Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mitumbwi ya mbao ndo inaenda kuokoa , daah kweli hii ni Zama za kijenkitile ngwale
NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.
Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege umepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.
Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”
===============
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria
View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195
===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA
Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022
Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.
Taarifa kwa kina zinafuata
Inaonekana ni karibu na ufukweni sijui ingekua katikati huko kama tungejua.
Kweli yule jamaa sijui ni naniKuna mtu alitabiri juzi hapa kuwa ndege itaanguka tena hapa jamii forums....
Yule jamaa ni mchawi
Wewe utakua Nabii wa mchongo ndo maana unakazia andiko lako ili Hali mwezio alisema ,ajali ni ajali ila si imehusisha ndege ambayo alisema Sasa shida yako nini?Alisema Ndege itakayoanguka 'itakatika Vipande Viwili' na Ina Logo nyekundu!
Yote hayo hayajatokea Kwa Precision!
Msimpe TU Sifa za Kijinga!!
Umewahi kusafiri kwa kudandia fisi?Pamoja na yote, ndege ndiyo Usafiri salama zaidi kuliko wowote.
Mmeanza kumkumbuka????Fastjet na precisionair wanatumia ndege za mtumba. Na fastjet ndio zilikuwa kimeo kabisa. Magu alilijua hili na ndio maana kwa kutumia kodi zetu akataka atuhakikishie usalama pia kwa kununua ndege mpya.
Lengo ilikuwa usalama kwa watanzania badala ya kusubiri majanga.
Mkuu siku hizi social media zinapata habari faster kuliko hivyo vyombo vya habari,Social media ni watu wengi ambao wapo maeneo mengi tofauti tofauti,so inakua rahisi kupata habari faster.
Sio Kila ndege inapoanguka huwa ni ubovu wa ndege, Hali ya hewa pia inaweza sababisha, turbulence au makosa ya rubani pia, nadhani tusubiri taarifa kamili kutoka Kwa wahusikarest in peace magu: reason ; magu alijua akili za watanzania zilivyo, bila kuwajibishwa hawawezi kubadilika, hapo inaoenekana ndege lazima ilikua na hitilafu lakini kwa kutaka faida ikapewa kibali cha kuruka na mamlaka za kiserikali. hapo ndo nampendea uncle magu, pole angetoa, lakini lazima angetoka na vichwa vya wakurugenzi, kwa nchi za wenzetu kurusha ndege huku ina hitilafu na ikatokea maafa hio ni manslaughter kabisa.
We jamaa ulipotea sana, muda mrefu mno.Ni emergency Drill...Sio ajali ya kweli
Alaf ajari imetokea hapo hapo uwanjani , ina mana Kwa nature ya uwanja ulipo karbu na ziwa vitu kama hvyo ni vya kutegemewa , inakosaje facilities kama hzo , duniani kote 80% ya ajari za ndege hutokea inapotaka kuruka au inapotaka kutua,Vitu vya kijinga sana....wanachoweza ni kununua magari mapya...ukisema wananuna..
Ulimwengu alishasema ogopa kundi la wajinga.
kafara kweli?Mungu awaokoe waliomo. Maana ziwa kubwa kama hilo lakini hatuna mfumo mzuri wa kuokoa watu wakipatwa na majanga.
Tangu ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996 ilipotokea hakuna juhudi za maana za kuwa na mfumo wa kisasa wa uokozi kwenye ziwa hilo kubwa barani Afrika.