Kwa jinsi alivyofungwa fungwa inaonekana alitupwa akiwa mzima mzima kama anavyoonekana hapo na kutoswa mtoni.
Eeh Mungu Baba ,Mwenye kila uweza na nguvu, Naomba ukakomeshe haya mauaji yanayofanyika dhidi ya watu mbali mbali, Nakemea pepo LA mauaji lililowaingia wahalifu hao. Naomba Mungu ukawabadilishe Roho za wauaji hawa wakawe na Roho iliyojaa Amani,upendo na unyenyekevu kwa wenzao ili Tanzania irudi katika hali Yake ya kuwa Mahali salama pa kuishi kwa kila RAIA.
Ee Mungu Baba mwenye enzi, naiombea na hii familia ya marehemu iliyoachwa katika taharuki na ukiwa, Ukawape nguvu na ujasiri wa moyo katika kipindi hili walichonacho cha huzuni kuu katika familia yao. Ukaiwezeshe familia hii istahimili msiba huu mzito kwao.
Naomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo anayeishi na kutawala daima na milele
Amina.
Raha ya milele umpe ee Bwana
Na mwanga wa milele umwangazie
Apumzike kwa Amani.
Amina.
Hivi ni kweli Polisi wamezidiwa maarifa na hawa wauaji?
Tulipofikia sasa, yamfaa Rais aingilie kati mauaji haya yanayoendelea kwa kufanyia mabadiliko ya kiutawala hii Wizara ili waje wengine wenye mbinu mpya kuwadhibiti hawa wahalifu.
Haya mauaji yanayoendelea sasa mwisho wake ni UPI?