Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Mimi nachosikitika hata zile media zenye kuhudhuria press za umbea kila siku kina Mwijaku leo hakuna hata mmoja wa kuhabarisha. Picha toka asubuhi zilezile watu hawajui kinaendelea nini. kweli na hizi smartphone leo watu wanashindwa kuleta updates wanaleta siasa katika mambo ya dharura eti mpaka mamlaka husika watoe habari. Hili ni tukio liko hadharani watu wako wanasaidia sio vikao vya siri vya kamati kuu sijui ni jambo la kitaifa mnafinika mambo kutisha watu kutuma picha updates? Mamlaka itatoa taarifa kamili lakini hakuna haja ya kuwanyima haki kuona kinachoendelea. Hofu ya nini? hii ni ajali hakuna aliyelaumiwa kwanini mnafanya mambo ya ajabu. kuficha haya mambo ndio mnawapa watu kutoa taarifa sio sahihi.
 
Hii ndio Tanzania tuijuayo siku zote.
ina maana hata jeshi letu la wananchi hapo Bukoba halina Helicopter hata mbili au tatu na chap kwenda pale kufanya tandemn lifting na kuipull chap hiyo ndege kwenye kina kidogo nchi kavu?.

Hapo ziwani Bukoba kabisa hakuna tag boats za kuivuta hiyo ndege?.

Ina maana hapo Bukoha mjini hakuna sling au belts za zaidi ya 20tons zikaungwa kama wananchi walivyounga hiyo kamba na Bulldozer ikavuta ikiwa nchi kavu?.

Miaka yote hapo kiwanjani pamoja na kuwa karibu na ziwa hakuna rescue yenye watu mahiri na vifaa kuokoa ziwani?.

Naamini ndege ilivyokuwa mwenye maji ndani ya ndege hakukuwa na power supply, hivyo hakukuwa na hewa, zaidi ya 1hrs ndani ya maji mkiwa kwenye ndege bila hewa... MUNGU UWANUSURU NDUGU ZETU.
 
Mili ya ma pilots ndo immetolewa Muda huu
Inaumiza ni vijana wadogo Sana ki -Umri
Wanefariki wote marubani
It pain

Khalafu tumeambiwa bado kulikuwa na mawasiliano kwenye ndege. Ni bahati mbaya sana. Criss management kwa kusema usicho na uhakika nacho ni bora kukaa kimya. Je ndege hizi nchini zinafanywia maintanance zinazozo stahili? Pole kwa wafiwa wote.
 
Mungu awaokoe waliomo. Maana ziwa kubwa kama hilo lakini hatuna mfumo mzuri wa kuokoa watu wakipatwa na majanga.

Tangu ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996 ilipotokea hakuna juhudi za maana za kuwa na mfumo wa kisasa wa uokozi kwenye ziwa hilo kubwa barani Afrika.

Inasikitisha sana R.I.P Mungu awape nguvu wafiwa. Kinacho shangaza zaidi, licha ya ajali hizi za majini na nchi kavu Taifa letu inelekea hatujifunzi kitu hata kidogo, ebu angalia vyombo vya uhokoaji vinatia simamzi kweli kweli - uwanja hupo kando kando ya Ziwa mtu ungetegemea Zima moto wangekuwa na speed boats pamoja na maboya just in case - vifaa vya kuvunja vyuma, gesi ya kuchomelea vyuma - floating cranes etc, si ajabu hakuna hata divers kama wangekuwepo wangevunja milango na madirisha pamoja na vioo vya mbele wanako kaa marubani wakavuta abiria kupitia sehemu zote hizo, sioni kama hilo lilifanyika.

Ninacho kisikia mimi baadhi ya watu bila aibu waki-suggest kwamba, eti: ndege ivutwe, hawana habari kwamba matairi yatakuwa yametitia kwenye mchanga,hivyo kuvuta ndege itakuwa ngumu labda kuinyanyua.
 
Hujajua ajari za ndege zinakuwaje. What if hii ni runway skid off ambayo imepelekea ndege kwenye tope la maji na kuzuia isiharibu airframe. Na vipi ulitaka ndege ivunjike watu wafe ndio iitwe ajari
Uchunguzi ufanyikee...sikubalii
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Miaka 5 nyuma nakumbuka natoka Dar naenda Mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya Iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
Maria akusaidieje sasa?
 
Watu 26 wameokolewa swali wameokolewa vipi? walitoka kwenye emerg exit na kama walitoka vipi mkuu wamkoa unakuja kusema bado tunawasiliana na rubani kwanini maelezo hayaingii akilini. cockpit inasehemu ya kuvunja na kutoka je kama exit imewatoa watu mnaosema wameokolewa hao wengine wako wapi? hii ni recevory ya ndege au ni rescue mbona mnatisha watu ku report hali halisi kweli hakuna hata picha za waliokolewa? siri za nini? hii ni accident sisemi muoneshe maiti lakini wale waliowazima shida iko wapi watu wapate faraja kidogo. watu wanavuta kamba askari kasimama na silaha utasema kuna vita. Aibu tena aibu sana. Hongera kwa wananchi wanawake kwa wanaume wanafanya wanachoweza.
 
Nadhani ukumbuki kilichotokea kwa MV Bukoba baada ya kuitoboa/kuikata ili kuokoa watu.
Mkuu nilitaka kuongezea hilo MV Bkb ila nikasema niache tu maana Ile meli watu walikuwa wengi sana na mizigo kupita uwezo wake kwa hiyo kuifanya izame haraka

Walipoitoboa ndio likawa kosa kubwa sana ikazama mazima na kina kiruhusu kuzama

Ila hii ndege ni tofauti kabisa haikizama na inaonekana kina ni kifupi sana kiasi cha kuiacha iwe juu
 
Huyo mkuu wa mkoa muongo sana. Chalamila ni muongo.
Kiongozi muongo hafai kuwa kiongozi ajiuzuru haraka sio kwamba ksababisha ajali hapana hana kosa lakini kwanini umasema uwongo na huyu sio mara ya kwanza wakati wa JPM huyuhuyu alisema kaongea na JPM mzima wa afya na anawasalimia. Huyu atolewe haraka sio kosa lake ajali lakini kiongozi kusema uwongo hadharani ni aibu hafai
 
Back
Top Bottom