Mimi nachosikitika hata zile media zenye kuhudhuria press za umbea kila siku kina Mwijaku leo hakuna hata mmoja wa kuhabarisha. Picha toka asubuhi zilezile watu hawajui kinaendelea nini. kweli na hizi smartphone leo watu wanashindwa kuleta updates wanaleta siasa katika mambo ya dharura eti mpaka mamlaka husika watoe habari. Hili ni tukio liko hadharani watu wako wanasaidia sio vikao vya siri vya kamati kuu sijui ni jambo la kitaifa mnafinika mambo kutisha watu kutuma picha updates? Mamlaka itatoa taarifa kamili lakini hakuna haja ya kuwanyima haki kuona kinachoendelea. Hofu ya nini? hii ni ajali hakuna aliyelaumiwa kwanini mnafanya mambo ya ajabu. kuficha haya mambo ndio mnawapa watu kutoa taarifa sio sahihi.