aise
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 5,175
- 16,488
Habari za usiku wakuu! Kuna mtoto wa miaka 10 amekutwa amejinyonga chumbani kwake hapa Buguruni.
Maelezo ya kina hayajapatikana ila kwa maelezo ya awali ni kwamba mtoto katoka shule mida ya saa tisa jioni na baada ya kufika nyumbani amefanya shughuli ndogo ndogo na baada ya muda umeingia chumbani na kujifungia humo.
Dada wa kazi baada ya kuona huyu mtoto kajifungia ndani kwa muda mrefu akaanza kupiga hodi ili mtoto afungue mlango.
Amepiga hodi sana baada ya kuona kimya na tayari hapo ni jioni kama saa 11 ikabidi atafutwe fundi avunje kitasa waingie ndani.
Baada ya kuingia ndani ndipo wakamkuta mtoto amejinyonya kwa kufunga kamba kwenye dirisha.
Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango.
Maelezo zaidi watakuwa nayo polisi baada ya kufanya uchunguzi wao