Bunge halina mamlaka kumhoji Askofu Gwajima alichoongea na waumini wake

Bunge halina mamlaka kumhoji Askofu Gwajima alichoongea na waumini wake

Aliyekudanganya kwamba CCM inaongoza kwa hizo ibara za katiba ni nani? Chama chake cha Siasa cha Askofu Gwajima kinajulikana tabia zake. Sasa anashangaa nini? Kwani hakujua anajiunga na chama cha aina gani? Na bado. Kuna siku hicho chama chake kitamtuma kwenda kupoteza watu, kuwapiga risasi watu, na hicho chama kina haki ya kuwatumia wanachama wake kufanya kazi zake zikiwemo za kuwaweka watu kwenye viroba.
Na kuwekeana sumu kama kilivyofanya kwa Mangula
 
Waumini wake ni wajinga.

Mtu kaiba kura mchana kweupe lakini mazombi bado yanamsikiliza.

Kuhusu chanjo anatakiwa achague kati ya ccm au kanisa la kitapeli,aache kimoja.

Mimi siamini siku ile kuwa yule Samia alichanjwa kweli,imekaa kisanii sana jinsi alivyochanjwa.

Gwajima ni tapeli lao walilolisaidia kuingia bungeni.

.Kawe wana bahati mbaya,gwajiboy na mzee mdee wote ni makalio
Yeye hakuiba kura ila chama chake! na ndicho pia kinachomsulubu, so cheni feki na hela feki ngoma inogile!!
 
ALijua kuwa ubunge wake umetokana na wizi,kwanini hakuukataa?
 
Waliomhoji gwajiboy walifanya hivyo ili wapate sitting allowance tu halafu wasikie Mambo ya ndaani ndani kabisa ya waziri.
Hawawezi kumfanya chidboy chochoote
 
Waumini wake ni wajinga.

Mtu kaiba kura mchana kweupe lakini mazombi bado yanamsikiliza.

Kuhusu chanjo anatakiwa achague kati ya ccm au kanisa la kitapeli,aache kimoja.

Mimi siamini siku ile kuwa yule Samia alichanjwa kweli,imekaa kisanii sana jinsi alivyochanjwa.

Gwajima ni tapeli lao walilolisaidia kuingia bungeni.

.Kawe wana bahati mbaya,gwajiboy na mzee mdee wote ni makalio
Yaani hapa Gwajima ndioalijimaliza kabisa hata Kama alikuwa mtumishi wa kweli wa Mungu ndipo alipomsaliti Mungu wake kwa kupitia mabox ya kura fake hanatofauti na Yuda sikarioti aliyemsaliti Bwana Yesu kwa vipande therathini vya fedha.
 
Askofu Gwajima,

Kwanza sikubaliani na wewe katika suala la kukataa chanjo ya Corona kwa kadiri unavyowahubiria waumini wako. Binafsi nimeshachanjwa na ninahimiza watanzania wote wachanje tofauti na unavyohubiri katika kanisa lako.

Hivyo, dawa pekee ya mimi kukupinga ni kwenda kuchanja na hivyo tayari nimeshachanjwa na sitarajii kupata madhara unayohubiri. Hivyo mimi ni mpinzani wako halisi katika mahubiri yako.

Lakini pamoja na kukupinga kwa staili yangu ninalipinga Bunge hatua linazochukua dhidi yako.

Umeitwa kwenye kamati ya Bunge kwamba umesema uongo na kushusha heshima ya bunge. Hapa mimi nakutetea kwa hoja zifuatazo.

Ulichokitoa kanisa kwako ni mahubiri kwa waumini wako. Waliandamana kutoka nyumbani wakakufuata kanisani kukusikiliza.

Ulisema vizuri kwamba unazungumza kama mtu wa Mungu na si kama mbunge wa Kawe.

Hivyo, ukifika kwenye kamati ya bunge kwanza waulize wanakutuhumu kwa kauli uliyoitoa wapi. Wakisema ni yale ya kanisani kwako kataa katakata kujibu lolote, waeleze mipaka yao kwamba dola ya Tanzania haina mamlaka ya kukuchagulia mahubiri na haina mamlaka na jambo la kidini.

Waambie wasome ibara ya 19(2) ya katiba inayosema kazi ya kutangaza dini siyo ya dola ni yako na wenzako mnaotangaza dini. Hivyo, usijibu chochote waache waamue wanachokitaka.

Kama wabunge wanakupinga waende kwenye makanisa yao na misikiti yao wafanye tofauti kama nilivyofanya. Mimi nimekupinga kwa kwenda kuchanjwa na ninahamasisha wengi kuchanjwa.

Hivyo, fanya kadiri ya maelekezo yangu, ukiwaacha kesho watafanya kwenye kanisa jingine kwa hoja tofauti.
Mtu asiye na kinga, ambayo ni chanjo, akiugua corona anaweza kuambukiza wengine ambao wanaweza kufa pamoja na yeye mwenyewe. Kwahiyo hili sio suala la dini au imani; ni sayansi.
Hata serikali inakosea kusisitiza uhiari wa chanjo. Ni hatari.
Ni wajibu wa serikali kulinda afya na uhai wa raia WOTE, pamoja na hao wanaotaka kujiua na kuuwa wengine.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom