Bunge halijatenda haki kutowasilisha muswada wa Bima ya Afya kwa wote

 
Nia ya Waziri wa afya ni njema ila utekelezaji wa nia hii katika uhalisia wa maisha ya kila siku ncini Tanzania ndio bado ni sinto fahamu. Kabla sija tazamwa kwa jicho la mke mwenza ni vyema kufahamu kwamba mkakati wa kufufua shirika la bima ya afya Tanzania kwa kudunduliza michango ya wanachama wapya ni hafifu. Ningependa kufahamu zaidi kuhusu gharama za uendeshaji za NHIF na deni la shirika hili ili kupata mantiki kuhusu idadi ya michango ambayo ita wezesha shirika hili kujiendesha bila bugudha. Kama malengo ya bima ya afya kwa wote ni kuboresha huduma za afya kwa watanzania wote basi hilo litakuwa jambo zuri lakini kama malengo ya mabadiliko haya ni kuifufua NHIF basi sidhani kama njia hiyo ni sahihi. Sambamba na hayo, wananchi kukosa huduma mbalimbali kwa kutokuwa na bima ya afya haina tofauti na kuwa lazimisha kujiunga na mfuko huu. Tusisahau kwamba ita mugharimu kila mtanzania shilingi 192,000 kwa mwezi kwa kifurushi cha chini kabisa cha NHIF. Katika mpango wote wa kuhusisha bima ya afya na huduma mbalimbali tujiulize kama kweli haya yote yana wezekana.

Tathmini ya kina inatakiwa ifanyike ili kufahamu nini haswa kina sababisha shirika hili kuanguka. Tuelewe kwamba serikali pamoja na watoa huduma za afya wanatakiwa waweze kuboresha huduma kwa wogonjwa bila kuwa na ongezeko la wagonjwa wa kulipia. Yaani badala ya kutumia masaa 12 kupata huduma kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili basi muda huu usiwe zaidi ya masaa mawili hata kwa wote wanaondelea kupata huduma katika kipindi hiki. Hii ina maanisha kuwa na watoa huduma wanaotosha na wanao jituma, kuwa na vipimo vya kisasa vinavyo jitosheleza na kuwa na dawa za kutosha kwa wagonjwa wote wanaopata huduma chini ya mfuko huu. Tusisahau pia umuhimu wa kuzingatia kikomo kwa kila mchangiaji ili kuhakikisha kwamba shirika halipati hasara na pia kuhimiza matumizi ya bima pale muhusika anapo ugua tu.
 
umesema vyema...umeonesha wasiwasi wako kuhusu bima ya afya ...umegusia changamoto na suluhu pia.hoja yangu katika uzi huu ni moja tu na muhimu.Bunge lilipaswa kutoa fursa hii adhimu ya mjadala ili maslahi ya wote yazingatiwe katika sheria ya bima ya afya au baada ya mjadala bunge lingetoa maelekezo kwa Serikali kuhusu bima ya afya kwa wote /namna bora ya uchangiaji wa huduma za afya nchini ...badala yake tumejionea danadana na ukwepeshaji wa mjadala huu bila sababu yoyote ya msingi unayoweza kuisemea.
Bunge limepoka mamlaka ya wananchi kuhusiana na mjadala huu...linapaswa liambiwe kuwa limepotoka
 
Sawa kabisa, bunge letu linatakiwa litunge sheria zinazohusu uendeshwaji wa NHIF. Labda NHIF act au kitu kama hicho. Vile vile tuna takiwa kuwa na mchakato wa uhakika na wa kudumu utakao toa maelezo kuhusu mambo yanayo jadiliwa bungeni. Nina hisi kwamba mambo mengi yanatakiwa yamalizwe huku chini na yasifike katika kitengo hicho cha serikali. Maoni yangu yanaeleza kwa undani kuhusu NHIF lakini wanao fahamu zaidi kuhusu suala hili ni wataalam wa afya wanao hudumia wagonjwa walio jiunga na mfuko huko. Janga hili ni fursa kwa washika dau wote kufanya reasearch na nina amini kwamba tutapata majibu yote kutoka watoa huduma kwenye hospitali zetu. Siamini kwamba wabunge wetu wana uelewa wa kutosha kuhusu suala hili na siku zote naamini kwamba usiandikie mate wakati wino upo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…