Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

8. Mtu anayefanya kazi za ziada nje ya muda wake wa kazi kwanini asilipwe.?
Kama posho zinafutwa basi ziwe zile zisizo za lazima kama za wabunge au ziara viongozi kwani ni sehemu ya majukumu yao.

28. Wakulima wachache wenye uwezo wa kufikisha mazao yao katika masoko ya kimataifa.
Nafikiri wageni waruhusiwe kwa utaratibu maalumu ili soko liwe huria halisia lasivyo wakulima wadogo watanyonywa zaidi na wenyeji.

29. Kanuni za uchumi zinakataa.
Hela yote inayokopwa iwe ya mfanyakazi au mfanyabiashara inaenda kuchochochea uchumi.
Mfanyakazi anayekopa kujenga nyumba, atanunua vifaa vya ujenzi, atakodi usafiri, atalipa vibarua na mzunguko wa pesa unakuwa mkubwa.
Wafanyakazi kutoruhusiwa kukopa sio sawa.

Nb 1: Mishahara ipande/ishuke kulingana na shilingi yetu inavyopanda au kushuka thamani dhidi ya dola. Kwani imekuwa kawaida gharama za maisha kuwa juu wakati mishahara ni ileile


Nb 2: Taasisi nyingi hazina wafanyakazi wa kutosha. Hatujafika kwenye kiwango cha kusema tupunguze wafanyakazi ili waliopo walipwe vizuri.
Ni vizuri kufanya uchambuzi wa kina kujua wapi pa kuongeza na wapi pa kupunguza ila la muhimu zaidi ni kuboresha maslahi ya wafanyakazi hasa mishahara.
 
8. Mtu anayefanya kazi za ziada nje ya muda wake wa kazi kwanini asilipwe.?
Kama posho zinafutwa basi ziwe zile zisizo za lazima kama za wabunge au ziara viongozi kwani ni sehemu ya majukumu yao
Lkn kaongezea hii ".....mishahara iboreshwe."
 
Wakuu

1. Inahusiana na wewe kubaki bila kuondoka. Utaelewa vizuri katika wakati sahihi.
2. Utasimamia kufutwa kwa sheria ya kutoshtakiwa isipokuwa kwa mkuu kwa maamuzi aliyofanya akiwa madarakani ikiwa sio ya kijinai.
3. Hakutakuwa tena na mafao ya kudumu kwa viongozi wastaafu wala wenzi wao. Kila mmoja achangie kwenye mifuko ya pensheni.
4. Idadi ya wabunge iwe sawa na idadi ya halmashauri na mbunge lazima awe na masters degree.
5. Madiwani wawe idadi sawa na idadi ya kata na lazima diwani aanzie digrii moja na kuendelea. Madiwani wawe na mishahara rasmi.
6. Bunge liwe taasisi huru kama muhimili na utaratibu wa kujiendesha uwe nje ya usimamizi wa executive. Bunge liwe na mamlaka binafsi kwenye utendaji wake wa kazi.
7. Hapatakuwa tena na wakuu wa mikoa, ras, wakuu wa wilaya na das. Halmashauri ziongozwe na wakurugenzi kitaalamu na lazima wawe na masters na wapate kazi kwa kuomba na kufanyiwa usaili.
8. Posho zote zifutwe mara moja maana ndio chanzo cha matumizi holela na yasiyokuwa na tija katika taifa. Mishahara iboreshwe.
9. Kila mfanyakazi wa serikali ajitegemee kwa usafiri kama ilivyo kwa sekta binafsi isipokuwa kwa safari za kikazi hivyo magari yanayotumiwa kuwachukua na kuwapeleka watu majumbani yaondolewe.
10. Mgombea ubunge/udiwani/urais na mtu yeyote anayemsapoti asichangie kwenye kampeni zaidi ya kiwango fulani kitakachopendekezwa. Wagombea wapate support kutoka kwa raia kama kweli wanakubalika.
11. Wawajibishwe wote waliohusika na mashambulizi na mauaji ya watu mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni.
12. Fedha zilizokuwa zinatumika kulipa wakuu wa mikoa/wilaya, ras/das pamoja na ofisi zao zielekezwe kwenye kilimo na viwanda ili kuajiri vijana na kukuza uchumi.
13. Katiba ya Warioba ifanyiwe marekebisho kidogo sawa na andiko hili na ipitishwe kuwa rasmi kwa kura ya maoni.
14. Tume huru ya uchaguzi iundwe itakayojiendesha nje ya mfumo wa siasa. Mwenyekiti apatikane kwa kuomba nafasi, kufanyiwa usaili na kuthibitishwa na bunge.
15. Mtu asikamatwe wala kufunguliwa mashtaka kabla ushahidi haujakamilika isipokuwa kwa makosa ya jinai kama mauaji, ujambazi, ubakaji nk
16. Wizara ziwe fixed kwa idadi na taasisi zipelekwe huko kama idara ili kuondoa msururu wa tozo wanazolipishwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa kigezo cha uwepo wa vibali vya mamlaka mbalimbali.
17. Kodi zifahamike kwa uwazi na kuondoa malipo mengine yote ya halmashauri. Boresha mazingira ya kufanya biashara kuvutia uwekezaji zaidi.
18. Jenga kiwanda chetu cha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani maana soko ni la uhakika likiwemo lile la nje
19. Jeshi la polisi lifutwe na kuundwe usalama wa raia kama taasisi itakayolinda raia na mali zao na uongozi wake upatikane kwa uteuzi wa baraza la usalama la taifa na kuthibitishwa na bunge.
20. Pasiwepo na wizara chini ya rais bali ofisi yake isimamie wizara zote na halmashauri zisimamiwe na wizara.
21. Makamu wa rais afanye kazi ya kusimamia shughuli za kila siku za serikali, ofisi ya waziri mkuu ifutwe.
22. Rais akishindwa kuendelea na majukumu yake kwa kifo, kujiuzulu au tatizo la kiafya, bunge litapiga kura kumchagua raisi atakayetoka miongoni mwa wabunge watakaoomba. Makamu wa rais aruhusiwe kuomba.
23. Mahakama ijiendeshe kwa kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa kuomba nafasi, usaili na kuthibitishwa na bunge.
24. Usalama wa taifa iwe taasisi inayojiendesha kwa weledi na kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa mtu kupendekezwa na baraza la usalama na kuthibitishwa na bunge.
25. Hapatakuwa tena na uteuzi wa nafasi yoyote utakaofanywa na serikali kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya uma zikiwemo bodi. Watu waombe, wafanyiwe usaili na kuthibitishwa na bunge.
26. Asiwepo mtu yeyote atakayezuia uhuru wa maoni kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa mtu anayetukana. Maoni mengine yote yawe huru kwa kila mtu.
27. Serikali ipime ardhi yote ya nchi na kuhakikisha hati zinatolewa. Aidha kuwepo na standard za ukubwa wa ardhi unaotolewa inayoruhusiwa kupata hati.
28. Kusiwepo tena na mauzo ya mazao ghafi kwenda nje ya nchi na wageni wasiruhusiwe kwenda kwa wakulima bali kuwe na masoko ya kimataifa maeneo ya mipakani.
29. Serikali ifute mara moja utaratibu wa mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuwakopesha wananchi mikopo binafsi inayolipwa kwa mishahara. Benki zikopeshe biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.
30. Mpango wa makazi rasmi uanze mara moja ili kuondoa uholela wa makazi unaoendelea nchi nzima ambapo watu wanajenga baada ya kuuziana vipande vya ardhi.

