🤣 🤣 🤣 🤣 🤣Acheni kukwepa mzizi wa tatizo na kushughulikia matawi yake. Tatizo lipo kwenye kiongozi wa umma kuwa pia kiongozi wa dini! Hapa ndipo lilipo tatizo hasa. Kuna mgongano wa maslahi. Ama angejiuzulu uongozi wa kanisa na abaki kama muumini wa kawaida au ajiuzulu ubunge na abaki kuongoza kanisa. Ndiyo maana huwa wanasema hata kama mtu ni mkurugunzi wa kampuni na anataka kugombea uongozi wa umma kama ubunge, inabidi ajiuzulu kwanza ule ukurugenzi ili akipata ubunge kusiwepo na mgongano wa maslahi. Gwajima angekuwa ameachia ngazi ya kuongoza kanisa lake na kuwa muumini wa kawaida haya yote yasingetokea.