Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Hakika Uchaguzi UMESHAKWISHA.

Kada nimelisoma bandiko lako FIKIRISHI na kulirudia mara 3.

Nimeona ukiutoa USHAURI ili kuleta MSISIMKO bungeni na kuwa kinyume na ulichopredict kuwa BORING.

Nipende kukumbusha kuwa Wakati wa bunge lililopita,Spika mh.Job Ndugai alipata kuwadhihaki wapinzani waliokuwa na tabia ya KUSUSA VIKAO VYA BUNGE kuwa HAAMINI KAMA WATARUDI BUNGENI KWA WINGI WAO...akaenda mbali kusema kuwa hadhani watapata hata WABUNGE 5...hili LIMETIMIA.

Mh.Rais wetu alipata kusema kuwa 2020 anatamani kuufuta upinzani,naamini hakusema aufute huku mitaani,bali BUNGENI.....hili LIMETIMIA.

Kwetu wanaCCM tunaoutii msimamo wa mwenyekiti wetu tunaona sawa tu wasiwepo bungeni...japo kwa miaka hii 5 ya KUTIMIZA MALENGO MAKUBWA aliyojiwekea mh.Rais na serikali yake....mh.Rais ana hulka ya kutopenda siasa za KUSUSA NA KUTOKATOKA BUNGENI...haina maana kuwa yeye si mwanademokrasia...la hasha kwani hata TRUMP ni mwanademokrasia lakini hajakubali kila LINALORUHUSIWA NA DEMOKRASIA na ndio maana anataka kusitishwe zoezi la kuhesabu Kura na kutaka mahakama iingilie kati,huu msimamo wake unaonekana na baadhi ya WADAU WA DEMOKRASIA kama KUYUMBAYUMBA kwa TRUMP Katika NORMS za DEMOKRASIA...huo utabaki ni mtazamo wao na Trump atabaki na mtazamo WAKE....


Awamu hii ya 5 IMEJIPAMBANUA kulijenga TAIFA kwa KASI YA AJABU kwani TULICHELEWA SANA.....

Ifikie mahali tukubaliane na HULKA YA MH.RAIS wetu ili TUPIGE HATUA KUBWA zaidi ya DEMOKRASIA "inayotakiwa" Katika nchi yetu CHANGA KIUCHUMI NA KIMAENDELEO.


Huko Mbeleni tutayafikia YOTE wayatakayo CRITICS wa mh.Rais na CCM.

Lastly nikushukuru kwa maoni yako CHANYA yenye mustakabali mwema was taifa,japo Binafsi ninataka YASITOKEE ya wapinzani kuteuliwa KIMBELEKO namna hiyo,kwani DEMOKRASIA ina gharama,na miongoni mwa gharama zake ni kupitia MACHUNGU ukiwa UNAJIPANGA ili uboreke zaidi na zaidi.

Uwepo wa wapinzani nje ya muhimili wa Bunge utawapa FURSA YA KUZIDI KUYASOMA MAPUNGUFU YAO na kuungana zaidi kuliko wakati Mwingine wowote ule.

Kudos Kamarade!
 
Paskali tafadhali Sana usiingilie maamuzi ya wananchi kwa hoja zako zisizokuwa na misimamo....kwanza hivi kwanza unawezaje kufanya kazi na vibaraka hao ambao baadhi yao wametumwa kuja kufifisha maendeleo ya nchi yetu..rubbish kabisa achana nap baadhi yao hao..mwana kulitaka mwana kulipata..bila watu kuliweka Taifa hili chini ya mikono ya Mungu labda lingesambaratika kabisa..na Wao hao ndio chanzo...hivi mtu utaibukaje na kuwaambia wazungu wakawashtaki Mahakama ya kimataifa baadhi ya wezi wa

kura, vyombo vya ulinzi na usalama, tume ya uchaguzi hii iliyosimamia vizuri uchaguzi..khaaa..eti wachunguzi wa kimataifa waje wawachunguze. Mwanasheria wao Amsterdam akaagizwa kufanya hayo..it's rubbish and stupidity...kabisa Mtanzania wa leo anafanya hayo..loh...waende zao achana nao..na hasa lissuu hafai hata kuishi nchini..Hana uzalendo anatumiwa tu huyo na mabeberu kwa manufaa wanayoyajua wenyewe..achana nao..ingawa wapo wanaojitambua kidogo hapo

Lakini Lissu, Zito hawafai hata kwa kulumangiwa...hata wananchi wa majimbo yao hawawataki, what do you expect. Eti kaenda kutafuta legitimacy ya kwenda ubelgiji kwa kwenda kujifungia ubalozi was ujerumani...eti anatishiwa..Lissu huyo...ina maana anaihusisha serikali na propaganda zao. Stu.p.idy...nani atamtafuta huyo chizi..mwache amalize kesi zake then aondoke Kama akiruka kifungo
 
Bunge lijalo

Spika -wabunge naona mmetulia saana hv ndo inavyotakiwa naona bunge zima Sasa ni Wastaarabu mpak raaahaa!

