Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Edmund mystic aliona utawala ujao ni wa chuma kweli kweli,yaani tutafunga mkanda kweli kweli,hii inamaanisha mchumi ndio atapewa na aliejiuzulu umakam ndio anaenda kupewa inavyoonekana!!

Kumbe kipindi kile amepotea haonekani alienda kupewa maelekezo!?Hadi tukavumisha kwamba!!!?

Sasa ni rasmi anapewa yeye!!na kweli ndie fdr anaingia bila kupigiwa kura kama yule wa america!!

Nadhani!
Mmmmh natamani tusiendelee na mama kwakweli
 
Execution approved?
Done and dusted it seems!!walishasema kwenye ule Uzi walioufuta moderators"Usaliti wa jemedari wa marekani"kwamba original plan in and out, desert mission!!

Sasa wamekuja na hii,it seems desert mission ambayo ni no reforms no election imeleta panic na mwenyekiti akafanya makosa ya kimkakati ndani na nje ya mipaka na Sasa makosa hayo yamemuondolea uhalali wa kutia Nia awamu ya pili!!

Nadhani!
 
Done and dusted it seems!!walishasema kwenye ule Uzi walioufuta moderators"Usaliti wa jemedari wa marekani"kwamba original plan in and out, desert mission!!

Sasa wamekuja na hii,it seems desert mission ambayo ni no reforms no election imeleta panic na mwenyekiti akafanya makosa ya kimkakati ndani na nje ya mipaka na Sasa makosa hayo yamemuondolea uhalali wa kutia Nia awamu ya pili!!

Nadhani!
"Brother"..ujio wa Tumia akili..umekugusa mno
 
Umejiandaa kufunga mkanda!!?

Hali itakua ngumu sana,posho za kibunge zote zitaondolewa,inawezekana wakashindia maji na karanga!!
Ni sawa tu kama tunatengeneza misingi thabiti ya nchi, taifa lilikuwa linaliwa utadhani halina watu watakaokuja baada yetu. Lazima ifike hatua tujue kutakuwa na wajukuu wa wajukuu zetu baada ya zaidi ya miaka 200 ijayo
 
"Brother"..ujio wa Tumia akili..umekugusa mno
Nimekua muumini wa kuzisoma nyuzi zake tangu ule wa 2020 was" Rais ambaye hajawahi kugombea,ilitokea marakani itatokea na huku" Hadi ule wa "usaliti was jemedari wa marekani" na ule wa FDR,na leo kanithibitishia hayakua maneno na kweli Desert mission ni hiyo "No reforms no election" ambayo imeleta kizungumkuti Kwa comrades na kufanya panic movement ambazo zinasaidia mlengwa FDR kushika japo kwa kuchelewa!!

Na marekebisho ya katiba ya warioba ni "zibaki mbili" kama alivyoandika kwenye uzi was "kitabu kilichoanza kuandikwa Kisha kikaachwa kitamalizika Kwa hesabu hii"

Zibaki mbili maana yake serikali mbili na sio tatu,no rasmi yawezekana mawaziri wasiwe wabunge tena!

Nawaza!
 
