Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Buguruni, Dar: Mtoto wa miaka 10 akutwa amejinyonga chumbani kwake

Huyo fundi ,dada wa kazi ,kaka wa marehemu wamekurupuka kuvunja mlango bila kufuata process za kuita mjumbe/mwenyekiti wa mtaa then wao ndiyo wawaite polisi then wajke kuvunja mlango ,kimasihara masihara unaweza kwenda kuisaidia polisi hata miaka 7 kwa uzembe tu.
Miaka7 kwa kuvunja mlango wa nyumba yako mwenyewe ili ujaribu kuokoa uhai wa nduguyo?
 
Unachuki na Walimu we bumunda.

Kwanini USISEME wazazi wake?

Kama aliuziwa na Mwalimu SI angejinylngea vyoo vya shuleni??

Tumia akili bichwa kubwa akili kisoda
We nawe huna akili kabisa, mimi kuna mjukuu wangu yupo darasa la pili somewhere, kuna siku mwalimu alimchapa kisa kavaa sweta la kawaida ajavaa lile la rangi ya taifa,na sweta wakalichukua,kumbuka siku iyo mvua ilikuwa imenyesha, baridi,na mtoto ana miaka nane wa kike tena, basi wakampora sweta wakalifungia stoo, ok,

Next day tena akataka amchape kisa sijui kwann kanunua sambusa nje wakati mwalimu yeye anauza mandazi darasani, mjukuu akagoma kuchapwa,maana jana yake walimchapa hadi kidole kikavimba, basi akamuuliza chagua nikuchape au uende ukamuite mzazi,mtoto akasema mi jana umenichapa sababu ya sweta hadi nna maumivu kwenye kidole,na leo unataka kunichapa tena,

Dogo akaondoka akaja kunishtakia babu yake,kiukweli nilimfuata yule mwalimu kwa ukali hswa,


Mkuu hawa walimu wa shule za msingi wamevurugwa na maisha sometimes wanawapa stress watoto,usiwatetee kabisa,kwani kuna kesi ngapi walimu wameua watoto? Walimu wengine madishi yameyumba,


Iyo shule juzi kuna mwalimu kasimamishwa kisa anawakaza wanafunzi wa kike,na kuwasumbua kuwatongoza.
Japo huyo aliyejinyonga haijulikani sababu nini,polisi ndio kazi yao watajua.
 
Mpaka majirani wote waliokua wanasaidia kwenye mchakato na kutoa ushauri nao 7 years?

"Hamza Kanuni" -Sheria haina macho.

Kama majirani nao wameshiriki kuvunja mlango hao waliochukuliwa kama watawataja na wao wanaweza kuchukuliwa kwenda kuisaidia polisi kwenye uchunguzi na ikithibitika kama hawahusiki wanaachiwa wote ,tatizo uchunguzi wa kesi kama hizo unachukua muda mreffu.
 
"Hamza Kanuni" -Sheria haina macho.

Kama majirani nao wameshiriki kuvunja mlango hao waliochukuliwa kama watawataja na wao wanaweza kuchukuliwa kwenda kuisaidia polisi kwenye uchunguzi na ikithibitika kama hawahusiki wanaachiwa wote ,tatizo uchunguzi wa kesi kama hizo unachukua muda mreffu.
Duh!! Aisee... 🤔🤔
 
kabla ya askari kufika watu kibao wamesha jazana ndani pale.
Si unajua mazingira ya uswahilini na elimu kwenye haya mambo ni kama hatuna.
Walichukua kisu wakakata ile kamba aliyojinyongea marehemu (nimesikia wanasema hili ni kosa lilifanyika)
Kwamba ilitakiwa askari ndiyo waje wamtoe pale kwenye kitanzi.
Ile kamba ina kazi kubwa kwenye ulimwengu mwingine
 
Msaada gani huo wakushusha maiti kutoka kwenye kamba ya kujinyongea bila ya jeshi la polisi kuwepo!? Labda mngesema mtoto mmemkuta kwenye kamba anapaparika ikabidi mumuwai kukata kamba hapo kidogo mnaweza mkaeleweka, tena na lazima mtoto angekua hai sema taabani!!
Sasa bila kuvunja mlàngo kujua humo ndani kuna nini wangefanyaje? Maana aliyeita fundi kuvunja mlango na fundi wote lock up. Wewe unaona sawa?
 
Kamba iliyotumika ni zile kamba za vipochi vya akina dada.
Sasa bado kuna sintofahamu maana dogo alikuwa bonge yule, ukiangalia na ile kamba pale ilipofungwa bado kuna kama ukakasi.
Miaka ya nyuma Sana nikiishi wilaya ya hai Kuna kifo kilitokea mtoto akajinyonga na shuka lililokuwa limeanikwa kwenye kamba, balaa lilikuja kwenye kuchimba kaburi watu walipigika ila kaburi liligoma ikabidi azike hivyo hivyo kwenye kaburi fupi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango"
haishi na wazazi wake (baba na mama)?
je anaishi na mama wa kambo?
 
"Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango"
haishi na wazazi wake (baba na mama)?
je anaishi na mama wa kambo?
Anaishi na wazazi wote wawili baba na mama.
Wazazi wake ni wale wa kutoka asubuhi kurudi usiku.
Nasikia wana biashara zao kariakoo
 
Wabanwe kende ukweli ujulikane.
Miaka 10 anajinyonga kwa sababu ipi?
Hana mpenzi hana stress za pesa nk
Tatizo lililopo baadhi ya muvi ambazo zinaonyeshwa majumbani zinabeba maudhui ambazo siyo sahihi kuangaliwa na watoto.
Mtoto itakuwa kajifunza kupitia muvi alizoangalia kuwa kujinyonga ni moja ya ufumbuzi wa changamoto anazokutana nazo mwanadamu katika maisha yake.
Saa nyingine kaudhiwa na huko shuleni na Mwalimu au mwanafunzi mwenzake akaona dawa ni kujinyonga.
Kupitia muvi watoto wa siku hizi wanajua mapenzi, ujambazi na hata uvutaji bangi nk.
 
Habari za usiku wakuu! Kuna mtoto wa miaka 10 amekutwa amejinyonga chumbani kwake hapa Buguruni.

Maelezo ya kina hayajapatikana ila kwa maelezo ya awali ni kwamba mtoto katoka shule mida ya saa tisa jioni na baada ya kufika nyumbani amefanya shughuli ndogo ndogo na baada ya muda umeingia chumbani na kujifungia humo.

Dada wa kazi baada ya kuona huyu mtoto kajifungia ndani kwa muda mrefu akaanza kupiga hodi ili mtoto afungue mlango.

Amepiga hodi sana baada ya kuona kimya na tayari hapo ni jioni kama saa 11 ikabidi atafutwe fundi avunje kitasa waingie ndani.
Baada ya kuingia ndani ndipo wakamkuta mtoto amejinyonya kwa kufunga kamba kwenye dirisha.

Polisi wamekuja wameuchukua mwili wa mtoto, dada wa kazi, kaka wa marehemu na fundi aliyevunja kitasa cha mlango.
Maelezo zaidi watakuwa nayo polisi baada ya kufanya uchunguzi wao
Ni huzuni kwa kwelii kwa mtoto umri uo kujinyonga
 
Back
Top Bottom