Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Attachments

  • 94AA7D9F-B56C-4800-BF6A-844553FE3D14.jpeg
    94AA7D9F-B56C-4800-BF6A-844553FE3D14.jpeg
    21.1 KB · Views: 3
Kikosi cha zima moto na uokoaji , kinatakiwa kutafakari katika haya hivi karibuni moto uliwaka kule mlina Kilimanjaro lakini jitihada za kuuzima moto zilikuwa siyo effective sana ikichangizwa na vifaa vilivyokuwa vikitumika, leo tena Ndege imedondoka lakini pia tumeendelea kushuhudia bado kikosi hiki hakijajipanga kisawasawa kukabiliana na matukio ya dharula katika maeneo tofauti tofauti. Serikali ione umuhimu wa kukiwezesha kikosi hiki ili kifanye wajibu wake kisheria kikamilifu... Roho za watu hazina spare...Mlima Kilimanjaro unaiingiza serikali fedha nyingii sanaaa. Basi upewe kipaumbele maalumu.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Wana wezesha jeshi la polisi kwa sababu polisi wanawasaidia kwenye mambo yao ya kisiasa, hao wengine ni dana dana tu!
 
Watu 26 wame okolewaje? , Wamepitia sehemu gani ambapo waliobaki hawawezi kupita?

Hii nchi ni aibu sana , Ina maana hatuna vitu vizito vya kuvuta hii kitu toka asubuhi saa mbili asubuhi? Crane/tinga tinga/ tunge approach kampuni za ujenzi wa Chinese waje watu saidie kuvuta.
Imenifikirisha pia😪
 
Watu 26 wame okolewaje? , Wamepitia sehemu gani ambapo waliobaki hawawezi kupita?

Hii nchi ni aibu sana , Ina maana hatuna vitu vizito vya kuvuta hii kitu toka asubuhi saa mbili asubuhi? Crane/tinga tinga/ tunge approach kampuni za ujenzi wa Chinese waje watu saidie kuvuta.

Ishakuwa bayana sasa kwamba walipita kutokea ule mlango wa dharura unakuwa karibu na mkia wa ndege...

Kama umewahi panda ndege utakuwa umewahi shuhudia huwa kuna mlango wa dharura nyuma mara nyingi ndege ikiwa inakaribia kutua au inapopaa mhudumu hukaa hapo karibu...
 
Hii imefungua macho kua:

- Maji yaliingia ndani kuanzia mbele likely impact ya kujikita kwenye tope ilitoboa mbele.

- At first waliokaa nyuma Walijiokoa wenyewe na walipotoka nje hakukua na vifaa vya kueleweka (see mtumbwi usio na engine).

- Hali ya hewa ilisababisha yote

- Je baada ya rubani kuona kashindwa kutua mara ya pili why hakupeleka ndege mwanza as promised? Je mafuta aliyokua nayo yalikua yanaweza ifikisha ndege Mwanza?

- Je Iliserereka mpaka ziwani au aliona afanye emergence landing since no way out?

Hii ni analysis ndogo based on maneno ya huyo abiria?

Poleni sana mliofikwa na mtihani
Mafuta ya reserve huenda alikuwa hana na akajua kurudi MZA hatoboi! Akaona bora aitupe majini tu
 
Mkuu wa mkoa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama anahusika moja kwa moja na huu uzembe.

Basi tu hatuna utaratibu wa kuchukuliana hatua lakini angetakiwa kujiuzuru kwa kusababisha yote haya
 
Taarifa mpya vip jmn nilikuwa offline takribani 4hr
 
Back
Top Bottom