Buguruni kunalemaza sana wakuu, hebu angalia nguvu ya 500!

Ukihama niachie room yako,huku kwetu hali si hali.
 
Mwaka jana nimekunywa juice mbovu kabisa Serena hotel kwa shilling 10,000/= wakati mtaani kuna juice bora kabisa glasi jero tu.
Kinachofanya Serena iwe ghali siyo ubora wa vyakula per se. Hata bia kama Safari pale inaweza kuuzwa bei kubwa mara nne au zaidi ya inavyouzwa kwenye bar ya mataptap Kawe. Umenikumbusha mzee mmoja aliambiwa bei ya sahani ya wali kwenye hotel ya nyota tano akawa anasema ''si bora nikanunue gunia la mchele''.
 
Supu ya mapupu,vichwa na utumbo wa kuku,kende za ng'ombe,al kasus,mishikaki ya sh.200,misosi ya Buguruni haiaminiki
 
Huu uzi umenikumbusha ktu. Pale manzese bhakressa mida ya jion hua kuna wamama wanapanga meza zao pale nje ya soko wanauza supu jero, maandaz mia mia. Ukiwa na buku unapata supu na mandazi matano😀

Afu ukitoka pale unashuka na ile barabara direct hadi uwanja wa fisi!!
 
Hiyo ni supu ya vitoto vya ng'ombe.
Kule Vingunguti wakichinja ng'ombe wakakuta ni mjamzito hivyo vitoto ndiyo wanauziwa wamama wa Buguruni wanaowapikia hizo supu za jero jero
Usidanganye watu ungesema labda ni nyama ya wanyama wengine km punda ama mbwa lakini nyama ya vitoto vya ng'ombe inajulikana mno kwa ulaini.
 
Buguruni ile ni sayari nyingine.
Niliwahi kutoka nilipotoka na kiu yangu, nikakatiza maeneo ya Kwa Mnyamani nikasogea dukani ninunue soda ili nipooze koo.
Nikatoa buku nashangaa naulizwa "nikupimie ya bei gani?".
 
Hahahaha . Elfu 5 inatosha na chenchi inabaki kumtoa ubishi jamaa
Hahahaha . Elfu 5 inatosha na chenchi inabaki kumtoa ubishi jamaa
 
Nyama ya ngombe, Kuku, Mbuzi na Nguruwe zilizokufa (rejects) ndio zinaletwa Buguruni
 
Mtauziwa mizoga au nyama za mbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…