Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Wangeenda na shule
Huenda kuna kitu kafanyiwa huko shule
Abuse imezidi sana na watoto hawako wazi kwa wazazi kisa kipigo

Mzazi anakuwa adui na mtoto, sasa matatizo yake ayapeleke wapi?

Wafundisheni watoto kuwa kujinyonga ni moto wa milele
Watoto wafundishwe pindi wakiwa wadogo
 
Hawa madada wa kazi nao wengine ni wa ajabu. Isije ikawa mtoto ameuawa, kisha akafungiwa ndani. Kuna wadada wa kazi wakiudhiwa na waajiri wao, wanaenda kulipizia kwa watoto.

Wazazi kuweni makini sana katika kuwapata wadada wa kazi, hasa unapokuwa na watoto.
Ni sahihi kabisa mkuu.
Na siku hizi huu mtindo wa kutumia madalali/Watu baki kutafuta wadada wa kazi sio mzuri kabisa.
Kwa vile mtu anakuwa na shida na uhitaji wa haraka anashindwa hata kutuliza akili kumpeleleza vizuri dada wa kazi kabla hajafika kwake. Hii ni mbaya, mbali ya binti kuleta matatizo lakini hata binti mwenyewe anaweza kupata matatizo na usijue pa kuanzia.
 
Habari za usiku wakuu! Kuna mtoto wa miaka 10 amekutwa amejinyonga chumbani kwake hapa Buguruni.

Maelezo ya kina hayajapatikana ila kwa maelezo ya awali ni kwamba mtoto katoka shule mida ya saa tisa jioni na baada ya kufika nyumbani amefanya shughuli ndogo ndogo na baada ya muda umeingia chumbani na kujifungia humo.

Dada wa kazi baada ya kuona huyu mtoto kajifungia ndani kwa muda mrefu akaanza kupiga hodi ili mtoto afungue mlango.

Amepiga hodi sana baada ya kuona kimya na tayari hapo ni jioni kama saa 11 ikabidi atafutwe fundi avunje kitasa waingie ndani.
Baada ya kuingia ndani ndipo wakamkuta mtoto amejinyonya kwa kufunga kamba kwenye dirisha.

Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango.
Maelezo zaidi watakuwa nayo polisi baada ya kufanya uchunguzi wao
Hizi movie zinamaliza wanetu, kaona kwenye muvi mtu kakerwa au kakwazika kaenda kujiua, na yeye anaiga anajua ndo suluhisho lilipo.
 
Mwili tayari umepelekwa Kwenye makazi ya milele, anapelekwa Nyanda za Juu Kusini huko.
 
Back
Top Bottom