Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Niwakumbushe Rais na Makamu wake wako nje ya nchi wakitafuta misada ili wajanja waje waile! Nchi ya mazombi hii twendeni tu!
Ushawahi kujiuliza uwanja uko karibu na ziwa lakini hakuna vifaa vya ukoaji! Our leader they do not think out of the box!
Makamu yuko Tanzania
Rais yuko Tanzania
 
Inamaana kwa taarifa hii Rubani hajajumuisha katika watu waliopoteza maisha? Lakini mkuu wa mkoa Chalamila alikuwa naongea watu 26 kuokolewa mbona namba imeanza kuleta mkanganyiko!
Ndege ilikuwa na jumla ya watu 43
waliookolewa 26
waliofariki 19
Hapo kuna walakini ngoja tuvumuilie tutapata taarifa zote kwa usahihi! Polen sana nyote!
Wanadai huenda waokoaji nao wamekufa
 
Kachwamba mkubwa (Abubakar Kachwamba) ndio zile figure za akina Makamba, Mzindakaya, nk.
Huwa nashangaa wahaya wanailaumu serikali kuwatelekeza huku hawawasemi akina Muhazi, Kachwamba, nk amabo walifuja Mali za walalaho na kujineemesha hadi wajukuu zao hawawasemi ....kwasababu ya msiba mkubwa wa kizembe ngoja niishie hapa ila Kuna siku nitaweka Uzi hapa wa wahuni wote wa Kagera waliojificha kwenye koti la CCM!

Huo uzi ukiuweka usisahau kunitagi
 
watu wamekufa wangapi,
poleni wafiwa, ajali haina kinga.
ajali hakuna aliye tarajia, Mungu azioumzishe roho za mrehemu.
 
Kufa tutakufa tena wote lakini tunakufaje ndo hoja ya msingi! Ifike mahali tutumie akili zetu na rasilimali zetu kujiweka tayari dhidi ya majanga kama haya. Emergency preparedness against disaster risks! ni muhimu sana na ndiyo maana Sendai Framework (2015-2030) imewekwa kuelekeza nini kifanyike.
Ni ajabu ndege inaanguka saa 2 asbh hadi jioni eti bado uokoaji unaendelea! Sitaki kuamini kuwa imetokea hivi kwa sababu ni Precision ingekuwa ATCL ingekuwa tofauti HAPANA! Tatizo letu sisi tumebakia kutukuza wanasiasa na viongozi hasa tukiwaona wakiwa kwenye magari na majengo ya kifahari.
Tanzania tumejisahau kiasi kwamba tunawaimarisha viongozi na chama tawala badala ya kuimarisha mifumo ya kulinda usalama wa wananchi!
Kitengo Cha majanga na maafa kipo ofisi ya waziri Mkuu uliza sasa mafungu yanayotengwa yanaishia wapi badala ya kuimarisha emergency preparedness?? Au ndo wajanja wachache wanatumia kuishi kifahari??

Ni hivi, tunapo furaie kuwa na viwanja, ndege, madaraja, magorofa, treni za umeme, pantoni, meli n.k tusisahau aspect ya emergency preparedness!! Tulazimishe Mifumo yetu iimarishiwe uwezo na rasilimali ili isiwe mizito sana katika kutenda kwa haraka na usahihi wakati wa ajali na dharura!
Dharura, ajali na majanga yapo na hayatokaa yaiishe. Hivyo inabidi tujiandae kwa elimu, vitendea kazi na bajeti (rejea Sendai Frame 2015-2030)!
Hii ya Precision haikupaswa kuwa hivi! Aki kusuasua kwa uokoaji kwenye ajali ya leo haina utofauti na kilichotokea kwenye ajali ya MV Bukoba 1996. Miaka 26 baadae, tumejifunza nini? Tumeboresha nini?
Nataka niamini kuwa hii ya leo imetufundisha kitu na sasa tutajiandaa dhidi ya majanga mbalimbali 😢😢😢

(MUNGU awarehemu marehemu. Awasidie wahanga wa tukio na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wote!)
 
Kufa tutakufa tena wote lakini tunakufaje ndo hoja ya msingi! Ifike mahali tutumie akili zetu na rasilimali zetu kujiweka tayari dhidi ya majanga kama haya. Emergency preparedness against disaster risks! ni muhimu sana na ndiyo maana Sendai Framework (2015-2030) imewekwa kuelekea nini kifanyike.
Ni ajabu ndege inaanguka saa 8 asbh hadi jioni eti bado uokoaji unaendelea! Sitaki kuamini kuwa imetokea hivi kwa sababu ni Precision ingekuwa ATCL ingekuwa tofauti HAPANA! Tatizo letu sisi tumebakia kutukuza wanasiasa na viongozi hasa tukiwaona wakiwa kwenye magari na majengo ya kifahari.
Tanzania tumejisahau kiasi kwamba tunawaimarisha viongozi na chama tawala badala ya kuimarisha mifumo ya kulinda usalama wa wananchi!
Kitengo Cha majanga na maafa kipo ofisi ya waziri Mkuu uliza sasa mafungu yanayotengwa yanaishia wapi badala ya kuimarisha emergency preparedness?? Au ndo wajanja wachache wanatumia kuishi kifahari??

Ni hivi, tunapo furaie kuwa na viwanja, ndege, madaraja, magorofa, treni za umeme, pantoni, meli n.k tusisahau aspect ya emergency preparedness!! Tulazimishe Mifumo yetu iimarishiwe uwezo na rasilimali ili isiwe mizito sana katika kutenda kwa haraka na usahihi wakati wa ajali na dharura!
Dharura, ajali na majanga yapo na hayatokaa yaiishe. Hivyo inabidi tujiandae kwa elimu, vitendea kazi na bajeti (rejea Sendai Frame 2015-2030)!
Hii ya Precision haikupaswa kuwa hivi! Aki kusuasua kwa uokoaji kwenye ajali ya leo haina utofauti na kilichotokea kwenye ajali ya MV Bukoba 1996. Miaka 26 baadae, tumejifunza nini? Tumeboresha nini?
Nataka niamini kuwa hii ya leo imetufundisha kitu na sasa tutajiandaa dhidi ya majanga mbalimbali [emoji22][emoji22][emoji22]

(MUNGU awarehemu marehemu. Awasidie wahanga wa tukio na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wote!)
Babu ungeandika kwa kifupi sna
 
Back
Top Bottom