Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Kwa taarifa yenu serikali inakwenda kufanya kazi kwa kasi mpya na wananchi wategemee maendeleo yenye tija.Tunapigania kuwa taifa lenye uchumi wa kati WA JUU.Tunatarajia kuwa taifa lenye uchumi wenye nguvu katika ukanda wa Afrika Mashariki kati na kusini. Upinzani utatuchelewrsha bana, mbona CHINA hana upinzani na mambo yake ni super.
 
Magufuli hajashinda Urais kwa haki kwanza ulijue hilo! La pili Wabunge wa Upunzani wameibiwa kura zao na kulikuwa na kura fake nyingi tu! La tatu usijifanye msamaria mwema kwa Wapinzani wewe ni moja ya watu WANAFKI SANA HAPA DUNIANI!
 
Baada ya JPM kuwaambia wakurugenzi kuwa hatawalipa mishahara iwapo watatangaza wapinzani kushinda ndio hili limetokea sasa.

Uchaguzi ulikuwa wa upendeleo na udanganyifu.NEC imetufikisha hapo.Hakuna mwwnye furaha
 
shutuma za Lisu kuwa kibaraka wa Wazungu hazina mshiko
Unasema hivyo kwa kuwa huna unachokijua juu ya hili. Sikulaumu!
Yeye aende zake huko Belgium akaishi kwa amani, sisi tunaendelea kujenga nchi yetu. Tumechelewa mno, tumepigwa sana, tumeliwa kwa muda mrefu; sasa tumepata mtu aliye serious kutuongoza tutoke kwenye hiyo hali, tutamuunga mkono na kumpa support kila iwezekanavyo oli tutoke kwenye hii hali. Sasa hivi hatuhitaji distractions zozote za kizembe.
 
Upuuzi wa aina yake huo. Msingi wa uchaguzi ni kuwapa wananchi fursa na mamlaka ya namna wanavyotaka kuongozwa hili halijafanyika. Wametangazwa kwa matakwa mtu mmoja. Basi aendelee kuteua wanaomuunga mkono na mauaji, mateso na kukanyaga katiba.
Ateue viti maalum toka CCM itakidhi matakwa ya kisheria.
 
...
 
Nipende kuwashukuru wote mliotoa michango yenu bila unafiki na kumshushua Pascal kwa unafiki aliouonyesha , anaouonyesha wote waliompa za uso bila huruma big up , Kati ya uliowataja ni nani alimwambia anashida na ubunge wa kuokotwa barabarani .

Nyinyi kaeni bungeni peke yenu muigeuze Tanzania kama ulaya . Muda sio mrefu mtajua madhara ya kumsukumiza wagonjwa wa bipolar disorder . Labda Kuna kitu watu hawakijui hii situation itawatesa CCM kuliko upinzani , usifikiri Wana CCM wanaipenda CCM kwa sababu ya rangi yake ya kijani au alama ya jembe na nyundo , walikuwa wanaipenda CCM kwa sababu ya maslahi , hivi una fikiri kwa uchache Nape , January , Kinana ,Makamba , Kikwete na wengine wengi bado wanaipenda CCM ?

Hata kuisikia hawataki ila hawawezi kujionyesha hadharani maana watakolimbwa .Jiwe hataki mtu yoyote yule apate hela anataka hela zote achukue yeye mpaka kodi za milango ya ofisi na viwanja vya CCM vinalipiwa kwenye akaunti hela zinaenda moja kwa moja kwa Jiwe na zamani ilikuwaje ? Unafikiri wanafurahi ?
 
Nilichojifunza kwenye hii post yako ni kwamba kumbe hamkujipanga kabisa na hili bao la mkono. Unapocheza draft lazima uwe unajua unavyotoa kete 2 uliwe una lengo la kula kete 5... Sasa wakati mnapora mkasahau kuacha angalau majimbo 30 ya upinzani, hata kwa Mbatia na Lipumba kama mlikuwa mmewakamia CHADEMA na ACT Wazalendo??? Sasa majuto ni mjukuu na kwa jinsi wananchi wanavyowajua wabunge wa chama chenu bungeni wanavyoboa, hata kama mkianzisha bunge live, mmeanza kujishtukia wenyewe.
 
Mimi ningeshauri hao wabunge wa upinzani walioshinda wajiunge tu na CCM na wapitishwe bila kupingwa!
Yule wa Chadema kule Nkasi naona ameshaanza kuota mapembe na kuanza kuvutana na viongozi wake, yanaweza kujirudia yale ya Sesil Mwembe ya kukingiwa kifua na viongozi wa bunge, let's wait and see.
 
