Hakika Uchaguzi UMESHAKWISHA.
Kada nimelisoma bandiko lako FIKIRISHI na kulirudia mara 3.
Nimeona ukiutoa USHAURI ili kuleta MSISIMKO bungeni na kuwa kinyume na ulichopredict kuwa BORING.
Nipende kukumbusha kuwa Wakati wa bunge lililopita,Spika mh.Job Ndugai alipata kuwadhihaki wapinzani waliokuwa na tabia ya KUSUSA VIKAO VYA BUNGE kuwa HAAMINI KAMA WATARUDI BUNGENI KWA WINGI WAO...akaenda mbali kusema kuwa hadhani watapata hata WABUNGE 5...hili LIMETIMIA.
Mh.Rais wetu alipata kusema kuwa 2020 anatamani kuufuta upinzani,naamini hakusema aufute huku mitaani,bali BUNGENI.....hili LIMETIMIA.
Kwetu wanaCCM tunaoutii msimamo wa mwenyekiti wetu tunaona sawa tu wasiwepo bungeni...japo kwa miaka hii 5 ya KUTIMIZA MALENGO MAKUBWA aliyojiwekea mh.Rais na serikali yake....mh.Rais ana hulka ya kutopenda siasa za KUSUSA NA KUTOKATOKA BUNGENI...haina maana kuwa yeye si mwanademokrasia...la hasha kwani hata TRUMP ni mwanademokrasia lakini hajakubali kila LINALORUHUSIWA NA DEMOKRASIA na ndio maana anataka kusitishwe zoezi la kuhesabu Kura na kutaka mahakama iingilie kati,huu msimamo wake unaonekana na baadhi ya WADAU WA DEMOKRASIA kama KUYUMBAYUMBA kwa TRUMP Katika NORMS za DEMOKRASIA...huo utabaki ni mtazamo wao na Trump atabaki na mtazamo WAKE....
Awamu hii ya 5 IMEJIPAMBANUA kulijenga TAIFA kwa KASI YA AJABU kwani TULICHELEWA SANA.....
Ifikie mahali tukubaliane na HULKA YA MH.RAIS wetu ili TUPIGE HATUA KUBWA zaidi ya DEMOKRASIA "inayotakiwa" Katika nchi yetu CHANGA KIUCHUMI NA KIMAENDELEO.
Huko Mbeleni tutayafikia YOTE wayatakayo CRITICS wa mh.Rais na CCM.
Lastly nikushukuru kwa maoni yako CHANYA yenye mustakabali mwema was taifa,japo Binafsi ninataka YASITOKEE ya wapinzani kuteuliwa KIMBELEKO namna hiyo,kwani DEMOKRASIA ina gharama,na miongoni mwa gharama zake ni kupitia MACHUNGU ukiwa UNAJIPANGA ili uboreke zaidi na zaidi.
Uwepo wa wapinzani nje ya muhimili wa Bunge utawapa FURSA YA KUZIDI KUYASOMA MAPUNGUFU YAO na kuungana zaidi kuliko wakati Mwingine wowote ule.
Kudos Kamarade!