyo chatter tunayoijua yawezekana ni sisi TU lakini kwenye medani Kuna tafsiri toafuti na hiyo tuijuayo!!

Vitengo vimekua na product nyingi tofauti tofauti na zenye malengo tofauti ki utawala na mstakabali wa taifa!!

Huyo Mzee ndio alioleta unafuu was maisha kwetu na wengi wetu tulivyo leo kiuchumi,kielimu ni kutokana na Ile kauli mbiu "maisha Bora kwa kila mtz" na mchango wake unajulikana!

Kwasasa yawezekana wanamtumia kivingine kufanikisha maandiko hay yanayoandikwa jukwaani leo!!

Huyo Mzee na sarakasi zake zote akianguka Leo wengi tutamlilia sana,huwezi leta maisha Bora kwa wananchi bila kuachia na kulegeza mambo Fulani Fulani hasa mapesa halmashauri plus mikopo ya elimu na biashara!!

Ni lazima pia utaharibu baadhi ya mambo Ili kutengeneza uchumi was watu wengi!!kama Mzee Mwinyi!

Kina Ben,jpm na Brother ajaye hao ni wanamatengenezo na maumivu yake SI ya kitoto!!

Kina Mzee mwinyi,kikwete na Mama samiah hao waleta faraja baada ya mbinyo na kukamuliwa!!mambo yapo hivyo mkuu!!
 
Back
Top Bottom