Bunge: Bodi ya Mikopo inahitaji Tsh. Bilioni 800 kukopesha wanafunzi wote nchini

Bunge: Bodi ya Mikopo inahitaji Tsh. Bilioni 800 kukopesha wanafunzi wote nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo amesema Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, (HESLB), inahitaji Sh800 bilioni ili iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote waliodahiliwa kujiunga na vyuo vikuu.

Nyongo ametoa kauli hiyo leo Jumanne Novemba Mosi, 2022 wakati akichangia hoja ya wanafunzi wa elimu ya juu kukosa mikopo iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM) Ezra Chiwelesa.

Amesema vigezo vinavyotumika kutoa mikopo vinavyoelezwa na HESLB, vinachanganya kwamba wanatoa mikopo kwa wanafunzi wasio na uwezo na yatima.

Amesema asilimia 62 ya mikopo inayotolewa na HESLB imekuwa ikitoa kwa wanafunzi waliosoma masomo ya sanaa (arts) ambao wakimaliza wanakwenda mtaani kwa sababu ya ukosefu wa ajira na hivyo kutorudisha mikopo.

Amesema asilimia 20 ya wadahiliwa wanaokwenda kusoma masomo ya sayansi na ndio waliopatiwa mikopo na asilimia tano japo hawakuomba.

Ametaka elimu itolewe kwa wazazi, kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa wanafunzi, lakini watalazimika kuilipa watakapomaliza masomo yao.

MWANANCHI
 
Sasa kama hao wachache hawakuomba kwa nn wapatiwe mikopo?hiyo ni janja janja ya bodi,imulikwe zaidi kuna kitu kimejificha. Kwani kigezo cha kupewa mkopo ni sharti usome sayansi. Ina maana wanataka watoto wote wasome sayansi? Basi kama ndivyo waishauri serikali ifute masomo ya arts wabaki na ya sayansi. Kwa hiyo bodi inatufikirisha wote waliosoma sayansi wanaajiriwa?
 
Wakati wanasema pesa kiwango hiki waangalie pia vigezo vinavyotumika na kama kweli wanafunzi wote wanaonufaika na mikopo kwa sasa wamepita kwenye msasa huohuo na vigezo hivyo hivyo, maana ni ushuzi mtupu.
 
Hatuhitaji Wana Sanaa wengi,tunahitaji wanasayansi na madakitari, kozi za IT, computer, engineering ndio zipewe mikopo kwa asilimia 100.
 
Serikali ikope iwakopeshe haraka, Ili hata sie tuliokatwa zaidi turejeshewe pesa zetu. Juzi waliniambia Ili tukurudishie kiasi kilichozidi kwenye makato yako kuipitia mshahara wako utaanza kufikiriwa kurejeshewa baada ya kupita siku 90. Haiingii akilini kabisa. Hii sheria sijui ilitungwa na nani?
 
Hatuhitaji Wana Sanaa wengi,tunahitaji wanasayansi na madakitari,kozi ,za IT,computer,engineering ndio zipewe mikopo Kwa asilimia 100
Hao wa IT na madaktari sasa hivi wako mitaani,hawana ajira sasa hiyo mikopo watalipaje?bora umfadhili kijana anayesoma veta ambaye akimaliza tu kozi yake anajiajiri kuliko hao ma white color job. Wakishamaliza tu hawafikirii kujiajiri bali kuajiriwa sasa unategemea nini jamani tuwe wakweli hii elimu ya makaratasi inaajirika kweli.ni wangapi mfano anayetaka kujenga nyumba yake ya kuishi anamchukua graduate amfanyie hiyo kazi.mtaani vijana wengi waliojiajiri ni product ya veta na wala hatuwaoni hao graduate.
 
January anaifilisi hazina keshaitupia zigo la 2.4 trillion ya madeni ya TANESCO ili aweze kukopa upya kufanya upuuzi wake in the name of modernisation ya shirika na ‘bi tozo’ anabariki upuuzi wake.

Sasa hizo hela za kuwapa watoto wa maskini wapate elimu watoe wapi wakati mapato ni kwa ajili ya sherehe za uzinduzi, makongamano, safari, OC za wizara, kulipa madeni ya maza, ya mashirika ya umma na kilichobaki kiliwe na wajanja kwa njia wajuazo.

Hawa sio watu wenye kujali shida za walalahoi wala watoto zao. Halafu wanamajibu ya dharau kweli awakawii kukwambia sio lazima kila mtu awe na degree wengine warudi makwao kulima.
 
Yaani kwenye huu uzi watu tuliopasuwa upande wa mfecane war"" 😎😎😎tunadharauliwa thana utafikiri tuliwaladhimisha msomee izo metamofosisi
 
Back
Top Bottom