Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Huo mwili baada ya wiki mbili wameutambua? Na mbona staili ni zile zile za watu walio kua wanafugwa kweny visandarus kweny Bahar ya hindi? Na huo MTO ndibaga usikute tuna share na mataifa mbalimbali ..ukute sio mwil Samson ni wa watu wa mataifa mengne kama ilivyokua bahari ya Hindi
 
Ninavyoona watu wanapoteza imani na polis na hali ikiendelea hivi wengi zaidi watapoteza imani hata na wanaoshabikia kwa sasa. Kitu cha kufanya ni kufumua mfumo wa uongozi. Wizara hii iwekwe chini ya rais km ilivyo Tamisemi. Waziri na IGP, sijui km wanajua majukumu yao kwani naona wamejaa ushabiki kuliko weledi
 
Maskini,naimagine jinsi alivyoteseka kuchinjwa bila nganzi,Binadamu ni zaidi ya mnyama.Babu yangu aliniambia zamani ukiona Binadamu unapata moyo,siku hizi ni bora ukutane na Simba kuliko Binadamu mwenzako.
IMG_20180315_073443_510.jpg

Mwili wake ndio huu hapa
 
Kuna watu walipatikana katika mtindo huo huo tukaambiwa ni wahamiaji haramu!
sasa huyu ana jina tusubiri kuambiwa kama kajiua iki kuketa taharuki au wauaji wa ndanu wamekopi mtindo wa disposal wa wale wanaowatelekeza wahamiaji haramu waluokufa ili kuketa taharuki,ama wasiojulikana kwa ujumla wake wanaendeleza wimbi la mauaji?
Na sijui katika pelelezi zao wamepata kugundua kama kesi zote zinawatendaji wa aina moja au ni isolated na hapo tuanze mbali ,mauaji ya Mawazo yule wa morogoro ,mvungi nk na kwenye utekaji
Kibanda ,roma,nondo ,masheikh nk.
Na waliopotea kote iangaliwe kama wahusika wanahusiana.
Mungu anazidi kuumbua mipango ya waovu na ile ya Jeshi la Polisi. Juzi wame tofautiana kauli. Leo hii nani atakua na imani na upelelezi utakaofanywa na jeshi la Polisi?
 
huyu aliyeanzisha style ya kuua watu kwa kuwaweka kwa viroba...Mungu amlaani
Kila jambo lina mwisho,na damu ya mtu siku zote hurudi mauaji haya ya kinyama mwenyekiti wa kijani hajawahi kuongea au kukaripia wanaofanya
 
Daaa.., siku zote hizo ndo aonekane Leo Mtoni au walimshikilia kwa Muda kabla ya kuamua kumtoa uhai? Na je lilikotelekezwa gari lake na huko alikopatikana ni maeneo ya karibu ama maeneo mawili tofauti?
Maswali ni mengi sana kuliko majibu, apumzike panapostahili...,
Lamadi sio mbali na geti la Serengeti. Maeneo hayo hayo. Unaweza kukuta huo mto umetokea Serengeti na Marehemu alitoswa mtoni huko Sererngeti.
 
Back
Top Bottom