Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria..
abiria 39 wahudumu 2 mapairot 2 jumla 43

waliookolewa 26 walio kufa 19 jumla ya idadi yoteni watu 45

swali: 45 - 43 = 02.
hawa wawili ni kina nani?
 
Hii ajali kama ni pilot error ndo imeisha hiyo maskini mana na pilot mwenyewe kafariki hakuna kesi ila kama ni shida ya ndege basi byebye precision airways...
Hopefully kuna siku tutaiona ripoti ya uchunguzi wa hii ajali kule kwa wale wadau wa aircraft investigation kama tulivyoiona ile ya KQ ilotokea miaka ile kule nchini Kameruni
 
Hivi kweli ata wangeleta bulldozer au trekta 2 wakafunga mnyororo waivute ingeshindwa kutoka?!...au ilitakiwa iwe kama ilivyokua!?
 
Hopefully kuna siku tutaiona ripoti ya uchunguzi wa hii ajali kule kwa wale wadau wa aircraft investigation kama tulivyoiona ile ya KQ ilotokea miaka ile kule nchini Kameruni
How i wish tuione
Wale wakija wenyewe ambao wametengeneza ndege lazima tutaiona tu
Nna hakika ripoti ya huko itakua tofauti na ya huku kwasababu ya siasa!
 
abiria 39 wahudumu 2 mapairot 2 jumla 43

waliookolewa 26 walio kufa 19 jumla ya idadi yoteni watu 45

swali: 45 - 43 = 02.
hawa wawili ni kina nani?
Itakuwa kuna waokoaji wamefia ndani ya ndege
 
Yaani hapo ata wangetumia V8s za RC,RAS, DC na DED ndege ingetoka tuu but ata kujaribu NO...kwakeli sometimes waweza kujiuliza hii nchi tumelogwa au ni nini...Jeshi Wana Yale matanker nayo wameshindwa kutumia...ila siku ya muungano au Uhuru utayaona kwenye maonesho uwanja wa Taifa...we are showing our weakness kwenye vitu vidogo sana..Mama Tanzania inasikitisha sana.
 
Andika mkuu kwa faida ya wengi.
Ndege huwa hazipati ajali mara kwa mara lakini huwa ikitokea ajali kupona ni nadra sana.
Na pia tanzania imejaa rushwa jambo ambalo unaweza kuta chombo kina hitilafu ila rushwa ikatumika kikaruhusiwa. Sitaki kucheza maisha yangu kamari
 
Hivi kweli ata wangeleta bulldozer au trekta 2 wakafunga mnyororo waivute ingeshindwa kutoka?!...au ilitakiwa iwe kama ilivyokua!?
Nguvu kazi waliona ndo tegeo lao.

Nafikili Uongozi mzima wa Mkoa wapaswa kuvunjiliwa mbali, airport vunjilia mbali, Waziri mwenye dhamana fika kesho hatakiwi kuwa ofisini asisubili fukuzwa, na sio mbaya waziri Mkuu akitafakari itakua busara sana
 
Inasikitisha sana. Hata vifaa vya kuokolea hatuna huku kutwa kucha ni misafari isiyo na kichwa wala miguu huku watu wako wanakufa kwa uzembe kabisa. Je ingeangukia huko ziwani katikati ingekuwaje?.. Hili taifa linahitaji mabadiliko makubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…