Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Kuna binadamu huwa mnajisahau sana.

Bunge likiwa na hali mbaya sisi tufanyaje kwa mfano?
Tulipe dawa?

Ikiwa wananchi wenyewe kwa matakwa yetu tulielewa kuwa hakuna haja ya kuchangua viongozi wa upinzani na kuamua tuliyo yaamua ile tare 28/10/2020.

Wewe inakuwaje tena unakuja kulalamika humu.Basi tumelogwa tena kulogwa hasa kusiko na dawa.

Hoja kama hizo za nini kipindi hiki?

Huu si wakati wa kuanza kulalama juu ya tulicho amua.Si muda wa kusingizia chochote kuwa kuna ubaya juu ya bunge na mihimili yote mitatu kwa ujumla.

Ni muda wa kufanya kazi na kuendeleza Nchi hii kwa kadri tulivyoamua sisi Watanzania.

Tuache kuomba omba huruma.

Bunge vyovyote litakavyokuwa ni matendo na maamuzi yetu sisi Watanzania hatuhitaji msemaji kwa sasa.
 
Sasa hao watakaoteuliwa na rais kwenda kambi ya upinzani watamsaidiaje rais, kwa kumpinga wakati yeye hataki kupingwa au unataka bunge la show kuwaridhisha ‘mabeberu’ ili watupe misaada, I don’t see the logic behind.

Hiyo kambi ya kuteuliwa na CCM kujifanya wapinzani haitakuwa tofauti na genge maalumu la CCM kujifanya wapinzani, Mrema type not healthy to our nation.

Tunataka kambi rasmi ya upinzani bungeni iliyo huru independent siyo ya kupangiwa na mtu, huyo Zitto unayesema apewe upendeleo hatakuwa Zitto tunayemjua.
 
Mugufuli alisema zamani ikifika 2020 hataki kuona chama cha upinzani na amesimama kwenye maneno yake. na kwasasa mpizania yoyote atakaye nyanyuwa kichwa chake nafikiri hukumu yake itakuwa ni kifo tu sioni jengine ni kama vile zanizibar hivi sasa mauwaji na utesaji unaendelea huko Pemba kila siku maiti zinaokotwa.

Halafu wewe ivi kukiwa na kampi ya upinzani bungeni inawasaidia nn CCM halafu unazungumzia maendeleo ivi wewe hujuwi kama ccm sasa ni mwaka wa 60 kutawala Tanzania ni maendeleo gani walioyaleta mpaka sasa bungeni wanazumgumzia matundu ya choo shuleni
 
Mkuu lengo la CCM limetimia "kuufuta upinzani" sasa sijui kama bwana Paskali hoja yako itasikizwa.

Itakuwa fatal mistake. Baada ya referendum 1992, Mwalimu Nyerere alisimama akasema wachache wape. Tunahitaji vyama vya upinzani. Mwinyi akaruhusu. Mkapa akawaacha, JK pia. Sio busara kuviacha vife. Vina mchango wake kwenye society
 
Kambi rasmi ya upinzani bungeni ilikua na maana kuanzia 1995 hadi 2015.

Kuianzia 2015 hadi leo hakuna haja ya kambi rasmi ya upinzani bungeni, kwakifupi hakuna haja ya vyama vya upinzani! kwanini tuwe wanafiki?

Kama rais anaona wapinzani ni wasaliti wanaomkwamisha kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya maziwa na asali sasa kuna haja gani ya kuwa nao bungeni?

Ikiwa NEC , TISS, Polisi na JWTZ wametumia nguvu zote kuhakikisha tunakua nchi ya chama kimoja kuna haja gani ya kuwa na kambi rasmi ya upinzani?

Tujifunze kukubali consequences za maamuzi yetu, unafiki ufike mwisho.
 
Sijaelewa unaposema wakiingiwa na huruma?

Kwani wao hawajui wajibu wao kuwa ni kuwatumikia watanzania na kuifanya Tanzania isonge mbele?

Yaani akili zetu sijui tunazificha wapi. Tunachagua watu watuongoze alafu tunataka watuonee huruma.
 
Mawazo mazuri sana, tena sana. But wao CCM waliona bora njia hii waliyotumia kuliko hiyo ambayo unawaza kaka yangu Paskali.

Wao wanataka upinzani ufe, na sio ufe tu but Tanzania mzima kusiwe na mtu mwenye mawazo mbadala.

Watu wote tuwe na wazo moja la mirad mikubwa, sisi inchi Tajiri, tunaonewa wivu na Wazungu, madaraja, flyover Yan watu wote tuwe na lugha moja.
Ni kweli kwani maisha hayataenda? Mwl.nyerere alituongoza kupitia mfumo huo na maisha yakaenda.Inaumiza sana kuwa na upinzani umaolifanyia udalali nchi yetu, upinzani uliotayari kupiga bei nchi.Hatuhotaji bora mfumo wa chama kimoja na rasilimali zetu xikabaki salama
 
Back
Top Bottom