Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Watu 19 wamethibitika kufariki dunia katika ajali ya ndege inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Precision, iliyotokea mapema hii leo mkoani Kagera.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Dar es kwenda Bukoba mkoani Kagera, na ilipata ajali hiyo ikiwa na watu 43 ndani.

Ajali hiyo imetokea katika ziwa Victoria, takribani mita 100 kabla ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
Kuna huwezekano hakuna aliyopona haiwezekani kwenye ndege kulikua na watu 43 waliookolewa 26 waliokufa 19 mbona hesabu zinagoma?
 
Ule uzi kwasasa unafwatiliwa na watu wa usalama wa timu ya tiss aviation wing na tiss terrorism protection wing kuwa makini.
Mkuu kweli tiss na watu wa avition waache kutafuta tatizo Ni nn had ndege kuanguka majini wao wako busy kumtafuta mtabiri blashit yaani .Kama. na wee upo ktk usalma unatafuta mtabiri bas hkn akili hutumiaa

Kwanza mtabiri last seen ni nov 3 had leo hi kimya yupo zake uko mashambani anapalilia mihogo yake
 
Precision air Waka matwe Kwa kutoa taarifa za uongo , watu 26 wame okolewa kupitia wpi? watu wako hapo , boat zime zingila ndege na hatuoni watu wakitolewa ndani ya ndege, ni ujinga gani kutangazia mme okoa watu 26 bila kuonyesha ni mahali walikopitia, na kudanganya eti Kuna watu wamebaki , ukweli ni kuwa hakuna kilicho okolewa.

Serikali Ina wajibika moja Kwa uzembe mkubwa, uliona wapi ndege Ina vutwa na kamba za katani au small boats kama hizo toka asubuhi? Kwakua ndege ipo sehemu ambayo haiwezi zama na hatuna vifaa vizito kama cranes/ tinga tinga za kuvuta au kunyanyua basi tutoboe kama safety procedure zitaruhusu kuokoa abiria.
Wee sie wabongo tunajibu letu pendwa kwenye mambo yote..."mipango ya mungu"
 
Mtoto wa kachwamba Amefariki pamoja na jitihada zote za Baba yake kuivuta hiyo ndege na bulldozer lakini amekuta mwanae kipenzi Ameshafariki.

Nimeumia Sana
Kachwamba Ni Nani mkuu embu wake code was kidg

Ila all in all poleni familia yake na taifa kwa ujumla kwa msiba huu mkubwa kuwai kutokea kwenye maswla ya aviation
 
Kuna huwezekano hakuna aliyopona haiwezekani kwenye ndege kulikua na watu 43 waliookolewa 26 waliokufa 19 mbona hesabu zinagoma?

Taarifa ya ndege kuwa na abiria 43 inasemekana ni sahihi pia idadi ya waliookolewa kuwa 26 wanasema nayo ni sahihi...

Idadi ya wafu 19, wanahisi huenda kuna waokozi 2 waliojitolea wamefariki wakati wakizamia majini kuokoa abiria...
 
nimemsikiliza mama mmja nazani ni kiongozi anadai haikua ajali bali lilikua zoezi la kutekeleza uokoaji, akiwa na maana ilikua planned accedent ili kujipima na uokozi katika majanga dizain hiyo[emoji849].. nimesikitika sana
Hiyo video unayosema ni ya muda mrefu Sana mkuu, mpaka muda huu Bado unaendelea kupotezwa na miruzi mingi tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni Ajali- Disaster.. zoezi la Testing.. Full Testing ni nadra kulifanya... huwezi ku involve Passengers... most of ISO zina care Human safety... kuliko kitu chochote.. yale mazoezi ya moto ni tofauti na hii ajali...
Wangeweza kufanya
1. Walk through testing...
2. Preparedness testing...
Sio hii....
@Mlolongo alitaka kunitoa kwenye reli eti kuwa Ni ajali zoezi

Jamaa sijui ametoa wapi hyo elimu ya namna hyo ya kupima utayari kwa kuzamisha ndege kwenye ziwa Victoria Tena ndege binafis ikiwa na watu mle ndani bladfakeni
Mlolongo
 
Huyo Kachwamba nimemsikia mzee anamsema miaka kama 15 imepita. Kuna jambo alifanya kwenye mamlaka yake
Kachwamba mkubwa (Abubakar Kachwamba) ndio zile figure za akina Makamba, Mzindakaya, nk.
Huwa nashangaa wahaya wanailaumu serikali kuwatelekeza huku hawawasemi akina Muhazi, Kachwamba, nk amabo walifuja Mali za walalaho na kujineemesha hadi wajukuu zao hawawasemi ....kwasababu ya msiba mkubwa wa kizembe ngoja niishie hapa ila Kuna siku nitaweka Uzi hapa wa wahuni wote wa Kagera waliojificha kwenye koti la CCM!
 
Precision air Waka matwe Kwa kutoa taarifa za uongo , watu 26 wame okolewa kupitia wpi? watu wako hapo , boat zime zingila ndege na hatuoni watu wakitolewa ndani ya ndege, ni ujinga gani kutangazia mme okoa watu 26 bila kuonyesha ni mahali walikopitia, na kudanganya eti Kuna watu wamebaki , ukweli ni kuwa hakuna kilicho okolewa.

Serikali Ina wajibika moja Kwa uzembe mkubwa, uliona wapi ndege Ina vutwa na kamba za katani au small boats kama hizo toka asubuhi? Kwakua ndege ipo sehemu ambayo haiwezi zama na hatuna vifaa vizito kama cranes/ tinga tinga za kuvuta au kunyanyua basi tutoboe kama safety procedure zitaruhusu kuokoa abiria.
PW hupata taarifa toka kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama
 
Huyo aliyepewa ubunge wa EA na kumuacha @paschalmayalla.
Familia ya Mzee Kachwamba ukoo wa panya walikula KCU hadi kubaki mifupa na bado wanae na wajukuu wanazawadiwa vyeo huko CCM...smahani wakuu nimekuwa too emotional na kusahau "msiba"
Dah haya pole kwa familia ila tusiwe too much emotional kwenye hili embu uchunguzi ufamyikee mnk hz za serekali sijui Hali zake ziko vip
 
Jana niliona kwenye taarifa ya habari kamanda wa Polisi akipokea "kitendea kazi" kwa ajili ya kufanya doria kwenye barabara kuu ya mkoa wa Pwani ili kuzuia ajali za barabarani, unajua ni kifaa gani alikuwa anazindua tena kwa kukata utepe ....GARI AINA YA TOYOTA PROBOX mtumba hadi taa zimeishafifia uke ungavu wake. Wanachi kuvuta ndege kwa kamba kama kokolo la sangara haishangazi sana. Tunakopa kununua V8. Pumbavu sana!
Dah ile ya jana polisi nilishangaa sana
 
Back
Top Bottom