Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

CCM mlichokifanya sijui kama mwanzoni mlifikiri kuhusu hilo ! Katibu Mkuu wenu alijinasibu waziwazi mtakachokifanya kwa kutumia dola na kweli mkakifanya mkidhani watu hawatoona au watanzania ni wale wa Zama za TANU huku wewe mwenyewe ukikiri CDM ikihitahidi itapata mbunge mmoja


Kuna mwalimu wangu aliniambia zamani usije ukamuamini mtu asiyependa ushindani! Ni muoga hata mafanikio yake ni ya uongo ! Kwa akili yangu siamini wahitimu,wastaafu ,watumishi ,wastaafu na wafanyabiashara waliamua kuchagua mateso kwa miaka mingine 5 ! Mlichokifanya ikiwemo kuzima mtandao mnayajua hatupaswi kujiuliza tena! Kigogo alishawaambia acheni kutafuta solution fupi kwa matatizo ya kudumu

Mwisho niseme sasa ni wakati wa mavuno kwanini nasema hivi na kwanini wanaccm mmeanza kuweweseka ni kutakapotokea hoja tata nani wa kupinga hata kama zinawaumiza nyie wenyewe ilhali mliozoea kuwatanguliza na kuwaita "wapingaji wa maendeleo " hawapo tena ! Jibu ni kuwa kama nyie ni familia moja mkiua majirani wakaisha basi mtabaki famiilia moja ndipo wivu baina yenu utaanza nanyi mtamalizana kama mlivyowamaliza majirani! Kwa rai yangu wapinzani wakae pembeni sasa nanyi mvune mlichopanda tutarajie watu kuitwa "washamba" live this time...!
 
Hao wote uliowataja na kupendekeza wateuliwe kuwa wabunge ni viongozi wa vyama vyao.Kwa hiyo wanaweza kufanya ukosoaji au kuwatumikia watanzania kupitia vyama vyao.
Ukizingatia malalamiko yao kwamba bungeni hoja zao huwa hazifanyiwi kazi,basi hawana haja ya kuwepo huko ambako kazi yao wanadai haina tija.
 
Mawakala wa MABEBERU ,wapinga maendeleo wakafanye nini Bungeni.
CCM imeshatimiza malengo
Bunge la chama kimoja upizani unakufa .
Nchi itapata maendeleo ya haraka sanaaa .itakuwa kama urayaaaaaa
Kama faida au hasara ya kuuwa vyama vya upizani tutaipata WOTE.
 
Sio huyu Mayalla Tu, Watanzania wengi waliosoma na wasio soma upeo wao wakuona vitu Kwa uhalisia ni mdogo Sana

Ukiona comments za Watu humu JF na mitandao mwengine ya kijamii utashangaa..

Tuna safari refu sana ya kulijenga TAIFA letu..
 
"Kufuatia poor performance ya vyama vya upinzani kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwa Watanzania kuvikataa na badala yake kukichagua CCM pekee, but 4!, idadi hiyo haiwezi kutimiza akidi inayotakiwa kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni".

Haya maneno hapa yata kuhukumu Siku moja Mkuu kwa kujifanya hukuona mambo yalio fanywa na upande wa pili dhidi ya Wapinzani.
Waafrika ni wanafiki,..

Nafikiri Kayayaona yaliyofanywa na CCM ikisaidiwa na vyombo vya dola,isipokuwa unafiki umemzidi
 
Logical, lakini hapo pa kumteua kibaraka wa mabeberu lissu ndo napingana na wewe. Hastahili kupewa heshima ya hivyo. Unalisaliti taifa lako, unahamasisha na kutaka taifa lako liingie kwenye machafuko ili kumeet your personal political interests, then upewe heshima ya kuteuliwa kuwa mbunge? Come on now ......!!
 
Logical, lakini hapo pa kumteua kibaraka wa mabeberu lissu ndo napingana na wewe. Hastahili kupewa heshima ya hivyo. Unalisaliti taifa lako, unahamasisha na kutaka taifa lako liingie kwenye machafuko ili kumeet your personal political interests, then upewe heshima ya kuteuliwa kuwa mbunge? Come on now ......!!
Mwizi ni mwizi kwenye imani yangu mwizi hukatwa mkono au shingo

CCM wezi hawafai kuwaongoza Watanzania,shutuma za Lisu kuwa kibaraka wa Wazungu hazina mshiko