Ukikosa akili kichwani kwako ujiandae kujazwa kila aina ya ujinga na upumbavu... Tumepata uhuru 1961 upinzani umeanza 1995 sasa jiulize kabla ya huo upinzani nini kilitufanya tusipige hatua za maendeleo?

Haya tokea 1961 mpaka leo nchi imeongozwa na Tanu/ccm lakini eti lawama ni wapinzani. Yaani ukiwa na majitu yasiyo na akili kama wewe ndiyo furaha ya watawala, na watakutawala huku wakipeana vyeo mpaka ushike adabu huku ukisugua matako.
 
Mpaka Leo una mawazo ya mtu kuuza inchi

Karne ya 21 bado unawaza kuuzwa

Ndio maana slogan ya lowasa ilikuwa ni ELIMU ELIMU ELIMU
Yaani mkuu mpaka naona aibu... Ila ukweli ni kwamba hawa ndiyo majority huko lumumba na ndiyo wanayoifanya kazi ya akina Bashiru na Pole pole kuwa rahisi.
 
Mkuu ukiona huyu bwana kaja na post kama hii jua kwamba huko ndani kwao linawatafuna maana hawakuwa wameangalia mbele kwenye mchakato wao wa bao la mkono... Wameanza kuona image mbaya itakayoonekana huko bungeni kwa outsiders na wadau wengine.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Anglia mbumbumbu lingine hili
 
CDM na ACT msidanganyike na kutudanganya kuwa mkikubali hiyo offer eti wakapatikane watu wa kupush ajenda ya kutaka/kuleta reforms kupitia mle bungeni, wote tunajua maamuzi ya bungeni huwa yanafikiwa kwa kupiga kura (Mara zote zikipingwa kwa ushabiki wa vyama, CCM vs vingine) Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi tz hakuna jambo ambalo serikali ya ccm italipeka bungeni likakwama au likapita kwa sababu kulikuwa na wabunge kadhaa wa upinzani, and vice versa (yaani upinzani tz tangu kuanzishwa kwako haijawahi kushinikiza Jambo lolote ile kubwa ambalo ccm wanilipinga/hawakubalini nalo likafanikiwa kupita bungeni)..

OTHERWISE kupata nafasi kadhaaa bungeni kwa ajili ya mshahara,posho na ruzuku ndio huwa lengo lenu japo mnajificha kwenye kutetea watz kwa kutaka reforms.

Nafasi hii CDM na ACT wanayopewa kufanya maridhio wanatakiwa waitumie vizuri kutokubali kugawiwa TU vyeo kama posho kwa yaliyo fanyika kwenye uchaguzi... Hakika hapa itadhihilisha upinzani tz Ni wasaka tonge kama ccm tu.

Badala yake waandae list ya demands kushikiza ccm na serikali kuitekeleza ili kufika maridhio na muafaka wa kitaifa wenye manufaaa ya muda mrefu kwa zaidi mtu mmoja mmoja au ya chama kimoja kimoja. Pia kukomesha haya yaliyotokea kwenye uchaguzi huu..

Demand list
1- kuvunjwa kwa NEC hii mara moja, ifanyiwe reforms ya muundo kuifanya iwe huru.

2- Polisi tz, ifanyiwe mabadiriko makubwa ya kuifunga isiweze kutumika kisiasa kunufaisha chama chochote.

3- Matokeo ya Rais tz yarusiwe kupigwa mahakamani,

4- Kufanyia marekebisho katiba haraka kunguza mamlaka ya Rais kuteua majaji ili kuongeza Uhuru wa mahakama,

5- Kupanga muda wa kumalizia mchato wa katiba mpya toka pale kwa rasimu ya Warioba... NB mchakato undelea Bila kuhodhiwa na wanasiasa Kama ilivyokuwa Hadi kupelekea ukakwama,

6- Ongezeaeni au kuboeesha haya.

Kukubali kupata viti kadhaa vya hisani bungeni itakuwa ni kujisaliti kwa msimo wenu kuwa mna hubiri mabadiriko/reforms.
Hakuna kipindi kizuri Cha kushinikiza ajenda/demand za upinzani Kama hiki ambacho mmeitwa mezani kujadiri kufikia mwafaka wa maridhiano,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…