Utahitaji kuwa na wafanyakazi wengi kama sasa hivi au upunguze wabaki wachache wanaolipwa vizuri na kuleta tija? Hilo pia utalifanyia kazi ili ajira nyingi zitokee kwenye sekta binafsi.

Natangulia kukutakia kazi njema.
Salute kwako mkuu safi kabisa 💯
 
Huu muendelezo wa nyuzi za huyu mheshimiwa naweza kuunga dot sasa. Mnyenyekevu anabaki na atasimamia reforms zitazozaa Taifa jipya la mfano. Mseminari na mtarajiwa atabakia alipopendekezwa na ndiye atasimamia pendekezo no.21. Bonge la draft *****!!
 
Shahada haidhihirishi uwezo wa kiongozi. Inaweza kuwanyima fursa watu wenye uzoefu wa vitendo lakini hawana stashahada.

Tengeneza mfumo wa kidigitali wa usajili wa ardhi ulio wazi kwa wote Mfano ule wa Tausi.

Mikopo kwa watu binafsi ni chanzo muhimu kwa uwekezaji wa ndani (k.m., kununua nyumba, kuanzisha biashara). Kusitisha ghafla kunaweza kushusha uchumi wetu. Nashauri tudhihibiti mikopo kwa viwango vya riba na masharti ya nafuu badala ya kuikataza.

Naunga mkono hoja. Uongozi uangalie CV ya mtu uadilifu wake, uzoefu wake na kazi alizozifanya kwa viwango huko nyuma na vetting ya uhakika.
 
Nakuunga mkono, isipokuwa kwa point 19 & 21. Jeshi la Polisi lisifutwe isopokuwa lifanyiwe marekebisho kimfumo na kikatiba/ kisheria.
Ofisi ya waziri mkuu isifutwe, ifutwe ofisi ya makamu wa rais
 
Done and dusted it seems!!walishasema kwenye ule Uzi walioufuta moderators"Usaliti wa jemedari wa marekani"kwamba original plan in and out, desert mission!!

Sasa wamekuja na hii,it seems desert mission ambayo ni no reforms no election imeleta panic na mwenyekiti akafanya makosa ya kimkakati ndani na nje ya mipaka na Sasa makosa hayo yamemuondolea uhalali wa kutia Nia awamu ya pili!!

Nadhani!
Makosa yamefanywa kwa kutokujua next move ya kila mission
Sasa ni hatari Mzee
 
Nakuunga mkono, isipokuwa kwa point 19 & 21. Jeshi la Polisi lisifutwe isopokuwa lifanyiwe marekebisho kimfumo na kikatiba/ kisheria.
Ofisi ya waziri mkuu isifutwe, ifutwe ofisi ya makamu wa rais
Ofisi ya makamu hawawezi futa sababu ya Muungano
 
Hii ndio ile briefcase..?
Siwezinkuweka sherehe,nasikitika coz yaliyopaswa kutokea yameschelewa na kama taifa tumerudi nyuma sana!!reforms zilipaswa zifanyike 2022 lakini mpewa jukumu hilo akasikiliza chawa na kuchagua maagizo aliyopewa na Hilo agizo kuu akaita "kijitabu"

Kifupi tumechelewa sana!!

Nasubiri kuona sarakasi za kumuingiza Brother!!
ile
 
Back
Top Bottom