Askofu Gwajima,
Kwanza sikubaliani na wewe katika suala la kukataa chanjo ya Corona kwa kadiri unavyowahubiria waumini wako. Binafsi nimeshachanjwa na ninahimiza watanzania wote wachanje tofauti na unavyohubiri katika kanisa lako.
Hivyo, dawa pekee ya mimi kukupinga ni kwenda kuchanja na hivyo tayari nimeshachanjwa na sitarajii kupata madhara unayohubiri. Hivyo mimi ni mpinzani wako halisi katika mahubiri yako.
Lakini pamoja na kukupinga kwa staili yangu ninalipinga Bunge hatua linazochukua dhidi yako.
Umeitwa kwenye kamati ya Bunge kwamba umesema uongo na kushusha heshima ya bunge. Hapa mimi nakutetea kwa hoja zifuatazo.
Ulichokitoa kanisa kwako ni mahubiri kwa waumini wako. Waliandamana kutoka nyumbani wakakufuata kanisani kukusikiliza.
Ulisema vizuri kwamba unazungumza kama mtu wa Mungu na si kama mbunge wa Kawe.
Hivyo, ukifika kwenye kamati ya bunge kwanza waulize wanakutuhumu kwa kauli uliyoitoa wapi. Wakisema ni yale ya kanisani kwako kataa katakata kujibu lolote, waeleze mipaka yao kwamba dola ya Tanzania haina mamlaka ya kukuchagulia mahubiri na haina mamlaka na jambo la kidini.
Waambie wasome ibara ya 19(2) ya katiba inayosema kazi ya kutangaza dini siyo ya dola ni yako na wenzako mnaotangaza dini. Hivyo, usijibu chochote waache waamue wanachokitaka.
Kama wabunge wanakupinga waende kwenye makanisa yao na misikiti yao wafanye tofauti kama nilivyofanya. Mimi nimekupinga kwa kwenda kuchanjwa na ninahamasisha wengi kuchanjwa.
Hivyo, fanya kadiri ya maelekezo yangu, ukiwaacha kesho watafanya kwenye kanisa jingine kwa hoja tofauti.