KERO Bunda: Hali ya Barabara inayokwenda TBC - Mnara wa Vodacom si nzuri, inahitaji matengenezo ya haraka sana

KERO Bunda: Hali ya Barabara inayokwenda TBC - Mnara wa Vodacom si nzuri, inahitaji matengenezo ya haraka sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Barabara ya ‘Mnara wa Vodacom’ inayochepuka kutoka barabara mpya iendayo Butiama-Nyamuswa-Ukerewe imekuwa kero kwa wakazi wa Ligamba mtaa wa Ligamba ‘A’—Wilaya ya Bunda, Mara.

Barabara hii, licha ya kuelekea kwenye minara ya Vodacom na ofisi za TBC pamoja na minara ya TBC, haijawahi kufanyiwa marekebisho tangu kipindi cha uchimbaji moramu uliokuwa unaendelea mtaa huo wakati wa ujenzi wa barabara kuu ya lami ya Ukerewe-Butiama.

Katika barabara hii, Vodacom wamepitisha nyaya za Fibre kuelekea kwenye mtandao wao na kusababisha mmonyoko wa ardhi huku nyaya zikibaki nje baada ya mvua za miezi hii.

Mnamo nusu ya kwanza ya mwaka huu, kwenye ufunguzi wa minara ya TBC Mkoani Mara, Waziri wa Ujenzi akiwa mgeni rasmi alitoa ahadi ya kujenga barabara hiyo lakini hadi sasa haijawahi hata kufanyiwa ukarabati.

Licha ya mashirika makubwa kutumia barabara hiyo, bado hali yake si nzuri huku madaraja na barabara vikiharibika vibaya kwa kukosa miundombinu kama mitaro.

Nitoe wito kwa serikali kuliangalia hilo na kushughulikia barabara hiyo inayotumiwa na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaoelekea Bunda mjini kwa ajili ya biashara zao za mazao na mifugo. Lakini pia shule ya Msingi Kilimahewa iliyopo katika njia hiyo.
IMG_1818.jpeg
IMG_1771.jpeg
IMG_1769.jpeg
IMG_1767.jpeg
IMG_1768.jpeg
IMG_1765.jpeg
IMG_1766.jpeg
IMG_1764.jpeg
IMG_1763.jpeg
IMG_1761.jpeg
IMG_1759.jpeg
IMG_1760.jpeg
IMG_1754.jpeg
IMG_1752.jpeg
 
Nyumbani kwa mwalimu Nyerere huku kweli Nyerere atendewi haki jamani
 
Back
Top Bottom