Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Dah 🙆🏿‍♂️
Hata Watoto huwa wanapitia nyakati ngumu pia nakumbuka nilipokuwa na miaka 11 kuna mtoto mwenzetu alichukua uamuzi kama huo. Alichukua zile kamba za nailon za kufungia marobota ya mitumba akafunga kwenye mbao iliyokuwa inashikiria roof ya velandar bahati nzuri alipojiachia tu ile mbao ikavunjika maana ilikuwa imeshaliwa na dumuzi ilikuwa imebaki na muonekano mzuri lakinj ndani ilikuwa imebaki unga tu.

Sababu kubwa ilikuwa ni manyayaso ya Mama yake mzazi alikuwa anamtumikisha sana na maneno ya kumtukana yaani hakuna jambo alilolitenda lilikuwa jema mbele ya Mama yake.
Kama Mama yangu tu. Hakuwahi kuwa mwema wala kuwa na jema. apumzike kwa amani.
 
Habari za usiku wakuu! Kuna mtoto wa miaka 10 amekutwa amejinyonga chumbani kwake hapa Buguruni.

Maelezo ya kina hayajapatikana ila kwa maelezo ya awali ni kwamba mtoto katoka shule mida ya saa tisa jioni na baada ya kufika nyumbani amefanya shughuli ndogo ndogo na baada ya muda umeingia chumbani na kujifungia humo.

Dada wa kazi baada ya kuona huyu mtoto kajifungia ndani kwa muda mrefu akaanza kupiga hodi ili mtoto afungue mlango.

Amepiga hodi sana baada ya kuona kimya na tayari hapo ni jioni kama saa 11 ikabidi atafutwe fundi avunje kitasa waingie ndani.
Baada ya kuingia ndani ndipo wakamkuta mtoto amejinyonya kwa kufunga kamba kwenye dirisha.

Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango.
Maelezo zaidi watakuwa nayo polisi baada ya kufanya uchunguzi wao
Ameacha ujumbe gani mkuu? Huyo atakuwa kanyongwa sio bure. Mtoto mdogo ana changamoto gani hadi kujinyonga? Serikali ifanye uchunguzi wa kina.
 
Ameacha ujumbe gani mkuu? Huyo atakuwa kanyongwa sio bure. Mtoto mdogo ana changamoto gani hadi kujinyonga? Serikali ifanye uchunguzi wa kina.
Mpaka jana begi lake la shule limepekuliwa kuona kama kuna ujumbe wowote kauacha lakini hakuna ujumbe wowote.
 
Wabanwe kende ukweli ujulikane.
Miaka 10 anajinyonga kwa sababu ipi?
Hana mpenzi hana stress za pesa nk
Hawa madada wa kazi nao wengine ni wa ajabu. Isije ikawa mtoto ameuawa, kisha akafungiwa ndani. Kuna wadada wa kazi wakiudhiwa na waajiri wao, wanaenda kulipizia kwa watoto.

Wazazi kuweni makini sana katika kuwapata wadada wa kazi, hasa unapokuwa na watoto.
 
niliwahi kujaribu kujiua nikiwa na miaka 11 nilimimina madawa ya mifugo kwenye soda fanta lakini sikuumwa hata tumbo. sishangai kwa huyo mtoto inawezekana kabisa. stress sio watu wazima pekee. mimi ilikua nina ugonjwa fulani ukawa unanipa shida sana kwenye maisha ya kila siku.
 
Unachuki na Walimu we bumunda.

Kwanini USISEME wazazi wake?

Kama aliuziwa na Mwalimu SI angejinylngea vyoo vya shuleni??

Tumia akili bichwa kubwa akili kisoda
No sio chuki mkuu,Mimi mwenyewe mwalimu ila alichoongea huyo mdau Yuko sahihi ,hawa watoto wanapitia magumu sana huku shuleni bila ya mzazi kujenga ukaribu na mtoto wake haya yaweza mkuta,

Yawezekana mtoto kabakwa/kanajisiwa na mwalimu na kutishiwa adhabu ikiwa atafichua Siri,Sasa kutokana na fadhaa kaamua kujiua,huoni kesi za walimu kubaka/ kunajisi wanafunzi ni nyingi sana siku hizi!?
 
Wamechukuliwa na Difenda usiku huu huu.
Lakini dogo kaacha maswali mengi sana.
Maana ametoka shule vizuri, hapa mtaani kuna mama anauza sambusa dogo amenunua sambusa vizuri, kaenda nyumbani kafua sare zake za shure vizuri, baada ya hapo kaingia chumbani ikawa mwisho wake
Au sambusa zake zilipotea?Dada aseme tu.
 
Back
Top Bottom