Kufa tutakufa tena wote lakini tunakufaje ndo hoja ya msingi! Ifike mahali tutumie akili zetu na rasilimali zetu kujiweka tayari dhidi ya majanga kama haya. Emergency preparedness against disaster risks! ni muhimu sana na ndiyo maana Sendai Framework (2015-2030) imewekwa kuelekea nini kifanyike.
Ni ajabu ndege inaanguka saa 8 asbh hadi jioni eti bado uokoaji unaendelea! Sitaki kuamini kuwa imetokea hivi kwa sababu ni Precision ingekuwa ATCL ingekuwa tofauti HAPANA! Tatizo letu sisi tumebakia kutukuza wanasiasa na viongozi hasa tukiwaona wakiwa kwenye magari na majengo ya kifahari.
Tanzania tumejisahau kiasi kwamba tunawaimarisha viongozi na chama tawala badala ya kuimarisha mifumo ya kulinda usalama wa wananchi!
Kitengo Cha majanga na maafa kipo ofisi ya waziri Mkuu uliza sasa mafungu yanayotengwa yanaishia wapi badala ya kuimarisha emergency preparedness?? Au ndo wajanja wachache wanatumia kuishi kifahari??
Ni hivi, tunapo furaie kuwa na viwanja, ndege, madaraja, magorofa, treni za umeme, pantoni, meli n.k tusisahau aspect ya emergency preparedness!! Tulazimishe Mifumo yetu iimarishiwe uwezo na rasilimali ili isiwe mizito sana katika kutenda kwa haraka na usahihi wakati wa ajali na dharura!
Dharura, ajali na majanga yapo na hayatokaa yaiishe. Hivyo inabidi tujiandae kwa elimu, vitendea kazi na bajeti (rejea Sendai Frame 2015-2030)!
Hii ya Precision haikupaswa kuwa hivi! Aki kusuasua kwa uokoaji kwenye ajali ya leo haina utofauti na kilichotokea kwenye ajali ya MV Bukoba 1996. Miaka 26 baadae, tumejifunza nini? Tumeboresha nini?
Nataka niamini kuwa hii ya leo imetufundisha kitu na sasa tutajiandaa dhidi ya majanga mbalimbali [emoji22][emoji22][emoji22]
(MUNGU awarehemu marehemu. Awasidie wahanga wa tukio na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wote!)