Bunda: Paroko Karoli Mganga mbaroni akidaiwa kughushi na kujipatia Tsh. Milioni 800

Bunda: Paroko Karoli Mganga mbaroni akidaiwa kughushi na kujipatia Tsh. Milioni 800

Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda mkoani Mara, Karoli Mganga anatuhumiwa kughushi nyaraka na kujipatia zaidi ya Sh800 milioni kinyume cha sheria.

Paroko huyo anatuhumiwa kuhusika kwenye tukio hilo pamoja na mhasibu wa parokia hiyo, Gerald Mgendagenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase alisema kutokana na tuhuma hizo, jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wote wa wawili na kufanya uchunguzi kwa ajili ya hatua nyingine zaidi.

Alisema tayari jeshi hilo limekamilisha uchunguzi na jalada limepelekwa Ofisi ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda alisema paroko huyo na mhasibu wake wanadaiwa kugushi nyaraka kwa nyakati tofauti na kujiapatia kiasi hicho cha fedha, mali ya parokia hiyo, kinyume cha sheria na taratibu.

Alisema mbali na kughushi nyaraka, watuhumiwa hao pia wanadaiwa kughushi sahihi za watu mbalimbali, hali iliyowawezesha kufanikisha malengo yao na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

“Sisi tumekamilisha upelelezi wetu tangu wiki iliyopita na jalada tumelipeleka kwa mwendesha mashtaka wa Serikali, hivyo tunasubiri hati ya mashtaka kwa ajili ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria," alisema.

Alisema watuhumiwa hao wako nje kwa dhamana wakisubiri kukamilika kwa mchakato wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali.

Credit - Mwananchi
Mgendagenda yaani mpitanjia au mtembezi.
 
Nijuavyo mimi, Paroko ndiye mdhamini wa mali zote za Parokia. Hata akitaka kutumia hovyo mamlaka aliyopewa kwa kuaminiwa, anaweza kufanya bila shida yoyote. Sijajua hilo limekaaje
Padre hana Mamlaka hayo aisee...ila kwa kushirikiana na watu aliowaweka inawezekana.
 
mapadre wanavuta sigara, wanakunywa wine na wananunua malaya....uliza kwa waliosoma seminary wanajua hizi mambo
 
Hiv ni mimi ambae sijui au na niny wenzangu.

Hivi kwenye hii kesi wa kulalamika ni Kanisa katoliki au parokia? Naonaga pia watu wanasema TAKUKURU waende mara simba mara Yanga, ila hizo si pvt bodies? So why TAKUKURU?
Takukuru inahusika na makosa yoteyawe private au public yanayohusu ufisadi na rushwa hata wewe ukifanya ufisadi kwenye kampuni ya familia yenu takukuru inahusika.

Na kwa kuongezea unappfanya jinai kwenye mipaka ya tanzania hata kwa ndugu yako inayokushitaki ni jamhuri siyo ndugu yako, ndug yako atakuwa shahidi tu.
 
Kwa sheria za kanisa katoliki hapo labda askofu wa jimbo ndo amshitaki. Paroko wa parokia ana mamlaka kamili na vitu vyote vilivyopo kwenye parokia. Pona ya wanaparokia labda iwe walifoji nyaraka za kutoa fedha.
 
Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda mkoani Mara, Karoli Mganga anatuhumiwa kughushi nyaraka na kujipatia zaidi ya Sh800 milioni kinyume cha sheria.

Paroko huyo anatuhumiwa kuhusika kwenye tukio hilo pamoja na mhasibu wa parokia hiyo, Gerald Mgendagenda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase alisema kutokana na tuhuma hizo, jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wote wa wawili na kufanya uchunguzi kwa ajili ya hatua nyingine zaidi.

Alisema tayari jeshi hilo limekamilisha uchunguzi na jalada limepelekwa Ofisi ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda alisema paroko huyo na mhasibu wake wanadaiwa kugushi nyaraka kwa nyakati tofauti na kujiapatia kiasi hicho cha fedha, mali ya parokia hiyo, kinyume cha sheria na taratibu.

Alisema mbali na kughushi nyaraka, watuhumiwa hao pia wanadaiwa kughushi sahihi za watu mbalimbali, hali iliyowawezesha kufanikisha malengo yao na kujipatia kiasi hicho cha fedha.