Wakuu

1. Inahusiana na wewe kubaki bila kuondoka. Utaelewa vizuri katika wakati sahihi.
2. Utasimamia kufutwa kwa sheria ya kutoshtakiwa isipokuwa kwa mkuu kwa maamuzi aliyofanya akiwa madarakani ikiwa sio ya kijinai.
3. Hakutakuwa tena na mafao ya kudumu kwa viongozi wastaafu wala wenzi wao. Kila mmoja achangie kwenye mifuko ya pensheni.
4. Idadi ya wabunge iwe sawa na idadi ya halmashauri na mbunge lazima awe na masters degree.
5. Madiwani wawe idadi sawa na idadi ya kata na lazima diwani aanzie digrii moja na kuendelea. Madiwani wawe na mishahara rasmi.
6. Bunge liwe taasisi huru kama muhimili na utaratibu wa kujiendesha uwe nje ya usimamizi wa executive. Bunge liwe na mamlaka binafsi kwenye utendaji wake wa kazi.
7. Hapatakuwa tena na wakuu wa mikoa, ras, wakuu wa wilaya na das. Halmashauri ziongozwe na wakurugenzi kitaalamu na lazima wawe na masters na wapate kazi kwa kuomba na kufanyiwa usaili.
8. Posho zote zifutwe mara moja maana ndio chanzo cha matumizi holela na yasiyokuwa na tija katika taifa. Mishahara iboreshwe.
9. Kila mfanyakazi wa serikali ajitegemee kwa usafiri kama ilivyo kwa sekta binafsi isipokuwa kwa safari za kikazi hivyo magari yanayotumiwa kuwachukua na kuwapeleka watu majumbani yaondolewe.
10. Mgombea ubunge/udiwani/urais na mtu yeyote anayemsapoti asichangie kwenye kampeni zaidi ya kiwango fulani kitakachopendekezwa. Wagombea wapate support kutoka kwa raia kama kweli wanakubalika.
11. Wawajibishwe wote waliohusika na mashambulizi na mauaji ya watu mbalimbali kwa miaka ya hivi karibuni.
12. Fedha zilizokuwa zinatumika kulipa wakuu wa mikoa/wilaya, ras/das pamoja na ofisi zao zielekezwe kwenye kilimo na viwanda ili kuajiri vijana na kukuza uchumi.
13. Katiba ya Warioba ifanyiwe marekebisho kidogo sawa na andiko hili na ipitishwe kuwa rasmi kwa kura ya maoni.
14. Tume huru ya uchaguzi iundwe itakayojiendesha nje ya mfumo wa siasa. Mwenyekiti apatikane kwa kuomba nafasi, kufanyiwa usaili na kuthibitishwa na bunge.
15. Mtu asikamatwe wala kufunguliwa mashtaka kabla ushahidi haujakamilika isipokuwa kwa makosa ya jinai kama mauaji, ujambazi, ubakaji nk
16. Wizara ziwe fixed kwa idadi na taasisi zipelekwe huko kama idara ili kuondoa msururu wa tozo wanazolipishwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa kigezo cha uwepo wa vibali vya mamlaka mbalimbali.
17. Kodi zifahamike kwa uwazi na kuondoa malipo mengine yote ya halmashauri. Boresha mazingira ya kufanya biashara kuvutia uwekezaji zaidi.
18. Jenga kiwanda chetu cha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na viwandani maana soko ni la uhakika likiwemo lile la nje
19. Jeshi la polisi lifutwe na kuundwe usalama wa raia kama taasisi itakayolinda raia na mali zao na uongozi wake upatikane kwa uteuzi wa baraza la usalama la taifa na kuthibitishwa na bunge.
20. Pasiwepo na wizara chini ya rais bali ofisi yake isimamie wizara zote na halmashauri zisimamiwe na wizara.
21. Makamu wa rais afanye kazi ya kusimamia shughuli za kila siku za serikali, ofisi ya waziri mkuu ifutwe.
22. Rais akishindwa kuendelea na majukumu yake kwa kifo, kujiuzulu au tatizo la kiafya, bunge litapiga kura kumchagua raisi atakayetoka miongoni mwa wabunge watakaoomba. Makamu wa rais aruhusiwe kuomba.
23. Mahakama ijiendeshe kwa kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa kuomba nafasi, usaili na kuthibitishwa na bunge.
24. Usalama wa taifa iwe taasisi inayojiendesha kwa weledi na kujitegemea na uongozi wake upatikane kwa mtu kupendekezwa na baraza la usalama na kuthibitishwa na bunge.
25. Hapatakuwa tena na uteuzi wa nafasi yoyote utakaofanywa na serikali kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya uma zikiwemo bodi. Watu waombe, wafanyiwe usaili na kuthibitishwa na bunge.
26. Asiwepo mtu yeyote atakayezuia uhuru wa maoni kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa mtu anayetukana. Maoni mengine yote yawe huru kwa kila mtu.
27. Serikali ipime ardhi yote ya nchi na kuhakikisha hati zinatolewa. Aidha kuwepo na standard za ukubwa wa ardhi unaotolewa inayoruhusiwa kupata hati.
28. Kusiwepo tena na mauzo ya mazao ghafi kwenda nje ya nchi na wageni wasiruhusiwe kwenda kwa wakulima bali kuwe na masoko ya kimataifa maeneo ya mipakani.
29. Serikali ifute mara moja utaratibu wa mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuwakopesha wananchi mikopo binafsi inayolipwa kwa mishahara. Benki zikopeshe biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.
30. Mpango wa makazi rasmi uanze mara moja ili kuondoa uholela wa makazi unaoendelea nchi nzima ambapo watu wanajenga baada ya kuuziana vipande vya ardhi.

Utahitaji kuwa na wafanyakazi wengi kama sasa hivi au upunguze wabaki wachache wanaolipwa vizuri na kuleta tija? Hilo pia utalifanyia kazi ili ajira nyingi zitokee kwenye sekta binafsi.

Natangulia kukutakia kazi njema.
Usiniambie kuna mtu anapewa rehersal huko ya vipaumbele vya taifa.
 
Lakini bila hii mikopo kuna watu wasingemiliki nyumba au mali walizonazo sasa.

Nidhamu ya kutunza fedha mwenyewe uje kujenga au kupata mtaji wa kuanzisha biashara kisha iweze kukopesheka shida kubwa sana kwa watu wengi.

Ningeshauri kuwe na kanuni nzuri za kudhibiti kiwango Cha hii mikopo na kukataza taasisi moja kununua deni na kumkopesha tena mdaiwa. Hii ni vicious cycle ya madeni hadi kusababisha utumwa na sonona.

Hili kaliangalieni huko kwenye vikao vyenu wa serikali iliyo kwenye kina kirefu(deep state).
Debatable.
 
Shahada haidhihirishi uwezo wa kiongozi. Inaweza kuwanyima fursa watu wenye uzoefu wa vitendo lakini hawana stashahada.

Tengeneza mfumo wa kidigitali wa usajili wa ardhi ulio wazi kwa wote Mfano ule wa Tausi.

Mikopo kwa watu binafsi ni chanzo muhimu kwa uwekezaji wa ndani (k.m., kununua nyumba, kuanzisha biashara). Kusitisha ghafla kunaweza kushusha uchumi wetu. Nashauri tudhihibiti mikopo kwa viwango vya riba na masharti ya nafuu badala ya kuikataza.
Kwa sasa elimu ya shahada ni basic. Ni lazima ibakie hivyo. Huo sio uongozi wa kichief. Kama unaluweza utakuwa mjumbe tu.
 
Ni sawa tu kama tunatengeneza misingi thabiti ya nchi, taifa lilikuwa linaliwa utadhani halina watu watakaokuja baada yetu. Lazima ifike hatua tujue kutakuwa na wajukuu wa wajukuu zetu baada ya zaidi ya miaka 200 ijayo
Kwani imeshafanyika,maana umeandika past tense as if imeshatokea
 
Back
Top Bottom