Bunge halina mamlaka kumhoji Askofu Gwajima alichoongea na waumini wake

Bunge halina mamlaka kumhoji Askofu Gwajima alichoongea na waumini wake

🤣 🤣 🤣 🤣 🤣Acheni kukwepa mzizi wa tatizo na kushughulikia matawi yake. Tatizo lipo kwenye kiongozi wa umma kuwa pia kiongozi wa dini! Hapa ndipo lilipo tatizo hasa. Kuna mgongano wa maslahi. Ama angejiuzulu uongozi wa kanisa na abaki kama muumini wa kawaida au ajiuzulu ubunge na abaki kuongoza kanisa. Ndiyo maana huwa wanasema hata kama mtu ni mkurugunzi wa kampuni na anataka kugombea uongozi wa umma kama ubunge, inabidi ajiuzulu kwanza ule ukurugenzi ili akipata ubunge kusiwepo na mgongano wa maslahi. Gwajima angekuwa ameachia ngazi ya kuongoza kanisa lake na kuwa muumini wa kawaida haya yote yasingetokea.
Mimi namwona Gwajima ni Mwanasiasa tu tena siasa za CCM. Asitudanganye eti ni kiongozi wa kiroho. Hakuna kiroho hapo, ni porojo za siasa tu.
 
Mimi namwona Gwajima ni Mwanasiasa tu tena siasa za CCM. Asitudanganye eti ni kiongozi wa kiroho. Hakuna kiroho hapo, ni porojo za siasa tu.
Kabisa. Huyu ni mtafutaji kama watafutaji wengine. Kwenye dini hayuko kabisa.
 
Kuna azimio la Bunge lililopitisha chanjo gwajiboy amekiuka? Hau ameshushaje heshima ya Bunge wakati Bunge lenyewe halina heshima.
 
Uganda haijaanza na Kibwetere watu kufia dini, walianza akina Karoli Lwanga kama hujui.
Kwa hiyo kwako wewe Kibwetere ni sawa na Lwanga? Kuna kundi la viongozi wa dini la akina Lwanga na kuna kundi la viongozi wa dini la akina Kibwetere na Gwajima na kuna makundi mengine pia. Usifikiri kila anayejiita kiongozi wa Kiroho basi yuko hivyo. wengine ni wachumia tumbo na wasanii tu kama Gwajima. Nini kilimfanya ajiunge na CCM na kugombea ubunge? Alitaka nini hasa zaidi ya maslahi?
 
CCM kwa CCM....mwl Nyerere aliwahi kusema kwamba "dhambi ya ubaguzi haiishi,ukimaliza kumbagua huyu kuwa sio mwenzako (mf wapinzani hawapo bungeni,jinsi walivyofanyiwa ccm wanajua) sasa wataanza kubaguana wao kwa wao
 
Unafahamu kadi ya uanachama wa CCM Dr. Slaa aliipata lini na alikuwa anafanya kazi gani?

Unamjua padri Supa wa Dodoma aliyekuwa mbunge?

Ficha umbumbumbu wako usipojua mambo.

Kwa hiyo kwako wewe Kibwetere ni sawa na Lwanga? Kuna kundi la viongozi wa dini la akina Lwanga na kuna kundi la viongozi wa dini la akina Kibwetere na Gwajima na kuna makundi mengine pia. Usifikiri kila anayejiita kiongozi wa Kiroho basi yuko hivyo. wengine ni wachumia tumbo na wasanii tu kama Gwajima. Nini kilimfanya ajiunge na CCM na kugombea ubunge? Alitaka nini hasa zaidi ya maslahi?
 
Kuna azimio la Bunge lililopitisha chanjo gwajiboy amekiuka? Hau ameshushaje heshima ya Bunge wakati Bunge lenyewe halina heshima.
Kwani hujui kuwa bunge lilimpongeza Salimia kwa kazi kubwa na kwa jinsi anavyoliongoza taifa? Rais aliunda tume ya Korona na ikatoa taarifa yake kuwa itolewe chanjo.

Pia waziri wa Afya alipeleka bajeti yake bungeni na kuainisha yatakayofanywa na wizara yake ikiwemo kupambana na Korona ikiwemo Chanjo.

Huyo huyo Gwajima na wenzake wakapitisha kwa makofi mengi. Leo anajifanya hataki. Aache siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Wanaomchukulia Gwajima kama kiongozi wa dini wanakosea tu. Yule ni mwanasiasa tena wa siasa za CCM.
 
Sisi tunamtaka mbele ya kamati atutajie majina ya viongozi waliopata rushwa ili kuiruhusu chanjo ya Corona.
Pia tunamtaka atuambie majina ya viongozi waliochanjwa chanjo fake.
Kisha tutamtimua bungeni akabinywe mbupu na manjagu.
Dini gani hiyo ya kuhubiri CORONA kila siku!!
 
Unafahamu kadi ya uanachama wa CCM Dr. Slaa aliipata lini na alikuwa anafanya kazi gani?

Unamjua padri Supa wa Dodoma aliyekuwa mbunge?

Ficha umbumbumbu wako usipojua mambo.
Kwani sasa huyo Dr Slaa ni Kiongozi wa Kiroho? Hivi kwanini huyo mchungaji wako Gwajima aliingia kwenye Siasa za CCM? Kama siasa za CCM zimemshinda dawa ni kuachana na hicho chama. Vinginevyo ni usanii tu wa Kisiasa, tena siasa za CCM ambazo zinafahamika
 
Bunge wala serikali hawahusiki na utafiti na majaribio ya chanjo ya kovidi-19, nilitegemea watafiti wangemwita gwajima kwenye kamati yao ya watafiti na wanasayansi na kumpasha ukweli wenyewe ulivyo kuliko watu fulani kudemka huko na ma hasira yao na mabavu yao kufanya crackdown kwa gwajima ili kumfumba mdomo asiseme anachokiamini......
 
Back
Top Bottom