Ndo ilivyo.
Miaka 30 sasa, watu wa mashariki mwa DRC hawajui amani. Walipo leo,kesho wapo kwingine.Wanawake kubakwa,ni kugusa. Mali za watu kuibiwa, kawaida. Mwanajeshi alikuwa mtu wa kuogopa. M23 ilipolianzisha Goma,watu walijua ni yale yale. Kadri siku zinavozidi kwenda, wakaona hali ni tofauti. Watu wakaanza kukesha wanafanya biashara,wengine wakitembea, mharifu akikamatwa, wanamalizana nae. Kila walipofika,hawajawahi kumdhuru raia. Ndo wameanza kuonekana kumbe ni watu wema. Ikawa sasa imefikia hatua hiyo unayoiona, risasi zinalindima nje, watu wanajifungia ndani, wakiwaona tu, shangwe. Jiulize, nchi ipi iliwahi tokea dunia hii,kwenye vita watu wakawasindikiza wanaoitwa waasi. Kifupi, ni dalili za kwamba watu wamechoka uongozi uliyopo.