BUKAVU: M23 yakuta mlango wa mji wazi

Wakongo wanaraha sana.Yaani rais akizingua makamanda wanamzingua.Tofauti na Tanzania CCM inawakamdamiza wananchi Kwa kuwanyimwa haki za kibiashara,kisiasa,kijamii n.k lakini makamanda wametulia tu.
 
Bahima empire inatakiwa ije na east
 
Wakongo wanaraha sana.Yaani rais akizingua makamanda wanamzingua.Tofauti na Tanzania CCM inawakamdamiza wananchi Kwa kuwanyimwa haki za kibiashara,kisiasa,kijamii n.k lakini makamanda wametulia tu.
Wananenepeana tu
 
Mambo Mengine ni Morali ya Vita.

Hata wewe ungekua mwanajeshi wa Burundi, Unapata wapi morali kwenda kufia DRC? Yani unapigana kulinda nn? Watu madini au Tshichekedi?
 
Rwanda itaonekana kusaidia kupindua serikali halali iliyochaguliwa kidemokrasia kitu ambacho sio kizuri hata kidogo.
Mbona unachanganya mafaili sasa mkuu! Kwa hiyo, mataifa yote yanapozungumzia kuiwekea vikwazo Rwanda, huelewi kinachoendelea? Kwa hiyo,ukahisi haijulikani kwamba ndo kilichopo!
 
Kuna video niliwahi kuiona wananchi wanawashangilia m23 hiyo imekaaje?
Ndo ilivyo.

Miaka 30 sasa, watu wa mashariki mwa DRC hawajui amani. Walipo leo,kesho wapo kwingine.Wanawake kubakwa,ni kugusa. Mali za watu kuibiwa, kawaida. Mwanajeshi alikuwa mtu wa kuogopa. M23 ilipolianzisha Goma,watu walijua ni yale yale. Kadri siku zinavozidi kwenda, wakaona hali ni tofauti. Watu wakaanza kukesha wanafanya biashara,wengine wakitembea, mharifu akikamatwa, wanamalizana nae. Kila walipofika,hawajawahi kumdhuru raia. Ndo wameanza kuonekana kumbe ni watu wema. Ikawa sasa imefikia hatua hiyo unayoiona, risasi zinalindima nje, watu wanajifungia ndani, wakiwaona tu, shangwe. Jiulize, nchi ipi iliwahi tokea dunia hii,kwenye vita watu wakawasindikiza wanaoitwa waasi. Kifupi, ni dalili za kwamba watu wamechoka uongozi uliyopo.
 
Felix ndo Kawa Rais bogus wa Congo kuliko Rais yeyote yule
Nilikuwa na imani sana na Felix nikidhani atabadilisha DRC.

Ameishi Ubelgiji kama Mkimbizi wa Kisiasa kwa miaka mingi hadi alipokuja kugombea urais

I expected morw from him. Has proved Failure.

Ni shida ya watoto wa vigogo waliokimbia nchi. Wanaenda kama matajiri kwa hiyo hakuna walichojifunza
 
Hao watu 3000+ waliokufa ni wanajeshi tu?
 
Madaraka ya kukabidhiana kwa sababu wewe ni mwanagu au mtoto wa furani. Siku zote ndo kama hivi.
 
Hao watu 3000+ waliokufa ni wanajeshi tu?
Raia wamo,japo kidogo. idadi kubwa ya raia, ni ya wanawake walioungulia gerezani, na wengine waliopatwa na risasi. Mi nadhani usitumie jina wanajeshi. Unajua serikali inakusanya vijana(Wazalendo), na hao ndo wanawekwa front, wakiaminishwa wanaaweza. Sasa, jiulize, huyo mtu atafanya nini, mbinu za kivita hajui,japo na wanajeshi wengine, hawajawahi pigana vita, vya polini au mjini, wanaanzaje! Hao ndo wengi waliouliwa
 
Sijajua miaka yote hiyo ya Felix alishindwa vipi kuunda jeshi imara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…