Wabunge-Paah!! Paah! Paaah!!

Spika-naona mkono pale Eeeh! Mh.gwajima ni hoja au Taarifa

gwajima _nina lakusema basi jamani Bwana Yesu Asifiwee saana!
 
CCM na NEC walishirikiana kutenda uovu wa kuondoa wagombea wa vyama vya upinzani tangu mwaka jana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wakaiba hadharani bila aibu kwa makusudi kabisa huku wakijiamini wanaulinzi wa polisi kwani hawakujua umuhimu wa vyama vya upinzani?
 
Nimesoma makala yako machozi yemenilenga lenga, nimeumia Sana umeandika kwa uchungu.

Nawaza tu mtu kama Zitto kuwa nje ya Bunge nani atatuchambulia Bajeti Kuu, Nani atachambua ripoti ya CAG...inauma Sana kwakweli.

Tujiandae kushuhudia viroja huko Bungeni, na vile Bunge litakuwa live itakuwa zaidi ya Futuhi.
 
Tunahitaji katiba na sheria zinazoeleweka siyo huruma na bla bla ili watu wanaojipendekeza kama wewe waonekane na kupewa teuzi. Watanzania tumeona kwa macho uchaguzi ulivyokuwa.

Bashiru alisema wazi kuwa CCM itatumia dola kubaki madarakani na wametumia tayari.

Mpinzani yeyote atakayekubali teuzi siyo Mpinzani bali anaangalia tumbo na kusaliti watanzania.
 
Bwana Njaa - tafsiri ya jina lako.

Kwa katiba yetu na muundo wa tume ya uchaguzi, wapinzani kushinda ni huruma tu. Kwa namna moja au nyingine wahusika wote ni watu walioteuliwa na chama. sasa maagizo yoyote ya kiongozi wa chama hayawezi kupingwa na mteule.

Tuchague moja. kama tunaamini vyama vingi vinatufaa, basi tubadilishe huu muundo wa tume

Au kama mfumo wa vyama vingi tunauogopa mtumie wingi wenu kuufuta. tutapiga kelele ,mtatuwekea wale jamaa wafanye usafi. tutanyamaza, itakuwa kama kwa mzeee Kibwenzi na maisha yatasonga tu

Hivi unashauri viti maalum kwa hao watu wa5 uliopendekeza wakafanye nini huko bungeni, wakapinge ili watolewe nje au wakaunge mkono mawazo ya upande huo
 
Wala halina hali mbaya. Nchi itapata maendeleo. Magufuli atapeleka maendeleo sehemu zote za nchi isipokuwa majimbo machache tu ya CHADEMA, ACT na CUF. Hakuna haja ya kusikitika. Tushangilie. Tanzania inakwenda kuwa kama Ulaya.

Post yako imejaa contradictions.
 
Magufuli hajashinda kwa kishindo Bali kapata ushindi wa LUSHINDO
Magu ni zee kura zenye mabegi.


1604741248341.png
 
Nilifikiri kambi rasmi ya upinzani iko kisheria kumbe inategemea huruma ya mtu mmoja, Watanzania tuna safari ndefu sana.
Mkuu Mwarobaini, Quinine , kambi rasmi ya upinzani ipo kisheria, ila ili iundwe rasmi, lazima kuwemo na akidi ya asilimia 12.5 ya wabunge wote ambao ni wabunge 44. Kwa idadi ya wabunge 4 tu wa kuchaguliwa kutoka upinzani, hata ukiwapa wabunge 20 wa viti maalum, bado akidi haitatimia, watu wawili pekee wenye uwezo wa kuteua wabunge ni Rais wa JMT kwa wabunge 10, na rais wa Zanzibar kwa wawakilishi 10, ambapo wanaweza kuja Bunge la JMT.

Vinginevyo pia Bunge lina mamlaka yake ya kutengua kanuni yoyote, hivyo kikao cha kwanza kitaanza na utenguzi wa hiyo akidi ya kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni ili iundwe na wabunge hao hao waliopo.
P
 
Kwahiyo hao wahuni walioiba uchaguzi hawakuyaona hayo yote hapo kabla isipokuwa wewe tu?

Hiyo intelijensia yao haina utambuzi wa maswala ya bunge na miongozo ya upitishaji wa bajeti isipokuwa wewe tu?
 
Back
Top Bottom