Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa Buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa?
Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500.

Wali ule unaouzwa 2,000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage!

Nataka nihame hapa Buguruni maana tangia nimehamia hapa ni kama nimepunguza kasi ya kupambana!

View attachment 2982368
Ukihama niachie room yako,huku kwetu hali si hali.
 
Mwaka jana nimekunywa juice mbovu kabisa Serena hotel kwa shilling 10,000/= wakati mtaani kuna juice bora kabisa glasi jero tu.
Kinachofanya Serena iwe ghali siyo ubora wa vyakula per se. Hata bia kama Safari pale inaweza kuuzwa bei kubwa mara nne au zaidi ya inavyouzwa kwenye bar ya mataptap Kawe. Umenikumbusha mzee mmoja aliambiwa bei ya sahani ya wali kwenye hotel ya nyota tano akawa anasema ''si bora nikanunue gunia la mchele''.
 
Supu ya mapupu,vichwa na utumbo wa kuku,kende za ng'ombe,al kasus,mishikaki ya sh.200,misosi ya Buguruni haiaminiki
 
Huu uzi umenikumbusha ktu. Pale manzese bhakressa mida ya jion hua kuna wamama wanapanga meza zao pale nje ya soko wanauza supu jero, maandaz mia mia. Ukiwa na buku unapata supu na mandazi matano😀

Afu ukitoka pale unashuka na ile barabara direct hadi uwanja wa fisi!!
 
Hiyo ni supu ya vitoto vya ng'ombe.
Kule Vingunguti wakichinja ng'ombe wakakuta ni mjamzito hivyo vitoto ndiyo wanauziwa wamama wa Buguruni wanaowapikia hizo supu za jero jero
Usidanganye watu ungesema labda ni nyama ya wanyama wengine km punda ama mbwa lakini nyama ya vitoto vya ng'ombe inajulikana mno kwa ulaini.
 
Buguruni ile ni sayari nyingine.
Niliwahi kutoka nilipotoka na kiu yangu, nikakatiza maeneo ya Kwa Mnyamani nikasogea dukani ninunue soda ili nipooze koo.
Nikatoa buku nashangaa naulizwa "nikupimie ya bei gani?".
 
Kitu gani siyo kweli mkuu?
Nakuomba njoo hapa buguruni muda huu nikununulie vitu vyote niliyo viorodhesha hapo!
Nitakununulia supu 500, wali 500, na chips kwa mama Aisha anauza 500, na juisi ya Matunda nitakununulia 300 ushushie!
Ukishiba nakupeleka kwa wahaya ukachague mwaamke yeyote unayemtaka kwa 3000 nitalipa mimi.

Serious njoo buguruni ili uache ubishi.
Hahahaha . Elfu 5 inatosha na chenchi inabaki kumtoa ubishi jamaa

Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa Buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa? Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500.

Wali ule unaouzwa 2,000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage.

Nataka nihame hapa Buguruni maana tangia nimehamia hapa ni kama nimepunguza kasi ya kupambana.

View attachment 2982368
Nyama ya ngombe, Kuku, Mbuzi na Nguruwe zilizokufa (rejects) ndio zinaletwa Buguruni
 
Hii ni Supu ya shilingi 500 hapa Buguruni, hivi kwa hali hii unaweza ukapata akili ya kuwa na vitu vikubwa? Buguruni hii kuna mpaka Chips za 500.

Wali ule unaouzwa 2,000 maeneo mengine hapa tunauziwa 1000, kuna mpaka kipimo cha 500 kama ukiomba unapata wali na maharage.

Nataka nihame hapa Buguruni maana tangia nimehamia hapa ni kama nimepunguza kasi ya kupambana.

View attachment 2982368
Mtauziwa mizoga au nyama za mbwa
 
Back
Top Bottom