Rwanda inaongozwa na mwanajeshi na yuko paranoid, ina kundi la waasi FDRL wanaisumbua, imetoka kwenye genocide alafu ipo active kwenye conflict ya jirani yake DRC.
Inazo sababu za kuwa na wanajeshi wengi tena wenye uzoefu, na kuwa na reserve yenye uhai kijeshi.
Maofisa wa jeshi wa Rwanda wengi wameshiriki mapigano mbalimbali, Rwanda kila mwaka wanajeshi wake hufa kwenye mapigano na wakati huu mwenye hizi misheni za M23 Rwanda inadaiwa imeishapoteza wanajeshi kama elfu moja. Na hapo hutokaa uone wapi Kagame ameenda kwenye mazishi au mapokezi ya miili ya wanajeshi waliokufa, hutoona wapi nchi imeomboleza wala raia kulalamika mitandaoni. Hata jeshi la Rwanda kupoteza wanajeshi 100 kwa mwezi sio big deal wala suala la kuumiza kichwa General Staff.
Sisi walikufa wanajeshi wawili ikaonekana maajabu na tataribu nyingi zikafanyika, raia wakatoa matamko mitandaoni.