Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

Unaruka ruka tu, umeomba katiba umepewa, unatoka nje ya mada kwa ujanja wa kitoto kabisa.
 
Finland na lithuan wamejiunga NATO na majiran wakaribu wa Urussi kwanini hajawashambulia
 
acha utoto,

umeomba kujua ikiwa katiba ya ukraine inatambua hilo la wao kujiunga nato, nimekupa!

so far inaonekana uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo,
Haya, chukua point tusipotezeane muda kwenye ignoratio elenchi.
Katiba iliyofanyiwa hayo marekebisho mwaka 2019 inahusiana vipi na uvamizi na uporaji wa Crimea mwaka 2014?
 
Kwani Ukraine ilikuwa ina uhasama gani na Russia ?
Kati ya Russia na Ukraine nani alikuwa na uhasama na mwenzake?
 
World Bank ilikuwa ikiikopesha Russia mabilioni ya $dola mpaka mwaka 2014. Na kuna wakati ndio ilikuwa mchangiaji mkubwa zaidi katika sekta yake ya utumishi wa umma.

USAID imeipa Russia mamilioni ya dola za misaada mpaka mwaka 2012, imeisaidia kukarabati katiba yake kuongeza uhuru kwa raia, imeisaidia kurekebisha sheria zake kodi za ardhi.
 
Huo sio ukweli, Ukraine haijawahi kuwa na utaratibu wa viongozi kubadilishana madaraka kati ya Pro-west na Pro-Russia. Viongozi wote wa nyuma waliotangulia kabla ya Viktor Yanukovych hawakuwa na upande wowote, walikuwa neutral. Viktor Yanukovych aliyechaguliwa mwaka 2010 ndiye aliyeanzisha vurumai za Pro-Russia na Pro-Russia West kutokana na kuwa fisadi aliyepitiliza na maslahi binafsi makubwa ya biashara huko Russia.
 
Putin ni jasusi mzalendo mno kwa nchi yake alijua bila kuwasogeza NATO mbali na moscow hao jamaa ipo siku watamgeuka vibaya , walikubaliana vizuri nchi zilizotoka ussr zisijiunge na NATO lakini nato akazinganisha kama nchi nane hivi tena kwa suprise ndo mbabe akaona akae chonjo
 
Sababu waliyotoa Russia ya kuivamia Georgia mwaka 2008 ni madai ya kwamba serikali ya Georgia ilikuwa ikifanya mauaji ya kimbari"genocide" dhidi ya South Ossetia ambao walikuwa waasi wanaotaka kujitenga kama kule Donbas.
 
upo sahihi sana
 
Putin na Tucker Carlson walikuwa wanapiga story za Russia na Ukraine jinsi walikuwa wamoja enzi hizo za Ivan the Terrible! Ni kihoja na upuuzi mtupu.
Baada ya vita vya pili vya dunia mataifa yote walikubaliana mipaka ya nchi iliyokuwa ikisimama wakati huo ndio itaendelea kuheshimiwa daima, walikubaliana watu wasirudishe historia tena nyuma ya zama hizo za giza kudai maeneo fulani ya nchi nyingine au nchi nyingine kuwa zilikuwa ni sehemu yake.
 
Finland na lithuan wamejiunga NATO na majiran wakaribu wa Urussi kwanini hajawashambulia
Urusi haiwezi kuishambulia Finland kwa sababu tangu uvamizi wa USSR kwa Finland mwaka 1940 uliozua Winter War Finland imekuwa ikijiandaa kikamilifu kivita na Urusi wakati wowote.
 
Kwani Ukraine ilikuwa ina uhasama gani na Russia ?
Kati ya Russia na Ukraine nani alikuwa na uhasama na mwenzake?
Russia hakua na uhasama na Ukraine ila Ukraine kumkaribisha US ndio shida ilipoanzia
 
Haya maneno ya vijiweni mtu yeyote anaweza kuyasema, muhimu ni ushahidi.
Ni mjinga tu asiyeona huu ukweli hata vita vya pili vya Dunia wafadhili wakubwa ni makampuni ya kimarekani
 
Kwamba urusi hana uwezo wa kuivamia hiyo nchi dhaifu Zaid ya Ukraine?acha kujiaibisha nafuu unyamaze tu
Urusi haiwezi kuishambulia Finland kwa sababu tangu uvamizi wa USSR kwa Finland mwaka 1940 uliozua Winter War Finland imekuwa ikijiandaa kikamilifu kivita na Urusi wakati wowote.
Ba
 
Hivi wewe unaishi wapi. Unafaham chochote kuhusu Palestina na Israel, unafahamu chochote kuhusu Gholan Height, unahamu chochote kuhu mgogoro wa Tanzania na Malawi na msimamo wa Uingereza....

Yapo mengi ya kujifunza na kuelewa nini kinapelekea migogoro hiyo na kisha linganisha na ulichosema kuhusu makubaliano baadà ya WWII. Na misimamo ya mabeberu.

Congo haina amani sio bahati mbaya
 
Palestina haijawahi kuwa taifa na pia mgogoro wa Malawi na Tanzania ni mwepesi sana na wapiga porojo tu ndio huwa wanaukuza, sheria ya kimataifa kuhusu mpaka wa ziwa au mto ni kwamba mpaka unakuwa katikati ya ziwa au mto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…