“Sisi tumekamilisha upelelezi wetu tangu wiki iliyopita na jalada tumelipeleka kwa mwendesha mashtaka wa Serikali, hivyo tunasubiri hati ya mashtaka kwa ajili ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria," alisema.

Alisema watuhumiwa hao wako nje kwa dhamana wakisubiri kukamilika kwa mchakato wa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Serikali.

Credit - Mwananchi
=========================​
Alleged Forgery Scandal Involving Catholic Parish Priest and Accountant in Bunda, Mara Region

In a surprising turn of events, the Parish Priest of the Catholic Church in Bunda, located in the Mara Region, Father Karoli Mganga, is facing accusations of document forgery and unlawfully obtaining over Sh800 million. The scandal involves the parish accountant, Gerald Mgendagenda.

Mara Regional Police Commander, Salim Morcase, addressed the media yesterday, revealing that both the priest and the accountant were arrested for investigation following the allegations. The police have completed their inquiry, and the case file has been forwarded to the Prosecutor's Office for further action.

According to Commander Morcase, the duo is accused of forging documents on various occasions to misappropriate the substantial sum of money, which belongs to the parish, contrary to the law and established procedures. In addition to document forgery, the suspects are also alleged to have falsified signatures of various individuals, enabling them to achieve their objectives and accumulate the mentioned funds.

"We concluded our investigation last week, and we have submitted the case file to the government prosecutor. We are now awaiting the issuance of charges for the suspects to be taken to court in accordance with the law," stated Commander Morcase.

While the accused individuals are currently out on bail, they await the completion of the legal process by the government prosecutor's office. The unfolding scandal has raised concerns within the local community and the Catholic Church, prompting authorities to take swift action against the accused priest and accountant.
Dili halichagui we ni nani,sema tu limebuma 😀😀
 
Kwa sheria za kanisa katoliki hapo labda askofu wa jimbo ndo amshitaki. Paroko wa parokia ana mamlaka kamili na vitu vyote vilivyopo kwenye parokia. Pona ya wanaparokia labda iwe walifoji nyaraka za kutoa fedha.
Mzee jinai siyo swala binafsi kama aliiba ni swala la serikali
 
Mzee jinai siyo swala binafsi kama aliiba ni swala la serikali
Nyaraka za uanzishwaji wa parokia zinaweza zikawa hazisapoti ukisemacho. Kwa sababu wakati wa kuanzisha akaunti huwa zinapelekwa nyaraka. Zile ndo zitaamua ni kosa au sio kosa. Ndo maana unaona askofu anafanya utumbo then vatican ina mrecall anaachishwa utume basi na kama ni kushtakiwa anashtakiwa kwenye mahakama za ndani ya kanisa. Kwenye katiba ya kanisa katoliki paroko mahalia ana mamlaka ya hadi kumkatalia msaidizi wake kwenda sehemu na namna ya kutumia fedha za parokia. Anayeweza kumoverule ni askofu wake peke yake. Je akithibithisha hajaiba bali amechukua hela zilizo chini ya mamlaka yake akatumia? Na vithibitisho akakutolea kuthibitisha yeye kama paroko ana mamlaka na fedha za parokia? Mtasemaje?
 
Ndio maana takukuru wanaingia kuchunguza wakithibitisha kuna jinai atafikishwa mahakama za kawaida
 
Hayo mambo hua yanazuka parokiani Ila mengi humalizwa chini kwa chini kupitia usuluhishi wa kanisa hua hayafiki mahakamani ni nadra sana sio kwamba hayapo, hili nimeshangaa limefukaje huko mahakamani wakati hua wanayamaliza humo humo kanisani na paroko anahamishwa kwenda parokia nyingine hata km katafuna Billion, adhabu yake nahisi labda hua ni kushushwa Cheo tu na kua padre wa kawaida lakini kesi nyingi za hivi hazipelekwi mahakamani zinamalizwa kanisani huko huko kuepuka kulichafua kanisa kwamba linaongozwa na maparoko matapeli
huo mkwanja ni mrefu sana aseee! hiyo ni hela ya miradi midogo midogo kwenye level ya halmashauri !! hapo TAKUKURU lazima chupi ziwacheze
 
Mdau anasema makanisa ya pesa ila msikitini hata hela ya umeme ni ugomvi. Ni kweli?
Muulize aliesema, mimi msikiti wa jirani yetu hawakuwahi kuwa na tatizo la umene na hawachangishi pesa za umeme.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom