Bukoba: Mwalimu wa dini ambaye pia ni Daktari wa Viongo akamatwa kwa tuhuma za kubaka watoto

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295
Jeshi la Polisi mkoani Kagera limemkamata na kumfikisha mahakamani Haruna Ayubu Rubai (63), Mwalimu wa dini ya Kiislamu na Daktari wa viungo anayemiliki kituo chake cha mazoezi ya viungo Bukoba mjini kwa tuhuma za kubaka watoto.

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 19 mwaka huu saa saba mchana katika kituo chake cha mazoezi ya viungo kilichopo Kata ya Miembeni, Tarafa ya Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, ambapo anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye pia alikuwa mwanafunzi wake wa madrasa.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoani Kagera kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

Aidha, Jeshi la Polisi limeongeza kuwa mnamo Oktoba 22, 2024 majira ya saa nane mchana, Rayana Issack aligundua kuwa watoto wake wawili wamebakwa, na mara ya kufikishwa hospitalini ilithibitika kuwa wameingiliwa sehemu zao za siri ambapo baada ya kuhojiwa walimtaja mtuhumiwa Haruna Rubai kuwa ndiye aliyewabaka.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limegundua kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kutoa msaada kwa familia zenye uhitaji kila Jumamosi, ambapo baadhi ya familia hizo huwatuma watoto wao kufuata mahitaji yao ofisini kwake, na ndipo hutumia nafasi hiyo kuwafanyia ukatili huo.

Source: Swahilitimes
 
tayari watu washa toa hukumu,huyu ni mtuhumiwa tu isije kuwa ni zengwe sisi tukakimbilia hukumu

kwa uzoefu nsha wahi sikia kesi ya hivi, mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya chadema akapewa tuhuma za kumbaka mtoto aliye jitolea kumlea

kumbe hapana, wahusika wa kumbaka yule mtoto wanafahamika kilicho mponesha mwana chadema ni...........

hii kesi ilitokea Katavi, mtaa majengo kwa wenyeji mnaweza uliza
 
Cc Faiza Foxy mtani wangu.
 
Kwa Viongozi wa Chadema hilo linajulikana ni Uongo.

Unajua kuwa Viongozi wa Chadema ni waadilifu kuliko Wachungaji na Mapadre??..

Kama ulikuwa hujui fahamu ewe Mwanadamu.
 
Back
Top Bottom