Bukoba: Rais Samia afungua Msikiti wa Jami'ul Istiqaama, Juni 10, 2022

Bukoba: Rais Samia afungua Msikiti wa Jami'ul Istiqaama, Juni 10, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais Samia akifungua Msikiti wa Jami'ul Istiqaama, Bukoba Mkoani Kagera, leo Ijumaa Juni 10, 2022

FU4DLGhWYAIxhZk.jpg

Shukrani za kipekee kupitia kwako Muwakilishi wa Balozi wa Oman, ziende kwa Sultan wa Oman na vilevile kwa niaba ya mtangulizi wake ambaye ndiye muasisi wa ujenzi wa Msikiti huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amin!

Wa ujumla niishukuru Serikali ya Oman si tu kwa msaada iliyoutoa katika Msikiti huu wa kifahari, lakini pia kwa ushirikiano wao mkubwa kwa Serikali ya Tanzania. Uhusiano wan chi zetu mbili ni wa muda mrefu, na wa kihistoria na wa kindugu pia.

Ni wajibu wetu sote kuuendeleza na kuudumisha kwa manufaa ya nchi zetu mbili ndiyo maana nimekubali mwaliko wa Mfalme wa Oman wa kuitembelea Oman siku chache zijazo.

Niwashukuru kwa kazi nzuri ya kujenga jamii ya Wacha Mungu wenye kutii mamlaka na Sheria zake kwa hofu ya Mwenyezi Mungu.

Hongereni na ahsanteni sana kwa kushirikiana kwa karibu na Serikali… ninaamini fika tukiendelea kuzienzi tunu zetu hizi, basi bila shaka amani katika nchi yetu itaendelea kudumu. Tukumbuke kuwa neema hii ya amani tuliyokuwa nayo, inatamaniwa na nchi nyingi duniani - hivyo tuilinde kwa juhudi zetu zote. Kama ni dua kama ni sala, tulinde amani yetu.

Katika nafasi yangu kama Rais wa Tanzania nimefanya kazi na viongozi wa Istiqama na kushirikiana nao kwa karibu.

Ni jambo la faraja kuwa Jumuiya ya Istiqaama imepata viongozi ambao wana nia na moyo thabiti kuhakikisha kuwa Jumuiya inapiga hatua. Mimi nishahidi najua miradi yao mingi.

Nimepata fursa ya kuutembelea ni Msikiti mzuri sana. Hii inaleta hamasa kwa taasisi nyi gine kujenga nyumba za ibada yenye hadhi ya kiwango kizuri.

Ni imani yangu kuwa waumini wa Mji wa Bukoba watajitokeza kwa wingi kutekeleza ibada zao katika Msikiti huu.

Msikiti huu pia umeambatana na Madrassa itakayotumika kutoa elimu sahihi ya Dini. Na nimepandishwa mpaka Madrassa na nimeiona ni ya kisasa. Na sidhani kama watoto watakataa kusoma hapa kwa mambo mazuri yaliyomo kule ndani.

Ni matarajio ya waliojenga Msikiti huu, ambao hata mimi ninaungana nao, kuwa Waumini wa Bukoba wataitumia Madrassa hii kuwasomesha watoto wao masuala ya kiimani na maisha kwa ujumla.

Tunaomba hivyo ili tujenge jamii yenye maadili mema. Tukumbuke kuwapatia watoto wetu mafundisho ya dini ni wajibu wetu adhima ambao sisi wazazi tunao kwa Mwenyezi Mungu. Na hii ni kwa dini zote.

Na nimeona Msikiti huu una Maduka, nimeambiwa una maduka saba (7). Mifarakano huja kwenye kutaka madaraka kwenye kusimamia na kuendesha Msikiti huu hasa kunapokuwa na vibiashara vinavyoleta riziki kwenye Msikiti huu.

Sasa, madhumuni ya kuweka maduka haya ni yatoe sadaka ndogo ya kuendeleza Msikiti huu. Mabomba yanapoharibika basi sadaka ile ikatengeneze mabomba ya maji. Rangi inapochakaa, pesa ile ikapake rangi.

Nimeongea na viongozi wa Istiqama wamesema wana namna nzuri ya kuendesha Misikiti yao na kama alivyosema Mufti hajawahi kusikia mifarakano katika Misikiti ya Istiqaama. Naomba wengine wanaojenga misikiti wafuate utaratibu huo.

Si matumaini yetu kusikia mifarakano kwenye nyumba za ibada na kumwabudu Mungu.

Kufanya shughuli zenu kwa uadilifu na kwa kufuata misingi ya Haki na Sheria, kwa hakika mafanikio yenu, hususan kwa kuwa na matawi 21 yanayofanya kazi za kiimani na kijamii na kujenga roho rahimu kwa Watanzania, mafanikio hayo ni ya kujivunia nay a kuigwa na taasisi nyingine.

Kama mnavyofahamu, Dunia ikiwemo Tanzania, tuna maradhi ingawa tumepewa tahfifu. Pamoja na tahfifu, tusijidanganye maradhi haya hayapo. Hatujui kinachokuja, kama maradhi hay ani kudra za Mwenyezi Mungu au kuna watu wanayatengeneza – hatuyajui.

Niwaombe sana Watanzania waende wakapate chanjo kuepukana na maradhi haya thakili.

Twende tukahimize Sensa. Lengo ni kujuana ili Serikali iweze kupanga mipango yake vizuri. Hata Mtume wetu pia alifanya Sensa kabla hajaenda vitani.

Ni vyema kuwahimiza Wanachi kuhusu umuhimu wa Senza ili tujuane, nani yupo wapi, anafanya nini na anaishi vipi.
 
Rais Samia akifungua Msikiti wa Jami'ul Istiqaama, Bukoba Mkoani Kagera, leo Ijumaa Juni 10, 2022


Sasa kama wizara ya fedha inatenga trillion 13.9 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na trillion 1 kwa matumizi ya maendeleo unatengemea rais atazindua nini km sio misikiti na sheli
 
Acheni upumbavu kuhoji vitu vidogovidogo. Kwani akifungua kuna shida gani. Wala yeye si wakwanza kuhusika katika hafla za kidini. Ni rais wa nchi, kila mtu na kila taasisi ina haki ya kumtumia.
Ww ndio mpuuzi kabisa anawezaje kufanya ziara zisizo kuwa productive kwa wananchi.... wananchi wanufaikaje na huo msikiti kutatua changamoto zao?
 
Acheni upumbavu kuhoji vitu vidogovidogo. Kwani akifungua kuna shida gani. Wala yeye si wakwanza kuhusika katika hafla za kidini. Ni rais wa nchi, kila mtu na kila taasisi ina haki ya kumtumia.
Sidhani kama kuna aliyeweka bayana kubeza.Mf mimi nimeuliza nijuwe.
 
Acheni upumbavu kuhoji vitu vidogovidogo. Kwani akifungua kuna shida gani. Wala yeye si wakwanza kuhusika katika hafla za kidini. Ni rais wa nchi, kila mtu na kila taasisi ina haki ya kumtumia.
Hebu mchukue na wewe umtumie tuone.
 
Back
Top Bottom