Wale walio saini mikataba mibovu miaka nenda miaka Rudi Kwa ajili ya political interests zao na kujaza matumbo Yao ndio inafaaa wasipewe heshima

Walaaniwe ,Waumbuke hapa Duniani na akhera
 
Siwashauri CDM kukubaliana na vyeo vyovyote vya mbeleko, vyeo hivyo wapewe vyama visivyo na uwezo wa kupata kura. CDM imepata kura nyingi sana, ambazo matokeo yake yamechezewa ili kuwabeba CCM. Itakuwa ni upuuzi kuporwa sehemu ulizoshinda kihalali kisha, uje upewe nafasi za upendeleo na aliyekupora ushindi. Ww Paskali ndio unatetemekea vyeo vya mbeleko, usilazimishe kila mtu apewe vyeo vya mbeleko. Nitawadharau sana cdm iwapo watakubali huo uteuzi huku hujuma ya wazi ikiwa imefanyika. Msitake kumgeuza rais ni Mungu huku akiwa ananajisi uchaguzi waziwazi.
 
Miongoni mwa waliofurahia kuhusu kufutwa kwa upinzani sasa hizi hoja zako za kutokuwepo bunge makini kwasababu hakutkuwepo na upinzani ni zanini?

Ujinga wenu watu mmewafanya vilema na kuwauwa kwa Ujinga wenu sasa fanyeni upuuzi wenu huko tuone kidole kimoja kitabanja chawa.
 
Hatuhitaji huruma ya mtu, tunahitaji uchaguzi huru na wa haki na pia kuwa na mahakama huru yenye kuweza kuamua mshindi halali pasipo kupokea maagizo kutoka kwa mtu yoyote.

Alafu acheni unafiki.Mnachokitafuta sasa ni wapinzani wachache ili mridhishe wafadhili na ili mfute aibu ya ubakaji wa demokrasia mlioufanya.

Endeleeni na Bunge lenu.

Huyu Paskali anaona watu ni wapuuzi, yaani uporwe ushindi kisha ukubali cheo cha huruma, tena toka kwa huyo huyo aliyekupora! Hawa akina Paskali ndio wanaondekeza chaguzi za nchi hii kuendelea kuchezewa na wahuni.
 
Bunge litakuwa lenye utulivu na lenye kujadili issues na sio watu.

Watanzania wanataka maji safi,afya bora,elimu bora,ajira,fursa za kibiashara na mazingira mazuri ya kibiashara,amani na utulivu basiii.

Hawaitaji watu maarufu wa kususia vikao na kufanya Fuji.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Pasco Yan haueleweki unataka nn japo unaweza jiona upo sahihi lakini usahihi wako ...... Anyway sitaki kukvunjia heshima yako
 
Anauokoaje upinzani aliotakanikwa muda mrefu ufe ??!! Kama amefanikiwa lengo lake hayimaye, anaanzaje tena kurudi nyuma katika malengo? Usimpotoshe!
 
Subiri uione Tz ya kijani inavyofanana, bado hata miswada haijaja bungeni unaanza kutafuta wa kuipinga? Hakuna kitu kinachoitwa bunge kubore, bunge si sehemu ya entertanment kuwa linatakiwa lisichoshe kulitazama, moja ya kazi ya bunge ni kupitisha miswada ili raisi asaini iwe sheria. JUST WAIT AND YOU WILL UNDERSTAND IF TZ NEEDS WAPINGAJI.
 
Hatuhitaji huruma ya mtu, tunahitaji uchaguzi huru na wa haki na pia kuwa na mahakama huru yenye kuweza kuamua mshindi halali pasipo kupokea maagizo kutoka kwa mtu yoyote.

Alafu acheni unafiki.Mnachokitafuta sasa ni wapinzani wachache ili mridhishe wafadhili na ili mfute aibu ya ubakaji wa demokrasia mlioufanya.

Endeleeni na Bunge lenu.
Tatizo kura zenu mnapigia JF na twitter!!
 
Ni kweli kwani maisha hayataenda? Mwl.nyerere alituongoza kupitia mfumo huo na maisha yakaenda.Inaumiza sana kuwa na upinzani umaolifanyia udalali nchi yetu, upinzani uliotayari kupiga bei nchi.Hatuhotaji bora mfumo wa chama kimoja na rasilimali zetu xikabaki salama

Kupitia Nyerere ndio tulivaa viraka, na yote ilichangiwa na kuzungukwa na watu waliocopy mitazamo yake.
 
Back
Top Bottom